Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Polisi walitumia nguvu kubwa mpaka ya akiba kuzuia kongamano la vijana wa CHADEMA kule Mbeya kwa kuwatenda unyama na kuwatweza vibaya viongozi wa kitaifa wa CHADEMA.
Kabla hakujapoa, Ngorongoro ikainuka, wamasai wakajaa barabarani kudai haki yao ya kutambuliwa kama raia huru wa nchi hii ambapo, walipinga vijiji na kata zao kufutwa na kusitishwa kwa huduma zote za kibinadamu maeneo hayo. Rais alitoa amri maisha yarudi kama kawaida baada ya shinikizo la siku kadhaa
Simiyu nako wananchi waliingia barabarani kudai haki yao ya usalama baada ya watu kadhaa kutoweka na wengine kuuawa na kutupwa. Maandamano hayo yalisababisha kifo cha Mtanzania mmoja. Hatujajua hatima ya wananchi wale kwa sababu hadi naandika uzi huu, jeshi la polisi ndo mtuhumiwa mkuu wa utekaji nyara, kutweza na hata kuua raia wasio na hatia. Mtu ataitwa polisi na kitakachojiri ni maiti yake kuokotwa porini....
Leo, tumeshuhudia Manyara, wananchi wamezuia magari wakiandamana kudai huduma ya maji safi na salama.....
Tunaendelea kushuhudia wananchi wakiamka usingizini kudai haki zao bila hofu.
CCM inazidi kubanwa kila kona huku chama hiko kikongwe kikiweka turufu yake kwa wasanii na influencers wa mitandaoni ambao hawana maadili wala mchango wowote kwa Taifa
Rais avunje Baraza la Mawaziri na kuteua upya. Hajachelewa
Muda si rafiki
Pia Soma
- Maandamano Makubwa Kata ya Olijoro Namba 5, Mkoani Manyara Wananchi Wafunga Barabara Kudai Maji, Polisi waingilia kati