Haya matamasha ya kikabila ni janga la Taifa: sasa hivi Wanyakyusa wako ITV

Haya matamasha ya kikabila ni janga la Taifa: sasa hivi Wanyakyusa wako ITV

Doslamari

New Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
4
Reaction score
1,499
Hivi vinavyoitwa matamasha ya kikabila yanayojitokeza kwa kasi siku hizi havina afya ktk kujenga umoja wa kitaifa. Kuna ajenda gani imejificha humu? Walianza wasukuma, halafu wanaigana utafikiri sifa kumbe ni janga. Karne hii watu mnatukuza ukabila? Mnaunda vikundi vinavyohamasisha ubaguzi? Viongozi wakuu mpo mnawakodolea macho mnafikiri wanafanya jambo la maana? Eti utamaduni tunataka utamaduni wa kitaifa.
Wanyakyusa wanasifika kwa ukabila, kuna wakati walijazana NBC lugha rasmi ofisini ilikuwa kinyakyusa wakaiua NBC kupelekea kuuzwa. Serikali ikemee hivi vikundi kabla haijachelewa, maadui wa Taifa hupenyezea ajenda zao humu.
 
Wanyakyusa wapo kila siku, tunajua mkoa wanatoka na tabia zao. Tunaishi nao mitaani, tunashiriki nao mambo ya kijamii kila siku na hakuna lililoharibika. Sidhani kama kufanya tamasha lao kupitia TV ndio kutawafanya Sasa wajione wapo kwenye jamhuri yao.

By the way Mimi ni mngoni usije ukadhani nimeandika kwa sababu ni mnyakyusa.
 
Mbona wakati wanajazana mi sikuwepo... Irudiwe irudiwe nipate kaz mi jobless.
Anyway huwa nafikir kma wew, siku hizi kuna vichama chama ving ambavyo havina msingi bahat mbaya vichama hiv au viumoja hiv vimeingia mpaka kwenye nyumba za ibada. Utakuta watu wa mkoa X wako busy at utasikia umoja wa watu wanaotoka mkoa Y. Najua nia njema wanayo hasa wengi ni kusaidiana katika mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ila kwangu huwa naona haina afya sana kwa mustakabar wa Umoja wa Taifa letu kw siku za Usoni
 
Sijawahi kuona mnapinga sherehe za krismasi, Eid au diwali.. zote hizo za kizungu, kiarabu na kihindi.
Wanyakyusa na wasukuma kupiga Ngoma zao tu, muafrika mwenzao ushaanza kulalamika eti ukabila!
Kuna ukabila gani hapo?
Wametoa hate speech yoyote?

Tujiheshimu na tuache kudharau mila zetu.

Na tutaanzisha cultural carnivals kusherehekea tamaduni zetu za kiafrika..
Nyie wazungu pori na waarabu Koko mjinyonge tu.
 
Mbona wakati wanajazana mi sikuwepo... Irudiwe irudiwe nipate kaz mi jobless.
Anyway huwa nafikir kma wew, siku hizi kuna vichama chama ving ambavyo havina msingi bahat mbaya vichama hiv au viumoja hiv vimeingia mpaka kwenye nyumba za ibada. Utakuta watu wa mkoa X wako busy at utasikia umoja wa watu wanaotoka mkoa Y. Najua nia njema wanayo hasa wengi ni kusaidiana katika mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ila kwangu huwa naona haina afya sana kwa mustakabar wa Umoja wa Taifa letu kw siku za Usoni
Siyo NBC peke yake hata bima walijazana
 
Nchi hii walioanza kuongoza walihakikisha wanaondoa ukabila na kujenga umoja wa kitaifa.
Ila upepo mdogo walionao viongozi wa Sasa ndio unarudisha ukabila ndio maana unaona machifu wamepewa kipaumbele Ila watu wakizungumzia Tanganyika inaonekana dhambi.
 
Back
Top Bottom