Huu hapaKuna uzi kama sikusei wewe ndio uliuanzisha miaka kadhaa nyuma ulikuwa ukihusiana na camouflages.. Something like that. Tukipata link itapendeza.
Nimeona kama hii mada ulio anzisha leo inataka kuendana. Huwenda camouflagers wapo kaziniHuu hapa
Camouflagers na informers
KISWAHILI ni wazugaji na wafichua habari Ni watu maalum lakini wa kila jinsia umri na kaliba... Kati yao wapo mpaka wezi matapeli, wakabaji na wachawi.. Lakini kila walipo wapo kwa lengo maalum.... Kutoa taarifa ambazo zitasaidia kubaini waovu na kuzuia hatari ama kulinda usalama wa nchi raia...www.jamiiforums.com
Hopeful mamlaka zenye dhamana zitachukua ushauri wako kama hawajaufanyia kazi bado au kuanza sasa kutoa majawabu ya uchunguz ambao wamekuwa wakifanya kuhusu masuala haya.Naandika tu kama mtazamo wangu.. Maana pengine hatua zinaweza zisichukuliwe haraka kutokana na aina ya wapelelezi tulio nao
Kuna conclusion zinatolewa haraka sana kwenye haya mauaji na vifo na watu wasio sahihi... Kwa wenzetu ripoti ya daktari ndio husema ukweli.. Lakini pia nyuma ya hivyo vifo na mauaji huwa kuna mengi yanayohitaji uchunguzi wa kina kabla ya kutoa majibu ya jumla
Wiki jana mwishoni kuna mzee alifariki nyumba ya wageni akiwa na mwanamke.. Police hata kabla ya kuchunguza ama kumshikilia mwanamke aliyekuwa na marehemu wakasema hakuna haja kwakuwa marehemu alikuwa na shida ya BP .. kwahiyo kajifia tu mwenyewe🥺
Tamko hilo la polisi likamweka huru aliyekuwa na marehemu.. Mwili ukazikwa maisha yanaendelea
Kisarawe Dada maarufu mitandaoni kwa kupiga danadana kakutwa kafa chumbani kwake na mwili ulishaanza kutoa harufu.. Walau hapa police wanasema wanachunguza. Sijui uhalisia wake
Jana tena huko Bonyokwa Manispaa ya Ubungo mume na mke wamekutwa chumbani kwao wamechinjwa hadi kufa huku kitandani pakikutwa na 'pesa nyingi'
Tayari baadhi wameshasema na mauaji ya visasi kutokana na dhuluma.. Ushahidi ukiwa ni zile pesa
Hiyo ni mifano michache tu ya hivi karibuni. Lakini ipo mingi sana na kesi zao ziliishia kusikojulikana
Kwa wafuatiliaji wa kesi za mauaji ni muhimu sana kufungua jalada la kesi husika kwakuwa, wauaji wengi huacha ushahidi ambao huja kujulikana baada ya vipindi virefu kupita
Mathalani kuna mauaji mengi yalitengenezewa hadithi tofauti ili kuficha ukweli
Mauaji ya wivu wa mapenzi unaweza kutengenezewa hadithi ya dhuluma. Watu wakaua na kuwekewa pesa ili kuficha ukweli
Mnakumbuka ile kesi ya yule mwanadada wa migodini kule Mwanza? Mauaji yake yalitengenezewa scene ya dhuluma kumbe ilikuwa wivu wa mapenzi
Shida nyingine hapo ni kwamba kuna majalada ya mauaji yalishafunguliwa lakini yakawa hayana mwendelezo.. Haya yametumika vibaya kuwabambikia watu kesi za mauaji😭Hopeful mamlaka zenye dhamana zitachukua ushauri wako kama hawajaufanyia kazi bado au kuanza sasa kutoa majawabu ya uchunguz ambao wamekuwa wakifanya kuhusu masuala haya.