Haya ndio makundi hatari yasipodhibitiwa yataitikisa sana Tanzania

LorenzoA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
5,889
Reaction score
17,753
Makundi hatari kwa maana ya nguvu ya kisiasa na uwezekano mkubwa wa kugeuza nchi kuonekana ni ya hovyo kabisa ni haya

1. Wamachinga wasio sehem rasmi
Sasa hivi ukienda Mwanza kwenye Kipleft cha bara bara ya Nyerere wachuuzi wanaanika vitunguu pale, yani kati kati ya ile round about,
Kariakoo ni mtindo mmoja, hadi wachoma mahindi wapo Kariakoo, Congo na gerezani haipitiki, na hakuna wakuuliza wala kuhoji, inapelekea wenye biashara kubwa wabanane hivyo hivyo kwa kupoteza biashara maana wenye magari hakuna anaeweza kupita Congo na Aggrey.

Stand mpya ya kuchomekewa ya Mbezi ndio balaa, wachuuzi na miavuli kama laki hivi yani na hakuna wakusema kitu.

2. Bajaji
Team kubwa kabisa katikati ya miji ya Moshi, Dar, na Singida, yani hata usiseme, sijui lengo la kuondoa vipanya Dar lilifanikiwa tukaamua tuje na Bajaj au ilikuwaje.. hovyo kabisa yani.
Kwani wakikaa nje ya mji biashara hakuna?

3. Bodaboda
Hapa hata nisiseme sana, utachoka ukangalia walivyotapakaa kila mahali, hakuna control hakuna nini, tena naambiwa wana kundi lao la kitaifa, dah

Hivi kweli kuyawekea haya makundi utaratibu ni kosa au ni dhambi? au ni zile siasa za Mnyonge na wazalendo zinaendelea?

Miji mikubwa bila nidham na utaratibu inageuka kuwa uwanja wa wanyanganyi.... huko tunakoelekea haya makundi hakuna wa kuwadhibiti, na inavyoonekana wanasiasa wetu wanawaogopa, ni suala la muda tu.

Mamlaka za majiji hivi kweli hata hili lazima rais ahutubie taifa?
 
Mimi hawa wamachinga feki waliojenga kwenye njia za waenda kwa miguu na baiskeli..barabara za Dar, Dodoma na Mwanza...
Watolewe, haya majiji yameharibika jamani!
Kwanza siyo salama kwao, iko siku lori litafeli breki na kukata mabolt na kuwaparamia.

Tunasubiria watu wafe au nini jamani ndiyo tuchukue hatua??

Inasikitisha na kufadhaisha sana.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Tundu Lissu, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
 
Huku Dodoma hata ikitaka kupack gari ,hamna sehemu wamejaa mpaka karibia na barabara
 
Sasa inabidi tuseme Gulio LA Dar es Salaam, au Mwanza, Dodoma au Arusha, je ustaarabu wetu umepotelea wapi!? Ni sawa unakwenda kwa mtu unakuta vitu vyote hadi vitanda na matandikio yapo sebuleni, ila kwa sisi kwenye biashara zenye leseni ndio full mkorogano!!
Ushauri, maofisa biashara waandae maeneo rasmi ili kila mlipa kodi awe na sehemu ya kunadi biashara yake aweze kulipa kodi stahiki
Tanroads barabara zimezibwa na vibanda na mvua ikinyesha inaziba culvarts na kusababisha Kingo kubomoka!! Nani mwenye uchungu!?
 
Hayo yote yanaweza kuliwa kichwa bila hata hata kujieleza kwa sababu Alipokuwa anaunua ndege kwa cash bila idhini ya bunge hakujieleza , alipojenga Bwawa la Umeme bila feasibility study na Tathmini ya mazinga hakujieleza, alipojenga uwanja wa ndege Chato hakujieleza. Zaidi sana alisema yeye ukimshauri ndio unaharibu kabisa.
Tundu Lissu, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
 
Kundi namba 1 lilipaswa kuwa wanasiasa kama Munde na wafia chama ambao hawataki kabisa kusika neno KATIBA MPYA.
Makundi hatari kwa maana ya nguvu ya kisiasa na uwezekano mkubwa wa kugeuza nchi kuonekana ni ya hovyo kabisa ni haya

