Haya majamaa yatatuzika kabisa game ya mzunguko wa pili

Haya majamaa yatatuzika kabisa game ya mzunguko wa pili

Pettymagambo

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2017
Posts
1,490
Reaction score
8,227
Kiukweli hawa watu wanatimu bwana, niseme wazi game ya mzunguko wa pili ya watani, sisi SIMBA yaani dakika 90 tutaziona kama mwaka, yaani hazitimii.

Pamoja na kuchukizwa na matokeo ya leo, ila nasema timu pekee inayoweza kuwapa tabu hawa Yanga labda Mamelod pekee, na Al Ahly asipochunga game ya mwisho anaweza akalowa palepale Cairo.

Hongera Yanga.
Hongera injinia Hersi.
Hongera mashabiki wa Yanga, japo roho inaniuma kuona sisi SIMBA tunaendelea kuokoteza mizigo ya wachezi tangu kusepa kwa Hanspope, sioni kiongozi kwetu mwenye nia ya kuipeleka timu kwenye kilele cha furaha kama ilivyo kwa injinia Hersi!

Hawa watu wakiamua wanaweza kutupiga hata 7-0 nipo hapa njooni mnitukane washabiki hobhelahobhela.
 
Hakuna jipya...!

Horoya alikufa 7 - 0 hatua hizo msimu uliopita kwa Mnyama.
 
Muhimu tu muingie tena kwenye mfumo wao. Hakika historia inaweza kujirudia tena. Ila msipoingia, basi siku zote mechi hugeuka kuwa ngumu sana kwa Wananchi.

Yaani ukitaka kuidhibiti Yanga, jitahidi tu akikufunga goli la utangulizi, hakikisha huruhusu goli la pili! Na ukishafikia hatua hiyo, paki basi na utafute goli la kusawazisha. Ukiruhusu tu goli la pili, basi mpira unakuwa umeisha kwa upande wako.
 
Umemkosea kumtukana namna hiyo kisa tu mpira. Hayo ni maoni yake, kwani tofauti ni ipi kati ya waarabu na Horoya? Au kwakuwa Yanga mmewafunga? Ni vibonde tu kama wengine.
 
Nasisitiza....!

Hakuna Jipya Kwa Utopolo...!

Ni juzi tu Wydad Casablanca Kafa 2 nil Kwa Mnyama...!

Nakumbusha tu Wydad ni wa pili Kwa Ubora Afrika itakuwa CRB..!
 
Back
Top Bottom