Pre GE2025 Haya ndio majina matatu ya wanachama wa CCM wanaoweza kupambana na Lissu jino kwa jino bandika bandua akimwaga mboga anamwaga ugali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyo Kalamaganda ana hasira muwako sana.

Hawezi kuvumilia maudhi ya Tundu.

Alikuwa mwalimu wangu wa Law.

Slow slow na tumbili sawa
 
Kinana, JK,makamba Sr, wasira, mhagama madam, Mama Abdul, makamba Jn, Rizi one, mwigulu, mola asipofanya Yale ya 17.3.2021.
Wengi tutakufa tukiwa mafukara na umaskini wa kutisha
 
Hakuna mwana CCM anayeweza kuleta majibu yanayoelewa na kukubaliwa na wengi kuwa ni majibu kwenye issue ya Muungano.

Nielewe nikisema hakuna. Issue ya Muungano hata tumkodi Malaika kutujibia hawezi akaeleweka.

Wewe tu ukiulizwa kwa nini Mzanzibar anakuwa Mkuu wa Wilaya Tanganyika na mtanganyika hawezi kuwa mkuu wa Wilaya Zanzibar unaweza kujibu?

Hapo halijawekwa suala la umiliki wa ardhi!
Kutoa majibu ya Muungano sahihi ni ngumu wanachoweza tu ni kutumia mabunduki na Majela
 
Lissu ni kijana wa mjini na amefanya siasa nyingi za hoja na za hovyo akiwa Bungeni na sasa majukwaani.

Kwa mtazamo wangu haya ndio majina ya wanachama 3 wa CCM wanaoweza kupambana na Lissu jino kwa jino bandika bandua.

Anahitaji kujibiwa vile anavyokuja akija kihuni anajibiwa kihuni akija kisomi anajibiwa kisomi.

1. Prof Palamagamba Kabudi

2. Hamprey Polepole

3. David Kafulilal
 
Kuna haja kwa kipindi hiki kuangalia katiba zetu upya

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hairuhusu Rais aliyopo madarakani au kustaafu kushtakiwa kwa kosa lolote lile

Je siku akitokea Mzanzibar akawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa makusudi ya kulindwa kisheria na kikatiba akawa anatapanya rasilimali za Tanganyika kwa maslahi yake au kwa maslahi ya kikundi fulani kilichopo Zanzibar jiulize nani wa kutetea au kuzilinda mali za Tanganyika?

Zanzibar wana serikali yao inayolinda mali na rasilimali za Zanzibar je Mali za Tanganyika zinalindwa na nani?
 
Hoja za Mh.Lissu zinaweza kujibiwa na yeyote wala hazina uzito wowote.
Kwa mfano.
1.Muungano hoja kiu ni uwepo wa Tanganyika....kwa ufupi kabisa Tanganyika ndio Tamisemi na Mkuu wake ni Mh.Waziri Mkuu.
2.Katiba Mpya...Wananchi wengi hawaifahamu vema katiba iliyopo ili Mpya ije ni lazima wananchi wapate Elimu ya katiba na waachiwe kufanya uamuzi kupitia kula ya maoni.
3.Tume huru ya Uchaguzi.
Uhuru wa tume upo sema tu wenye kusimamia chaguzi ndipo changamoto uanza na kupekelekea chaguzi kugubikwa na sintofahamu nyingi.
4.Je ni sahihi Kiongozi mkazi wa eneo lingine ndani ya JMT kufanya maamuzi/maendeleo sehemu nyingine....Jibu ni ndio,sababu wapo Viongozi wengi walioteuliwa kwa nafasi mbalimbali tunawaona kila siku wakizunguka Nchi nzima kutekeleza na kutatua kero za Wananchi.
Ndio maana hata yeye Mr.Lissu anazunguka maeneo ambayo sio ya kwao kuhimiza mabadiliko.
 
