Haya mambo ya kupangiana kucheza usiku TFF mwisho ikatae kuburuzwa

Haya mambo ya kupangiana kucheza usiku TFF mwisho ikatae kuburuzwa

Anonymous Caller

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Posts
1,434
Reaction score
1,930
Sisi ndio Host kwenye haya mashindano...na mwenyeji ana haki zake...
Haki zake ni pamoja na kuhusishwa kupanga muda sahihi wa mechi kuchezwa katika nchi yake.

Kucheza saa mbili usiku sio desturi yetu...hili ni jambo geni..na hata inapotulazimu kucheza bas iwe as emergency...isiwe ndio mazoea...CAF wanatakiwa kuheshimu hilo.

Na Haya mambo huenda wakati mwingine yanasababishwa na upole wa TFF......
Leo TFF wanalalamikia mahudhurio hafifu uwanjani wakati wanajua fika muda wa saa mbili sio rafiki kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi....

kwasab mechi za makundi tayari zimemalizika...haipo tena sababu ya kucheza usiku, wakati fixture inaonyesha kutakuwa na mechi moja tu Kwa kutwa.

Juzi Kenya Kamtia adabu Morocco baada ya mechi yake kuchezwa saa TISA....kenya alishinda akiwa na Red card ya mapema tuu.

Iweje Kenya aruhusiwe kucheza muda aliojipangia na Morocco halafu ishindikane kwa Tanzania ambaye naye ni mwenyeji pia?

Haya mapelekesho ni ya kuyakataa kwa hoja kama hizi.

Kwanini Mamelodi mechi zake anacheza jioni tu.
Uliwahi kuona lini Tp mazembe akicheza usiku pale lubumbashi?
Tofauti ya muda wao na hapa kwetu ni saa 1 tu.

Juzi kule marekani kwenye Fifa Club World cup mliona mechi zilikuwa zikichezwa jua la saa 8 kwa majira ya kule...na watu walicheza.

Nakumbuka kuna siku tuliwahi kucheza na Tunisie saa 4 usiku kwasababu za kipuuzi kabisa.
Mbona nchi nyingine hazifanyiwi hivi.

Kama ni uenyeji wa CHAN hata Rwanda alishawahi kuwa host kama sie ila hakuwahi kupangiwa ovyo kucheza muda kama wetu.

Tukutane ijumaa saa kumi kwa mkapa.
 
Yanga kabla haijahamia uwanja wa KMC, mechi zake zote ilikuwa inapendelea kucheza usiku. Hata sasa watu wamekuwa wanaomba uwanja ufungwe taa ili mechi zipigwe usiku. Kitu ambacho mlikuwa mnakitaka wenyewe kwa sababu zenu wenyewe leo mnaona ni figisu. Tena mkipeleka mechi saa 8 mchana ndiyo kabisaaa majukwaa tayakauka.
 
Back
Top Bottom