1. Wamachinga wasio sehem rasmi
Sasa hivi ukienda Mwanza kwenye Kipleft cha bara bara ya Nyerere wachuuzi wanaanika vitunguu pale, yani kati kati ya ile round about,
Kariakoo ni mtindo mmoja, hadi wachoma mahindi wapo Kariakoo, Congo na gerezani haipitiki, na hakuna wakuuliza wala kuhoji, inapelekea wenye biashara kubwa wabanane hivyo hivyo kwa kupoteza biashara maana wenye magari hakuna anaeweza kupita Congo na Aggrey.

Stand mpya ya kuchomekewa ya Mbezi ndio balaa, wachuuzi na miavuli kama laki hivi yani na hakuna wakusema kitu.

2. Bajaji
Team kubwa kabisa katikati ya miji ya Moshi, Dar, na Singida, yani hata usiseme, sijui lengo la kuondoa vipanya Dar lilifanikiwa tukaamua tuje na Bajaj au ilikuwaje.. hovyo kabisa yani.
Kwani wakikaa nje ya mji biashara hakuna?

3. Bodaboda
Hapa hata nisiseme sana, utachoka ukangalia walivyotapakaa kila mahali, hakuna control hakuna nini, tena naambiwa wana kundi lao la kitaifa, dah

Hivi kweli kuyawekea haya makundi utaratibu ni kosa au ni dhambi? au ni zile siasa za Mnyonge na wazalendo zinaendelea?

Miji mikubwa bila nidham na utaratibu inageuka kuwa uwanja wa wanyanganyi.... huko tunakoelekea haya makundi hakuna wa kuwadhibiti, na inavyoonekana wanasiasa wetu wanawaogopa, ni suala la muda tu.

Mamlaka za majiji hivi kweli hata hili lazima rais ahutubie taifa?
 
Mimi hawa wamachinga feki waliojenga kwenye njia za waenda kwa miguu na baiskeli..barabara za Dar, Dodoma na Mwanza...
Watolewe, haya majiji yameharibika jamani!
Kwanza siyo salama kwao, iko siku lori litafeli breki na kukata mabolt na kuwaparamia.

Tunasubiria watu wafe au nini jamani ndiyo tuchukue hatua??

Inasikitisha na kufadhaisha sana.

Everyday is Saturday............................... 😎
Kaka Kwa MWANZA Nyerere road huwez pitisha lory kwenye hiyo RA ninyoisema hapo
 
Hao wote cha mtoto

Kundi hatari la madalali wa wa wawekezaji matapeli ndo hatari zaidi.

Professor Muhongo
Ngeleja.

Bashe..
 
Dhahama tu.... hakuna kinacho patikana au kuendeleza, uharibifu wa miundombinu, takataka zao na maji ya kuoshea viombo,masufuria humwagwa barabarani mchana mweupe.

Angalia pawepo na nidhamu za size za miamvuli na mabanda na usafi...
 
1. Wamachinga wasio sehem rasmi
Sasa hivi ukienda Mwanza kwenye Kipleft cha bara bara ya Nyerere wachuuzi wanaanika vitunguu pale, yani kati kati ya ile round about,
Kariakoo ni mtindo mmoja, hadi wachoma mahindi wapo Kariakoo, Congo na gerezani haipitiki, na hakuna wakuuliza wala kuhoji, inapelekea wenye biashara kubwa wabanane hivyo hivyo kwa kupoteza biashara maana wenye magari hakuna anaeweza kupita Congo na Aggrey.
Wa kulaumiwa ni serikali haijawawekea mazingira supportive ya kufanya biashara hizo, watu wa aina hiyo wapo duniani kote tofauti na sisi ni kwamba wametelekezwa, hawajawekewa miundombinu wezeshi ya kufanya hizo biashara bila kuathiri sector zingine
 
Niliona Mwanza katikati ya Jiji Nyerere road nyanya chungu na bamia zinapatikana kwa wingi
 
Back
Top Bottom