1.Mahusiano yatakushinda kwa sababu hata kwenye makosa yako utamlaumu mwingine hivyo utaachwa kila mara na bado utajiona upo sahihi kuachwa π
2.Utaendelea kubaki na makosa yako na wengi watachukia kufanya kazi na wewe wataanza kukukwepa.
3.Utaona kila mtu hafai kwa sababu utataka upate mtu mkamilifu 100% kitu ambacho hakiwezekani
4.Kimafanikio utakwama kwa sababu mafanikio ni pamoja na kukubali makosa yako, kujifunza na kufanya upya.
UKIONA KILA MTU HAFAI JUA WEWE NDIO HUFAI KWA KUJIONA MKAMILIFU 100%
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako