Haya are the most intelligent people in Africa (Eastward) followed by Kikuyu in Kenya

Tarafa ya kiziba mkoani kagera wilaya mpya ya missenyi, ndiko sehem ambako wanapatikana maprofessa 1/3 ya maprofessa walioko Tanzania, sababu ni kama ifuatavyo
1. Wamisionary walikaa kule mapema , na ikawa sifa kwa aliyekuwa anasoma kama wamisionary hivyo watu wa kiziba wakawa na mwamko wa elimu mapema
2. Miundombinu ya elimu nchini Uganda ilikuwa imara zama zile ikapelekea wanakiziba kwa kuwa wapo maeneo ya kanyigo karibu na Uganda wasome kule maana wazazi wa zaman walitaman watoto wao waende shule ambazo kwa kusema ukweli huku hazikuwepo, ila wakaamua kuwapeleka Uganda,
3. Baada ya wao kupata elimu Uganda wakawa na mifumo ya kuanzisha shule mbalimbali za TARAFA, hazikuwa za kata zilikuwa za TARAFA nyingine mikononi mwa serikali japo zilijengwa na wananchi na nyingine za binafsi mfano, BWABUKI, BURUDEA, TWEYAMBE, KADEA, KABALE, MARUKU, MUGEZA, OMUMWANI , nk, hizi zilisaidia sana watu kwenda shule hata kama hawakuchaguliwa na serikali, hivyo ikasaidia kuongeza idadi ya wasomi
4. Kiziba wanasoma kwa ushindani na anasoma akiwa na role model wake mfano wao wanasoma ili wawe kama fulan aliyewatangulia
" ninesoma kule japo kwetu Mara ,baba yangu alikuwa ni mhasibu wa TANICA uko kagera hivyo ikalazimu niwe Kule kimasomo mpaka alivyostaafu" ila darasan ni kama ifuatavyo utasikia kila mmoja
Nasoma niwe kama TA RUGEJUNA,
Nasoma niwe kama na kazi ya TA MULOKOZI
Nataka nije niwe kama TA NDYANABO
nataka kusoma alivyosomea TA RWEGASIRA
na kwa kipindi hicho huyo ambaye unataka kuwa kama yeye akikusikia anakusaidia, hivyo ikaansha ari
5. Waliosoma mapema waliwasaidia ambao wamekwama hasa kwenye ada au kuwataftia shule,
Mfano mzee Balyagati ana program ya kusomesha watoto wasiopingia 1000 kwa mwaka mpaka vyio vikuu na kuwasomesha had PhD
Mzee Wellington George, ana wasomesha watoto wengi sana hasa pale hekima na tweyambe secondary na wengineo wengi
Kuna mifuko ya kusomesha watoto kama GSES, HEDEMORA PARTAGE na mengine

Hayo yote juu yamesababisha kiziba iwe juu na kupelekea kuwa wanapata PhD's wengi hadi professor,

Siku hizi asiyejua anaweza kudhan wahaya hawana ubabe tena kuelimu lakin watu hawa wapo sana mikoa mingine na majina walianza kuyabadili makusudi hawatumii ya kihaya kwa usalama wa elimu yao na Huduma hasa kutoka kwa wasiowapenda

Hivyo ndo mafanikio yako hivyo

Kiziba mpaka sasa wameshatoka si maprofessa tu Bali ukienda sehem inaitwa KIGARAMA KANYIGO KUNA MABIBI AMBAO KILA.NYUMBA WANAONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA, NA WAUME ZAO AU WATOTO WAO WANAISH ULAYA NA KWINGINEKO DUNIAN,

KIZIBA NDO UNAPATA NYUMBA ZENYE HADHI YA KUWA MJINI , KUNA NYUMBA ZIKO KULE HATA BUKOBA MJIN HAKUNA
 
Mi sio muhaya, ila hata bila hii takwimu:-

Hawa jamaa ni kweli wanajisifu kua wana akili na ni kweli wako vizuri sana Darasani.

Japo hawajui kutamka
L na R kwa ufasaha[emoji16][emoji16]
Heheheh RARA- LALA[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 

Mkuu,
Ahsante kwa maelezo mazuri, ambayo naamini kuwa hata sehemu zingine za Tanzania watachukua hatua ambazo tarafa ya Kiziba huko mkoani Kagera walizichukua kuhusu elimu miaka mingi iliyopita na kusaidia maeneo mengine ya Tanzania kuinua mwamko wa kielimu katika maeneo yao zaidi ya kampeni ya madawati na elimu bure.
 
Daaahh, kanyigo adi rahaa, je wengine vp?
 


TPB; Letisya Rutashobya ni Mngoni/Mmatengo; ameolewa na Mhaya.
 
Hao wote hawajasaidia chochote nchi hii..wanazidiwa na prof.muhongo kutoka Musoma na j.k.nyerere
 
Hapo mengi mtoe maana ni wa kawaida sana ...ila sifa ndo nyingi...mfano mzuri ni manji na mo
 
Sawa lakini kwa nini mkoa wenu bado ni one of the poorest in Tanzania? All the money is in KILIMANJARO BABY!
 
wangekuwa hata wazungu wana mawazo kama haya wasingefika hapa walipo
mawazo finyu ya mtoa mada ndio yanayozalisha umaskini
 
Sawa lakini kwa nini mkoa wenu bado ni one of the poorest in Tanzania? All the money is in KILIMANJARO BABY!

Mkuu, nenda ukatembelee vijiji vya Bukoba mjini na vijijini alafu urudi jamvini utwambie hali alisi uliyo ikuta huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…