Dr Count Capone
JF-Expert Member
- Feb 7, 2017
- 1,878
- 3,263
--IN FACT--
MAJENGO YASIYO NA MFANO ULIMWENGUNI
COLLESEUM
Majengo haya yalianza kujengwa enzi za dola ya ROMA (ROMAN EMPIRE),lengo kuu la kujengwa kwake ni kuwa sehemu ambayo watu wanakutana kwaajili ya kushuhudia tukio fulani likitokea kwa mfano burudani (ni kama viwanja vya mpira wa miguu vinavyotumika siku hizi.
''MUHIMU: KAMA BADO HUJA'LIKE' PAGE YETU YA FACEBOOK IFAHAMIKAYO KAMA 'CLYZ MOOD' LIKE HIVI SASA KUPATA FACTS NYINGI KAMA HII PIA UNAWEZA KUALIKA MARAFIKI WA'LIKE' PAGE YETU.
TAFADHALI USISITE KUTUACHIA MAONI YAKO HAPO CHINI ''
Katika karne ya ishirini wataalam wa ujenzi hawakuwa nyuma katika kuhakikisha wanatengeneza maeneo bora zaidi ambapo watu watakutana pamoja ili kupata burudani ikiwemo michezo kama mpira wa miguu.'dizaini' (DESIGN) ya ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu vya siku hizi umetokana na mtindo uliokuwa unaonekana wa majengo ya COLLESEUM kwa namna moja ama nyingine.Hivyo basi wataalamu wa ujenzi wa dola ya ROMA ya kale walichangia pakubwa katika maboresho ya ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu siku hizi.
CHUO KIKUU CHA OXFORRD (OXFORD UNIVERSITY)
Chuo hiki ni chuo kikongwe na maarufu sana kwa watu wanaozungumza lugha ya kiingereza na duniani kwa ujumla,tarehe sahihi ya kuanzishwa kwake haijulikani,lakini wasomi wanaamini kuwa kilianzishwa katika miaka ya 1100 A.D.
Chuo cha OXFORD kinajuisha jumla ya colleges 39 na kumbi za wazi saba (ambazo ni za taasisi za kidini).
Kila college inajiendesha yenyewe ndani ya chuo,kila college inadhibiti uanachama wake pamoja na shughuli zake za ndani.
Chuo cha OXFORD kinaendesha 'makumbusho ya chuo kikuu' yalio ya kale sana,pia ina mfumo mkubwa kabisa wa maktaba za kujisomea ndani ya UINGEREZA.Watu wengimashuhuri walipata elimu yao kupitia chuo kikuu hiki cha OXFORD wakiwamo mawaziri wakuu wa UINGEREZA ishirini na saba,washindi wa tuzo ya NOBEL ishirini na nane na viongozi wengine wakuu wa serikali nyingi duniani kote.
Chuo hiki hakina CAMPUS KUU ila college,idara na vituo vyake vingine vimetawanyika mji mzima na ndio maana chuo hiki wakati mwingine kinaitwa kwa lugha ya kizungu "CITY UNIVERSITY".
Majengo ya chuo hiki kama RADCLIFF na SHELDONIAN THEATRE hutumika kwa matamasha ya muziki,hotuba (lectures) na sherehe za chuoni hapo.Kabla ya kujengwa kwa SHELDONIAN THEATRE kanisa la chuo liitwalo UNIVERSITY CHURCH OF ST.MARY THE VIRGIN lilikuwa linatumika kwa sherehe za chuo lakini baada ya ujenzi wa SHELDONIAN THEATRE shughuli za sherehe zilihamia humo.
THE FORBIDDEN PALACE/CITY
THE FORBIDDEN PALACE ni mkusanyiko wa majengo ya kifalme yalioko CHINA ambayo yalikuwa yakikaliwa na wafalme wa nasaba za MING na QING.
Jina sahihi la majengo haya ni IMPERIAL PALACE (IKULU YA KIFALME),jina la FORBIDDEN PALACE limekuwa likifahamika zaidi kutokana na historia ya hapo nyuma ya majengo haya ambapo watu wa kawaida enzi za utawala wa MING na QING DYNANSTY hawakuruhusiwa kabisa 'kutia maguu' katika ardhi za majengo haya.
Haya ndio yalikuwa makazi ya wafalme ishirini na nane (28) wa wakati wa tawala za MING na QING DYNASTIES.
Majengo haya yalianza kujengwa mwaka 1406 na kumalizika mwaka 1420.Muundo wa majengo haya unajumisha jumla ya majengo 980 ambayo yamechukua nafasi ya ardhi ya zaidi ya ekari 180.Majengo haya ya kifalme yamekuwa chachu katika maendeleo ya tamaduni na maswala ya ubunifu katika ujenzi ndani ya ASIA MASHARIKI,pia lilitangazwa na kuongezwa kwenye orodha ya maeneo yenye urithi wa kale na UNESCO mwaka 1987.
THE PENTAGON
Kitu gani cha kwanza huja kichwani baada ya kusikia PENTAGON? au huwa unakumbuka tukio la september eleven?
PENTAGON ndio jengo pekee ulimwenguni lenye kujumisha ofisi nyingi.PENTAGON ni makao makuu ya idara ya ulinzi ya MAREKANI,ipo ARLINGTON COUNTY,VIRGINIA,MAREKANI.Pentagon ilidizainiwa na mbunifu GEORGE BERGSTROM na likajengwa na JOHN McSHAIN.Jengo hili limechukua nafasi ya ardhi ya zaidi ya square metre 600,000 na inakadiriwa kuwa na wafanya kazi zaidi ya 26000 (jumla ya wafanya kazi wa maswala ya ulinzi na wale wasiohusika na mambo ya kijeshi).
