Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
- Thread starter
- #21
Zemanda,Changamoto ni lugha yako mzee sio kwamba tunashindwa kuelewa unachosema ila msisitizo wako una msukumo wa udini.
Kwa mfano kwanini uniita hiyo association TAA halafu unasema washirika wake ni waislam? Kwani uislam ni kabila au dini? Hao watu kabla ya kuwatambua kama waislam unaweza kuwatambua kama watanganyika , wamatumbi,wahaya, wachagga,wasukuma,wakerewe au wazaramo,basi hata kwa jinsia zao uwaite wanaume ila kwanini utumie identity ya dini?
Basi tukubaliane hiyo TAA haikuwa taasisi ya kisiasa katika uhuru bali ilikusa ni organization ya kiislamu kutetea masilahi ya waislamu ya TANGANYIKA of which ukiiweka katika huo mtazamo tayari inakosa uhalali wa kuwa sehemu ya mafanikio ya taifa la watanganyika ambao misingi yetu haikubaliani na udini,ukabila wala ubaguzi wa rangi na ubaguzi wowote mwingine.
So nikuulize swali na unijibu chenga?
Uhuru wa TANGANYIKA kwa mtazamo wako ulikuwa ni movement ya kidini iliyofanywa na waislamu tupu halafu ilipofanikiwa wananyang'anywa na Nyerere?
Hivyo vyama vya awali vya wadai uhuru kwa ukoloni vilikuwa ni vyama vya kidini au kiimani au vya kiislamu?
Je,nyaraka za hivyo vyama zilikuwa na utambulisho upi? Utambulisho wa hili ni shirikisho au chama cha waislam wa TANGANYIKA au?
Hebu tupe ilmu.
Usiwajumuishe watu wengine kwa lugha ya wingi.
Naeleweka sana na vitabu vyangu vinapendwa sana.
Izungumzie nafsi yako.
Waasisi wa African Association walikuwa tisa na kati ya hao sita Waislamu.
Sababu ya hali hii ni kuwa Wakristo walikuwa wanaonywa wasijiingize katika siasa.
Haya kaeleza Kleist Sykes katika mswada wa kitabu cha maisha yake alichoandika kabla hajafariki mwaka 1949.
Hawa Waislamu katika African Association baada ya kuunda AA 1929 mwaka wa 1933 wakaasisi chama kingine Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika).
Hayo maswali yako yote nishayajibu:
View: https://youtu.be/5g_DMWsh_uE?si=efweuiGmZoGMy1gJ