GenuineMan
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 7,885
- 18,636
Daaah dadeki😭😭😭Kuna mama,
Mshahara wake ni chini ya laki tatu, anaishi na watoto wa kijana yake ambae ashafariki.
Watoto bado wanasoma.
Basi yeye na mme wake wamepambana weee mpaka wamesimamisha nyumba ya kuishi huko mbele ya mbagala huko. Nje ya jiji la DSM.
Nyumba ni zakawaida tuu. Za kipato cha chini.
ile wameamia tuu hata miezi miwili haijaisha.
Ardhi ya lile eneo ikaanza kupasuka, nyumba nazo zitengeneza nyufa kubwa tuu.
Kila siku nyufa zinaongezeka.
NYumba ikawa haiwezi kukalika tena.
Imebidi warudi tena kwenye nyumba ya kupanga.
Fikiria mali, muda, damu na jasho waliyotumia kujenga nyumba halafu imekuwa ghofu ghafra.
Umaskini ni kama ndio shetani mwenyewe.
Umeshasema lazima uingie gharama kwenye msingi, baada ya kozi nne tena na hapo kuna lenta.Mwandege, Vikindu, Kisenvule ardhi yake ni mchanga mwingi hivyo ujenzi wake lazima uingie gharama kwenye msingi, baada ya kozi Nne na Linta bila hivyo nyumba inageuka chujio la chai.
Hapo sio umasikini ila kujenga bila kufuata kanuni
Na Mimi ndipo nashangaa mtu anakimbia nyumba yake kisa nyufa..?. 🤔🤔🤔Niliwai kukaa Nyumba ambayo Haina madilisha ni pazia tu in December mvua zimekazana balaa ilikuwa ikifika usiku tunawaza na familia
Ile tumelala tu mvua ya upepo mkali hamna madilisha tunaamka tunashikilia mapazia na mikono kwakubana ukutani 🥺 uku mwingine akipiga deki maji yanayo pita chin ya mlango mpaka upepo utulie then tunakamua zile pazia
But alhamdullilah🤲🤲 yalipita yote kwa neema yake alie juu.
Bila ku solve tatizo utahangaika sanaNa Mimi ndipo nashangaa mtu anakimbia nyumba yake kisa nyufa..?. 🤔🤔🤔
Ila siyo hii ya kukimbia nyumba kisa nyufa 😃😃😃Kuna wakati unaweza kupitia changamoto nyingi ktk maisha mpaka ukajisemea Mungu kanifungia vioo nini?