Haya ndio maisha halisi ya Darassa

Huyu jamaa angempata mtu kama sallam awe meneja wake angefika mbali mana akiendelea kufanya show za buku tano kumi hatafaidi matunda ya kazi zake
 
Kama ni kwake yuko vizuri angalau, maana maisha ya wasanii wa bongo nao.
 
Darasa hakikisha nyimbo yako ya Muziki inakuingiza nyumbani kwako!!yaani mpaka ufumue mjengo wa maana ndio uwaonee huruma wana hiphop wenzio,kaza mwanangu kitaeleweka tu..

Wakamue hao mapromota bei kubwa kwenye show,wapige hata million nane tisa!!usiwaonee huruma,kwa ulipofikia sasa hivi unajaza ukumbi wowote ule bongo hii..

Halafu Hanscana usimchekee sana japokuwa ni meneja wako,mtoto wa Arusha yule kwenye hela haaminiki...Hakikisha unakuwa na final say wewe kama wewe!!komaa na management mpaka kieleweke,usicheke nao kabisa..hii ndio time yako ya kuuaga umaskini bro..
 
Kama ni kwake yuko vizuri angalau, maana maisha ya wasanii wa bongo nao.
Hiyo ghorofa amepanga tu!!game lilikuwa halijamkubali bado darassa..yaani akomae na single hii ya MUZIKI mpaka ahamie kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…