Haya majina huwa yanatumika visivyo sana

Haya majina huwa yanatumika visivyo sana

Kaka ngoja nikusaidie kitu

Umesema 0-17 utambuliso wao huwa ni mvulana na msichana hapa huwa tunawatambua kuwa ni watoto ambapo tuta wagawanya kwa makundi kulingana na jinsia zao mfano wenye umri 15 tutawaita watoto wakikume au wakike kulingana na umri wao kuwa ni mdogo na kisheria kuwatambua kama watoto

Ukija kwa wenyw umri 18-35 hawa kwa ujumla tunawatambua kama vijana ambapo tutawagawanya kwa majina kuwa msichana na mvulana kwa kuamini hawa wote hawaja oa wala kuolewa na kuzaa lakini kama akizaa au kuoa na kuwa na familia basi tutawatambua kama mwanaume na mwanamke na sio msichana na mvulana

Hapo umenielewa
 
Rejea kwenye asili ya neno BINTI

Sisi tumelikopa tu kutoka lugha ya Kiarabu, neno binti halikutokana na kibantu.

Na maana yake inaeleweka.
 
Dah, ama kweli elimu yetu inahitaji kufumuliwa na kurekebishwa ili tusiwe na wahitimu ambao hawana uwezo wa kuchambua mambo na kuyarekebisha.

Wewe unaonekana hata darasani ulikuwa unameza tu definitions na haukuwa na uwezo wa kutengeneza definition yako kamili.

Nime elezea vizuri kabisa kule juu labda kama hauelewi na hauna uwezo wa kusoma kiswahili vema.

Nimesema vema kule juu kuwa Unaposema Kijana unakuwa unamuongelea mwanaume wa rika la umri ambao nimeelekeza pale juu.

Kimsingi, jamii inatabia ya kutumia maneno kwa mapokeo. Ukienda hata kwenye vitabu vinamwita mwanadamu MAN. kwasababu kihistoria mwanadamu aliyeumbwa ni Mwanaume na mwanamke alitengenezwa kama ubavu wa huyo mwanaume so mwanamke huwa hachukuliwi kama mwanadamu kamili kimaagano.

Sasa ukija katika rekodi za mapokeo ni kuwa wanaume wa umri mdogo yaani vijana ndio wamekuwa wakitumika katika platforms mbali mbali za kisiasa, kiuchumi, kisayansi na mengineyo. Miaka hii mabinti nao wameanza kuingia ila wanakuta documents zote zinatumia neno vijana kumaanisha washiriki wa umri chini ya watu wazima.

Sasa imekuwa adopted hivyo hivyo ila mimi nataka tupate kupeana elimu kuwa documents zinabidi kusoma vijana na mabinti kama vile zinavyosema wanaume na wanawake.

Ndio maana hata ukienda katika medani ya mashujaa utaona siku hizi kuna neno Sheroes limeongezwa kwa maana ya mashujaa wakike ambapo zamani lilitumika neno Heroes sasa wanawake wanaona hili neno kwao haliwatambulishi vema.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Nakubaliana nawe elimu yetu inahitaji kufumuliwa kwa sababu wewe huelewi kuwa hata binti anaweza kuwa kijana.

Nakwambia hivi, hiyo definition yako ya kijana kuwa ni mtu mume ni mbovu na si Kiswahili fasaha, mnatuharibia lugha.

Hutakiwi kuanza kujiwekea definitions zako tu, mwisho utatuambia mzee ni mtoto mchanga asiyezidi miezi sita.

Kijana ni mtu ambaye amevuka utoto lakini hajafikia uzee. Anaweza kuwa mtu wa kike au kiume.Full stop.


Ukitaka kulazimisha kijana awe mtu wa kiume, unajionesha lugha huijui, unalazimisha tu.

Kinyume cha binti ni bini, au mvulana, si kijana.

Kwa sababu hata binti anaweza kuwa kijana.

Ni kipi usichoelewa hapo?
 
Wataalam au wataalamu?
Uzi wako ungekuwa mzuri kama usingedanganya.
Kijana ni yeyote aliyepo umri wa kati au msichana au mvulana.
Acha kupotosha watu na epuka ukali.
Huyo jamaa ana dalili za ugonjwa wa akili wanasaikolojia wanauita "delusions of grandeur".

Ni tabia fulani ya kujiona wewe uko zaidi, mtaalamu, mkubwa sana, wakati huna lolote.

Mtu hajui hata maana ya kijana tu halafu anakuja hapa kujishebedua?
 
Mianagenzi jahili, ilojivika stahili
Kuharibu Kiswahili, tumezishika dalili
Tukipiga usaili, kupitia ushairi
Kujikuza mafaili, kujitia umahiri

Mianagenzi mitwana, tunayo ana kwa ana
Twaipiga kwa spana, hapahapa twaibana
Asomjua kijana, huyo jambo lake hana
Anapiga danadana, goli hatofunga kana

Kujipa utaalamu, kwa kalamu ya haramu
Ni sawa uchakaramu, usiokwisha awamu
Amkia kwa salamu, upate sifa dawamu
Ujenge zako fahamu, majinuni wa sanamu

Barawa mpaka Lamu, Mvita hata Mrima
Maungwana wana hamu, sio vita kurindima
Kuungana binadamu, kujikita kwa heshima
Kupatana bila zamu, kujishika kwa hekima

Sio ubaya kwa inda, na kujikuza uledi
Tafuta hidaya kinga, ya kujifunza wenyeji
Weka yako kaya kinda, ya kujitunza weledi
Nyoosha palipopinda, kama fundi wa gereji

Jiepushe na umwamba, uso bichwa wala guu
Utajifunga kwa kamba, uteleze chini puu
Ukajitoa muhanga, bure bilashi ukuu
Ukautoa upanga, kuviasi vijukuu

Kaditama nimefika, beti saba zakutosha
Nimezoza Kiafrika, keti muosha huoshwa
Pomoni sitafikika, kiasi sijapotosha
Lugha yetu yatukuka, johari isiyochosha
 
Natumai nyote muwazima wa afya ya akili na mwili. Leo napenda kuweka sawa matumizi sahihi ya majina haya haya ambayo yamekuwa yakitumika visivyo kuwakilisha rika na jinsia ya kundi husika la watu.

Kama kweli lugha ya malkia yaani English, kuna majina huitwa collective nouns ambayo hutumika kwa kundi bila kubagua tofauti zake. Mfano ukisema children unakuwa umelenga group la watoto bila kusema umri, rangi, jinsia au tofauti zao zingine. Halafu kuna specific nouns ambazo hutumika kulenga specific group ya watu mfano ukisema "one month african baby boys" hapo unakuwa very specific.

Sasa naomba turudi kwenye hoja yangu ambayo imebidi kuiandikia uzi leo baada ya kuona kuna upotofu kama sio mkanganyiko katika matumizi sahihi. Kumekuwa na mkanganyiko wa kimatumizi kwenye jina Kijana. Neno kijana nimeona likitumika kinyume miongoni mwa wana taaluma, viongozi na taasisi kumaanisha mtu wa umri mdogo jambo ambalo ni sahihi kwa upande m'moja ila sio sahihi kwa upande mwingine.

Ni sahihi kwasababu ni kweli kijana ni mtu wa umri mdogo katikati ya mtoto na mtu mzima. Lakini si sahihi kumwita mtu umri mdogo wa jinsia ya kike kijana sababu sio jinsia yake. Mtu wa umri mdogo wa jinsia ya kike huitwa binti.

Sasa leo nikaona niweke kumbukumbu sawa na kurekebisha huu upotofu ambao hata hawa watu wa serikalini na viongozi wengi wamefeli kurekebisha ili kuweka sawa matumizi ya misamiati ya lugha yetu ya taifa.

1. Katika kundi na watu waliopo umri kuanzia miaka 0 hadi 17, jinsia ya kiume huitwa MVULANA na jinsia ya kike huitwa MSICHANA. Hii ni kwa mujibu wa standards za kimataifa ila huwa tofauti kulingana na tamaduni tofauti.

Kwa mfano kwa standards za kimataifa mtu nzima huanzia miaka 18 kwenda juu ila ukija afrika ni tofauti, mtu wa kike akivunja ungo tu kwa maana kuona hedhi yake ya kwanza papo hapo hiyo uchukuliwa kuwa ni ameshaingia utu uzima na si MSICHANA tena bali ni binti. Na mtu wa kiume akishaanza kuonyesha dalili za kupevuka au balehe then huyo huchukuliwa ni mtu mzima na si MVULANA tena bali ni Kijana.

2. Katika kundi la watu kuanzia umri kuanzia miaka 18 hadi 35, jinsia ya kiume huitwa KIJANA na jinsia kike huitwa BINTI. Hii ni kwa mujibu wa standards za kimataifa ila huwa tofauti kulingana na tamaduni tofauti.

Kwa mfano kwa tamaduni za mataifa mengi ukitoa mataifa ya kimagharibi kama US, UK, Canada etc, kwa sisi Africa, Asia, Arabic huwa vijana na mabinti wanaooa na kuolewa katikati ya umri huu huondoka katika kundi hili la vijana na mabinti na kuwa mtu mume mtu mke yaani wanaume na wanawake.

So kwa mfano unaweza kuta mtu amefika miaka 35 hajaolewa wala kuoa huyu hawezi endelea kuitwa kijana au binti bali ataitwa mwanaume au mwanamke basi. Ila kama katika umri huo umemkuta ameoa au kuolewa title yake itakuwa Bwana na bibi. Yaani bwana fulani au bibi fulani.(bibi haimaanishi umezeeka maana watu mtashtuka hapa[emoji23][emoji23])


So ukitazama hadi hapo utaona kuna mtiririko huu ufuatao.

Umri 0 hadi 17 = MVULANA/MSICHANA
Umri 18 hadi 34 = KIJANA/BINTI (kwa wasio ndani ya ndoa)
Umri 35 hadi 55 kuendelea = Bwana /Bibi

Natumai hadi hapa nimeweka rekodi sawa na kuondoa utata wa matumizi ya haya majina. Lakini pia kuna majina mengine ambayo hutumika kama status mfano mume na mke. Hawa ni wanandoa. Ila sio wahuni wawili wanaishi pamoja wajiite mume na mke hao ni kijana na binti mwamflani.

Anyways, nakaribisha maswali kwa ufafanuzi zaidi.
Ninavyoelewa ni kwamba mtoto ye yote wa kike ni 'binti' daughter, ndio maana huku pwani wana Bit. Juma yaani mtoto aliyezaliwa na Juma hata kama ni mtu mzima; binti linaonesha ni mtoto (wa kike) wa fulani, yaani kazaliwa na fulani; kwa mwanume tunaitwa 'mwana' -son yaani mtoto wa kiume wa fulani ingawa hili halitumiki sana, ila ndivyo linavyopswa kutumika. Labda Wanyakyusa huenda ndio maana 'Mwa' yaani Mwakyusa kifupi cha mwana wa Kyusa; Mwakipesile kifupi cha mwana wa Kipesile. Ingawa kwao neno Mwana linahusu jinsia zote.
Neno 'mwanamke' woman ni mtoto ye yote wa jinsia ya kike bila kujali umri kuanzia mtoto mdogo hadi mtu mzima na 'Mwanaume' man, ni mtoto ye yote wa kiume kuanzia kuzaliwa mpaka mzee anaitwa hivyo.
Kijana 'Youth' na ni mtu ye yote wa jinsia ya kike au ya kiume mwanye umri nafikiri miaka 12 (anapobalehe kwa mwanaume na kwa mwanamke anapovunja ungo) hadi hiyo 35. Mvulana na msichana pia yanaweza kutumika kwa kwa mtoto wa kiume au kike wa miaka 12 -18 na kwa msichana pia. Haya yanaingiliana ila unaweza kutofautisha unapotaja kuonesha umri au maelezo unayotakakuyatoa kuhusu huyo mtu. Haina maana huyo msichana huwezi kumwita mwanamke, au 'binti' wala mvulana huwezi kumwita mwanamume, au 'mwana' au huwezi kumwita binti. Ni heshima yao kuitwa hivyo
 
wameshindwa*

¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤

Hutegemea ukomavu (maturity) wa mhusika:

  • Asiyekomaa ni mtoto: mvulana ama msichana
  • Aliyekomaa ni mtu mzima: mwanaume ama mwanamke
  • Anayeelekea kukomaa ni kijana: jinsia zote

Source: common sense 😀
 
Back
Top Bottom