Haya majina huwa yanatumika visivyo sana

Kaka ngoja nikusaidie kitu

Umesema 0-17 utambuliso wao huwa ni mvulana na msichana hapa huwa tunawatambua kuwa ni watoto ambapo tuta wagawanya kwa makundi kulingana na jinsia zao mfano wenye umri 15 tutawaita watoto wakikume au wakike kulingana na umri wao kuwa ni mdogo na kisheria kuwatambua kama watoto

Ukija kwa wenyw umri 18-35 hawa kwa ujumla tunawatambua kama vijana ambapo tutawagawanya kwa majina kuwa msichana na mvulana kwa kuamini hawa wote hawaja oa wala kuolewa na kuzaa lakini kama akizaa au kuoa na kuwa na familia basi tutawatambua kama mwanaume na mwanamke na sio msichana na mvulana

Hapo umenielewa
 
Rejea kwenye asili ya neno BINTI

Sisi tumelikopa tu kutoka lugha ya Kiarabu, neno binti halikutokana na kibantu.

Na maana yake inaeleweka.
 
Nakubaliana nawe elimu yetu inahitaji kufumuliwa kwa sababu wewe huelewi kuwa hata binti anaweza kuwa kijana.

Nakwambia hivi, hiyo definition yako ya kijana kuwa ni mtu mume ni mbovu na si Kiswahili fasaha, mnatuharibia lugha.

Hutakiwi kuanza kujiwekea definitions zako tu, mwisho utatuambia mzee ni mtoto mchanga asiyezidi miezi sita.

Kijana ni mtu ambaye amevuka utoto lakini hajafikia uzee. Anaweza kuwa mtu wa kike au kiume.Full stop.


Ukitaka kulazimisha kijana awe mtu wa kiume, unajionesha lugha huijui, unalazimisha tu.

Kinyume cha binti ni bini, au mvulana, si kijana.

Kwa sababu hata binti anaweza kuwa kijana.

Ni kipi usichoelewa hapo?
 
Wataalam au wataalamu?
Uzi wako ungekuwa mzuri kama usingedanganya.
Kijana ni yeyote aliyepo umri wa kati au msichana au mvulana.
Acha kupotosha watu na epuka ukali.
Huyo jamaa ana dalili za ugonjwa wa akili wanasaikolojia wanauita "delusions of grandeur".

Ni tabia fulani ya kujiona wewe uko zaidi, mtaalamu, mkubwa sana, wakati huna lolote.

Mtu hajui hata maana ya kijana tu halafu anakuja hapa kujishebedua?
 
Mianagenzi jahili, ilojivika stahili
Kuharibu Kiswahili, tumezishika dalili
Tukipiga usaili, kupitia ushairi
Kujikuza mafaili, kujitia umahiri

Mianagenzi mitwana, tunayo ana kwa ana
Twaipiga kwa spana, hapahapa twaibana
Asomjua kijana, huyo jambo lake hana
Anapiga danadana, goli hatofunga kana

Kujipa utaalamu, kwa kalamu ya haramu
Ni sawa uchakaramu, usiokwisha awamu
Amkia kwa salamu, upate sifa dawamu
Ujenge zako fahamu, majinuni wa sanamu

Barawa mpaka Lamu, Mvita hata Mrima
Maungwana wana hamu, sio vita kurindima
Kuungana binadamu, kujikita kwa heshima
Kupatana bila zamu, kujishika kwa hekima

Sio ubaya kwa inda, na kujikuza uledi
Tafuta hidaya kinga, ya kujifunza wenyeji
Weka yako kaya kinda, ya kujitunza weledi
Nyoosha palipopinda, kama fundi wa gereji

Jiepushe na umwamba, uso bichwa wala guu
Utajifunga kwa kamba, uteleze chini puu
Ukajitoa muhanga, bure bilashi ukuu
Ukautoa upanga, kuviasi vijukuu

Kaditama nimefika, beti saba zakutosha
Nimezoza Kiafrika, keti muosha huoshwa
Pomoni sitafikika, kiasi sijapotosha
Lugha yetu yatukuka, johari isiyochosha
 
Ninavyoelewa ni kwamba mtoto ye yote wa kike ni 'binti' daughter, ndio maana huku pwani wana Bit. Juma yaani mtoto aliyezaliwa na Juma hata kama ni mtu mzima; binti linaonesha ni mtoto (wa kike) wa fulani, yaani kazaliwa na fulani; kwa mwanume tunaitwa 'mwana' -son yaani mtoto wa kiume wa fulani ingawa hili halitumiki sana, ila ndivyo linavyopswa kutumika. Labda Wanyakyusa huenda ndio maana 'Mwa' yaani Mwakyusa kifupi cha mwana wa Kyusa; Mwakipesile kifupi cha mwana wa Kipesile. Ingawa kwao neno Mwana linahusu jinsia zote.
Neno 'mwanamke' woman ni mtoto ye yote wa jinsia ya kike bila kujali umri kuanzia mtoto mdogo hadi mtu mzima na 'Mwanaume' man, ni mtoto ye yote wa kiume kuanzia kuzaliwa mpaka mzee anaitwa hivyo.
Kijana 'Youth' na ni mtu ye yote wa jinsia ya kike au ya kiume mwanye umri nafikiri miaka 12 (anapobalehe kwa mwanaume na kwa mwanamke anapovunja ungo) hadi hiyo 35. Mvulana na msichana pia yanaweza kutumika kwa kwa mtoto wa kiume au kike wa miaka 12 -18 na kwa msichana pia. Haya yanaingiliana ila unaweza kutofautisha unapotaja kuonesha umri au maelezo unayotakakuyatoa kuhusu huyo mtu. Haina maana huyo msichana huwezi kumwita mwanamke, au 'binti' wala mvulana huwezi kumwita mwanamume, au 'mwana' au huwezi kumwita binti. Ni heshima yao kuitwa hivyo
 
wameshindwa*

¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤

Hutegemea ukomavu (maturity) wa mhusika:

  • Asiyekomaa ni mtoto: mvulana ama msichana
  • Aliyekomaa ni mtu mzima: mwanaume ama mwanamke
  • Anayeelekea kukomaa ni kijana: jinsia zote

Source: common sense 😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…