Jengo la PENTAGON lina ghorofa tano (5) kuelekea juu na basements (sehemu ya nyumba iliopo chini ya ardhi) zenye level mbili.
Moja ya tukio la kukumbukwa kuhusu PENTAGON ni lile la septemba 11,2001.Hii ilikuwa ni miaka sitini (60) baada ya kuanza ujenzi wa jengo hili,ndege ya AMERICAN AIRLINE FLIGHT 77 iliotekwa ilipaa na kugonga upande wa magharibi wa jengo hilo na kuua watu 189.Hili lilikua ni shambulio la kwanza dhidi ya mali ya serikali ya MAREKANI ukiacha lile shambulio la kuunguzwa kwa mji na WAINGEREZA wakati wa vita vya mwaka 1812 kati ya UINGEREZA na MAREKANI.
TAJ MAHAL
Ni zawadi gani ushawahi kufikiria kumpatia mpenzi wako? cheni ya dhahabu?,simu kali kama IPHONE X? gari aina ya FERRARI,PORSCHE,LAMBORGHINI? au mjengo mkali ZANZIBAR?
Jengo hili la TAJ MAHAL lilijengwa karne ya 16 na mfalme SHAH JAHAN ikiwa ni kama zawadi kwa mkewe kipenzi.
Linatambulika kama moja ya majengo mazuri ulimwenguni.TAJ MAHAL imejengwa kwa malighafi bora kutoka bara ASIA na INDIA- ina inasemekana kuwa tembo wapatao 1000 walitumika katika ujenzi wa TAJ MAHAL (tembo hawa walitumika kwenye kubeba mawe,vito na malighafi nyingine za ujenzi).
TAJ MAHAL inajumuisha msikiti,bustani na nyumba ya wageni.Wakufunzi wamekuwa wakibishana juu ya jambo gani linalilifanya jengo la TAJ MAHAL kuwa zuri na la kipekee?
Wapo wanaosema kuwa uzuri na upekee wa jengo hilo unatokana na mfumo na mpangilio wa majengo yake,wengine wanasema ni kutokana na namna 'VITO' vilivyopambwa katika jengo hilo vinavyoendana na mwanga wa jua hivyo kupelekea kubadilika kwa rangi ya jengo mara jua linapochomoza na wakati wa kuzama kwake.
Pia kuna wengine wanasema kuwa uzuri na upekee wa jengo hilo unatokana na lengo lililopelekea kujengwa kwa jengo hilo;
LENGO LA UJENZI KWA KIFUPI
Jengo hili lilijengwa kutokana na amri ya mfalme SHAH JAHAN ambae aliamuru mafundi bora wa ujenzi wajenge jengo hilo kwa ustadi wa hali ya juu na baada ya kumalizika kwake alikabidhi kama zawadi kwa mke wake kipenzi.
Ona ni mapenzi gani alionayo mfalme kwa mkewe.
Tunaomba uwe 'judge' katika kuamua ni kitu gani kinalipa upekee jengo hili,hata kwa kutazama picha zake hap chini.
KREMLIN
Huenda ushawahi kusikia kabla jina hili likitajwa,ndio,mara nyingi linahusishwa na serikali ya URUSI.
KREMLIN ni neno la lugha ya kirusi lenye kuwakilisha jengo au 'ngome iliopo katikati ya mji'.
KREMLIN ni mkusanyiko wa majengo yenye kuwa na ofisi nyingi za serikali ya URUSI mjini MOSCOW nchini URUSI.Jengo hili lipo juu kidogo ya mwinuko likitazama MTO MOSKVA kwa njia moja ama nyingine,jengo hili lipo kama ngome limekuwa hapo kwa takriban miaka 1000,eneo hilo lilipewa jina KREMLIN katika karne ya 14.
KREMLIN ipo ndani ya kuta zilizojengwa kwa mtindo wa pembe tatu zilizozojengwa kuzunguka majengo ya KREMLIN,majengo hayo yamechukua nafasi ya ukubwa wa ekari 68.
Kuta ni za tofari za rangi nyekundu,minara yake juu imechongoka mfanowa penseli,majengo yake yamepakwa rangi nyeupe na njano huku paa zake zikiwa zimepakwa rangi ya kijani ambazo rangi zote zinapendeza kimuonekano.Ndani ya mkusanyiko wa majengo ya KREMLIN kuna jengo kongwe zaidi ya yote, hili ni kanisa kubwa la DORMITION lililojengwa katika miaka ya 1470.
KREMLIN imeshuhudia matukio kadhaa na muhimu ndani ya kuta zake, mfano:
IVAN alijenga ikulu ndani ya KREMLIN.
Wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia (warusi wao wanaita 'great patriotic war',vita kuu ya kizalendo) kiongozi wa USOVIETI wa wakati huo JOSEPH STALLIN 'aliwakimbiza' wavamizi wa kijerumani mpaka kutoka katika milango ya kuingilia MOSCOW (tukio hili linawezekana kluwa ni tukio kubwa sana kufanywa na kiongozi yeyote wa USOVIETI na URUSI).
Leo hii KREMLIN inajumuisha ofisi za mamlaka ya juu ya serikali ya shirikisho la urusi.KREMLIN itabaki kuwa ni jengo la kukumbukwa zaidi katika historia ya taifa kuu la URUSI hata kama itakuja kubadilishwa matumizi hapo baadae.
#PROUDLY_SPONSORED_BY
JSRindustries
CLYZ MOOD FB PAGE
KENDRICK STUDIO
#IMEPEWA_NGUVU_NA
HAMIS KIMWAGA (BINGWA)
ABA YASSER
JUMA KILUMBI