Mkuu umejiuliza maswali ukajijibu. Bottom line ni kipato. Ukiwa na uwezo wa kuendesha Range Rover, maana yake wewe kwako Mafuta siyo shida. Nikinunua Mercedes na service nafanyia DT Dobie…nitasemaje kwamba Mercedes ni gari mbovu? Kama ulivyoandika hapa, determinant ni pesa. Basi.
Haya maswali yote unayoyaona humu…ni kutafuta unafuu wa uendeshaji au kumiliki haya magari.
Kwenye maisha kuna level inafika…service ya gari, bei ya mafuta…siyo issue tena.
Kama bado unaamini kuna gari hazina spare au zinasumbua…endelea kujitafuta. Hujajipata bado.
Wakati mwingine issue sio hela tu mkuu...... VIPAUMBELE na availability ya uendeshaji wa kila siku
Watu wanadhani as long as una hela ya kununua kitu basi unanunua tu bila kuangalia other factors....,, hii ndio kasumba yetu watu masikini
Mojawapo wa issue inayo wasumbua sana Mwendokasi ni spear na service, ni tofauti kabisa na mabasi yale yangekua scania au aina nyingine ambazo wauza spear na service wapo wengi
Jeshi la polisi wamenunua magari aina nyingi sana lakini hadi leo magari ya muda mrefu utakayo yakuta mitaani yanafanya kazi ni Toyota mkonga, Landrover 110 na Toyota Landcruser za bosi..... magari aina zingine yote kwisha habari yao sababu ya spear na service
CCM waliagiza magari sijui Mandraham hayakumaliza miaka miwili yote yako juu ya mawe
Sasa hivi wana Toyota zinadunda spear kama zote
Kuwa na hela haimaanishi ununie kitu chochote “kizuri” bila kuangalia factors zingine
Sasa ununue Benzi unaishi Kigoma halafu service unaenda kufanyia DT Dobie Dar kisa tu una hela
Uzuri wa kwenye social media kila mtu ni tajiri anashauri watu wajitafute kama unavyo tushauri kama tunashindwa kununua Vorgue kisa spear na service basi TUJITAFUTE