Haya maneno yangeingia rasmi kwenye kamusi ya kiswahili

Haya maneno yangeingia rasmi kwenye kamusi ya kiswahili

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Tarehe 30 september kila mwaka ni siku ya utafsiri duniani. Tunaotafsiri vitabu tunapata shida sana kwa kukosekana kwa maneno rasmi ya kuelezea maana fulani.

Lakini mtaani utakuta kuna maneno mazuri yanayoelezea jambo hilo vizuri sana. mfano.
1. Neno la kiingereza MEAN/MEANNESS. Halina tafsiri rasmi nzuri ya kiswahili. Lakini mtaani neno KAUZU/UKAUZU ni tafsiri nzuri na yenye kueleweka.

2. Neno FANATIC/FANATICISM. Neno hili halina tafsiri nzuri rasmi ya kiswahili, lakini mtaani tuna neno UNAZI (Kutokana na NAZISM) linatafsiri vizuri sana neno hili. mifano ni mingi.

Ni wakati wa kuangalia uhalisia zaidi kuliko urasmi.
 
Back
Top Bottom