Haya majina tusiwape newborn (watoto)

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Ndg wana MM,

Kwa uzoefu nilioupata baada ya kuishi hapa duniani miongo kadhaa nimegundua kuwa watu wenye majina kama Shida, Tabu, mawazo, siamini, Mwaka mbaya, Sura mbaya, Sikitu, Tatizo na mengine yanayofanana maisha yao huwasumbua sana.

Hivyo "TUACHE KUWAPA WATOTO MAJINA HAYA"

Unaweza kutaja na mengine.
 
Hivi kuna watu wanaitwa Mwaka Mbaya na Sura Mbaya?

Halafu, hivi hayo majina kama Tabu, Mawazo, na mengineyo ya hivyo mara nyingi huwa ni ya Waislam eeh, au nimekosea?

Kama ni hivyo huwa najiuliza kwa nini....

Mwingine anaitwa Mkejina, habari, neno, sabuni, chausiku
 
Fikirini, Havinitishi, Havijawa, Chausiku, Zinduna...
 
Mwingine anaitwa chuki, mke jina , dharau, sikitu n.k
 
sikitu, liziki, mwanjaa, mwaka, chausiku, mwanvua, yako mengi tuu.
 
wewe unasema tusiwape watoto majina haya
lakini ndio majina yayoendana na matukio. mimi sioni sababu ya kuyakandia. nanikama kumbukumbu. na sikwamba eti mtoto atakuwa anaishi maisha yanayofanana na jina lake si kweli hiyo. mfano mtoto anaitwa shida eti na yeye atakuwa hivyohivyo? laasha. mfano mwingine mwamvua na yeye atakuwaje? atakuwa anatabia ya mvua?
 

Mkosasura,SIOGOPI,HAVINTISHI,
 

We umeangalia haya ya kiswahili tu! je ya kilugha kama
1: Lulanzi kwa wahehe ulanzi.
2: Marwa kwa wakurya pombe
3: Warwa kwa wasukuma pombe nk. hiyo n mifano michache bado ya wachaga wanyakyusa wangoni(mapunda) wasambaa waruguru(kobelo) kizungu Bold nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…