Haya masuala nayahusisha na ukosefu wa Utawala Bora

Haya masuala nayahusisha na ukosefu wa Utawala Bora

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,227
Reaction score
6,670
Hivi karibuni, na hadi sasa, kuna mijadala ya kisiasa ambayo kimsingi chimbuko lake ni utawala bora. Baadhi ya mijadala ni pamoja na:

[emoji830]︎ Madai ya Katiba mpya;
[emoji830]︎ Utawala wa sheria;
[emoji830]︎ Tozo;
[emoji830]︎ Wasiojulikana;
[emoji830]︎ Mashtaka ya kisiasa;
[emoji830]︎ Kuonezeka kwa uhalifu km Panya "road"; nk.

Kwa mtazamo wangu haya masuala nayahusisha na ukosefu w Utawala Bora hasa kutokutumia mamlaka za ngazi za chini ambazo ni Serikali za Mitaa na Kijiji. Kwa mfano:

[emoji830]︎ Bajeti ya Taifa huandaliwa pasipo kushirikisha Wananchi kupitia Serikali zao za Mitaa/Vijiji. Wananchi wanapaswa kukutana na kuandaa bajeti zao ambazo zitakuwa msingi wa Bajeti ya Taifa. Ushahidi ni michango ya Wabunge wakati wa Kikao cha Bajeti ambapo Wabunge wengi hutoa maombi kuhusu mahitaji katika majimbo yao; na
[emoji830]︎ Ni katika Serikali za Mitaa/Vijiji ambapo kila mkazi anajulikana kiasi cha kujua tabia ya kila mmojawapo kuweza kuthibiti matendo ya uhalifu.

Ushauri

Ili Viongozi wa Serikali za Mitaa/Vijiji waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo, madaraka na mamlaka yao yaainishwe kwenye Katiba ya JMT. Iliyopo kwa sasa, Ibara ya 61, inawapa tu Wakuu wa Mikoa wajibu na mamlaka.
 
Back
Top Bottom