Tuliomaliza shule wakati magroup ya whatsapp hayajaanza tulibadilishana mawasiliano tu..baadae teknolojia ikatukutanisha kwa sura zetu pichani na wengine hawaweki nyuso zao isipokuwa avatar au picha za wanawe nakadhalika. Kazi inakuwa na maswali pale lnapokuwa hamuonani na mnaanzisha group la malengo ya kusaidiana katika shida....
Michango inaanzishwa na mmoja anampoteza mazazi mnachangia kwa masikitiko makubwa japo hamujui ni kwa moyo wa kibinaadam na kuwiwa tu mnachangia 30k kila mmoja wengine hadi 50k
Kuna kitu nakiwaza tofauti japo si kwa nia mbaya kwamba baada ya miaka zaidi ya 10 mnauhakika gani hiyo.michango sio fraud? N muda mrefu na pesa ni mwanaharamu
Hata kama si fraud.
Mimi labda naamini sana watu kwenye misiba, sasa fraud inakujaje?.
Mtu anamuua mzazi ili mumchangie? Watu wanaenda kumkabidhi mfiwa rambirambi kwenye msiba, ina maana mfiwa ana fake msiba ili apewe rambirambi au fraud inakuwaje hapo?
Kwangu suala la fraud silioni sana.
Ila, hata kama si fraud, tujitengenezee utamaduni mwingine wa kujiwekea akiba na kujitosheleza wenyewe bila kuchangishanachangishana kila inapotokea msiba.
Kuna watu wengine sio big deal, kuna watu wengine mnawaumiza kwa michango ya kila mara. Hata ikiwa michango ni ya hiyari, kwenye macho ya wengi watu wanaona haya.
Pia, mimi nina allergy na vimichangomichango ya kila mara, inabidi watu wawe na fund ya kutoa pesa haraka hata kama inahitajika kwa dharula. Sasa hivi vimichango mpaka watu watafutane, wafukuzane, wahimizane, tarehe zikiwa mbaya mpaka wasubiri mwisho wa mwezi, karaha tupu.
Afadhali hata kuchanga kwenye mfuko kwa mwaka mzima. Halafu misiba ikitokea mna fixed amount mnaweza kutoa kwa kila member.
Mfuko kama huu utaondoa matatizo kama ya mtu kuchangia wengine na kutochangia wengine, jambo ambalo mara nyingine linaleta mgawanyiko.
Hivi kwa nini watu kama wa bima wasichangamkie watu kukata bima ya maisha? Kuna bima mpaka za vikundi, hivi vikundi vya shule havijui hii bima? Au hizi bima zina matatizo ambayo mimi ndiye siyajui?
Au ndiyo utamaduni wetu kuchangishana watu wajione wako pamoja? Maana kuna jamaa yangu mmoja alikataa kuchangiwa harusi, akasema kama kuna mtu anataka kuchangia harusi yake achangie kijiji cha Wamasai wapate maji, kwa ni nzuri tu asiwape watu mzigo wa kuchanga.
Lakini, kikichotokea ni kwamba, kuna watu walimsema kuwa anaringa na anajiona anaweza kumaliza gharama za harusi yake peke yake bila ya kuwapa watu nafasi ya kuchangia.
Wamakonde walisema "Ukichimama.nchale, ukikimbia nchale".
Ukichangisha lawama. Usipochangisha lawama.