Haya mayai ni na nini?

Haya mayai ni na nini?

vukani

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Posts
244
Reaction score
166
Mama mmoja alikuwa akifanya usafi nyumbani kwake, kwa bahati akakuta kibox kidogo chini ya mvungu wa kitanda, alipokifungua alikuta kuna mayai matano na shilngi milioni mbili.
Mumewe aliporudi alimuuliza kuhusu kile kisanduku na mayai ni ya nini?
Yule bwana akamjibu mkewe kwamba, alijiwekea utaratibu kuwa kila akitoka nje ya ndoa ananunua yai moja na kulihifadhi mle katika kisanduku.
Mkewe akiwa na furaha akamwambia duh! yaani tangu tuoane miaka mitano iliyopita umetoka nje ya ndoa mara tano tu! kumbe wale walikuwa wananiambia kuwa wewe ni malaya sana hawakuwa sahihi ki hivyo.
Mke akauliza, haya na hizi shilingi milioni mbili ni za nini?
Mume akamjibu kuwa, huwa anyauza yale mayai pindi yakiwa mengi na fedha huweka humo!
Duh! mke akataharuki, na kuanguka chini na kuzimia.........

Cheka kidogo..........................
 
Duuuh,

Inamaana huyo jamaa katoka nje ya ndoa before hayo mayai matano mara 8,000?

2,000,000 / 250 = 8,000

Lol itakuwa imeota sugu kabisa jamaa yake
 
Haya mayai ni na nini?????????????????????????????
 
Hahahahaha duh Balaaaa hapo mama kazimia kazi ya kumzindua inahitajika..ila kama mama alikuwa na clues kwamba mumewe anatoka nje kwann astuke hivyo?Na hayo mayai yalipokuwa mengi hakuyaona? ni mtazamo katika hii joke
 
Back
Top Bottom