Wadanganyika tushauzwa na ccm. Zanzibar ina wimbo wa taifa, ina bendera, ina bunge, mwingi anapata miariko nje kama rais wa Zanzibar. Muungano umebaki wizara tatu kwa maslahi ya Zanzibar. Wizara ya fedha, ulinzi, na mambo ya nje, ila serikali tatu ni robo lengine la ulaji kwa wanasiasa kama kweli kuna nia njema ya kuendeleza udugu wetu basi serikali moja ndilo jibu. Lakini uroho wa ving'ora wanasiasa hawata kubali ili kulinda maslahi yao.
 
Kuna haja kwa kipindi hiki kuangalia katiba zetu upya

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hairuhusu Rais aliyopo madarakani au kustaafu kushtakiwa kwa kosa lolote lile

Je siku akitokea Mzanzibar akawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa makusudi ya kulindwa kisheria na kikatiba akawa anatapanya rasilimali za Tanganyika kwa maslahi yake au kwa maslahi ya kikundi fulani kilichopo Zanzibar jiulize nani wa kutetea au kuzilinda mali za Tanganyika?

Zanzibar wana serikali yao inayolinda mali na rasilimali za Zanzibar je Mali za Tanganyika zinalindwa na nani?
Mali za Tanganyika hazipo kwa sababu Tanganyika haipo.
Vyama vya siasa ili viwe na nguvu ni lazima virudishe kwanza Mali za Wananchi zilizopatikana enzi ya mfumo wa Chama kimoja.
 
Naunga mkono kwa prof. Kabudi. Kafulila anao uwezo lkn maCCM wanamuona siyo mwenzao ni (ng'ombe aliyekatika mkia). Kwahiyo atashindwa kuwa huru.
 
Hoja za Mh.Lissu zinaweza kujibiwa na yeyote wala hazina uzito wowote.
Kwa mfano.
1.Muungano hoja kiu ni uwepo wa Tanganyika....kwa ufupi kabisa Tanganyika ndio Tamisemi na Mkuu wake ni Mh.Waziri Mkuu.
2.Katiba Mpya...Wananchi wengi hawaifahamu vema katiba iliyopo ili Mpya ije ni lazima wananchi wapate Elimu ya katiba na waachiwe kufanya uamuzi kupitia kula ya maoni.
3.Tume huru ya Uchaguzi.
Uhuru wa tume upo sema tu wenye kusimamia chaguzi ndipo changamoto uanza na kupekelekea chaguzi kugubikwa na sintofahamu nyingi.
4.Je ni sahihi Kiongozi mkazi wa eneo lingine ndani ya JMT kufanya maamuzi/maendeleo sehemu nyingine....Jibu ni ndio,sababu wapo Viongozi wengi walioteuliwa kwa nafasi mbalimbali tunawaona kila siku wakizunguka Nchi nzima kutekeleza na kutatua kero za Wananchi.
Ndio maana hata yeye Mr.Lissu anazunguka maeneo ambayo sio ya kwao kuhimiza mabadiliko.
Umeidharau Sana Tanganyika, nchi ukaipe hadhi ya wizara. Nimelia Sana.
 
Majobu rahisi hasara za wajukuu wako
 
Naunga mkono kwa prof. Kabudi. Kafulila anao uwezo lkn maCCM wanamuona siyo mwenzao ni (ng'ombe aliyekatika mkia). Kwahiyo atashindwa kuwa huru.

..Kabudi alikuwa kwenye tume ya Warioba na aliunga mkono serikali 3.

..akimkabili Lissu atakumbushwa alichokuwa akikisema 2014 alipokuwa kwenye tume ya Warioba.
 
Swala la muungano ni gumu kwa pande zote mbili. Ndiyo sababu kukawa na wizara inayoshughulikia . Kama kitu kiko sawa hakuna sababu ya kuwa na wizara ya namna hiyo. Wenyewe wanaita kero za muungano. Kwa nini tuwe na muugano wenye kero? Hapo ndipo anapowashindia na majibu hakunaaa
 
..Kabudi alikuwa kwenye tume ya Warioba na aliunga mkono serikali 3.

..akimkabili Lissu atakumbushwa alichokuwa akikisema 2014 alipokuwa kwenye tume ya Warioba.
Tatizo ccm wengi huwa wanatengua misimamo yao ya awali iliyowapa umaarufu.
 
Back
Top Bottom