Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!

Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!

Mimi na nina hakika tupo wengi tu hatuutakki muungano lakini si kwa nia ya kutaka vyeo au madaraka kwa hiyo maneno yake hayo hayatuhusu. Anayewalenga yeye ni wale wanaotaka kuuvunja muungano kwa ajili ya vyeo na madaraka.

Halafu binadamu gani huyo "anayewaapiza" wenzake kwa ajili tu wametofautiana kimtazamo?

Ni kweli Kuwa wengi wenu ni wajinga sana kiasi cha kupelekeshwa na Pepo za kisiasa tuuuu. Ni wajinga sana kiasi cha kushindwa kabisa kuielewa hotuba ya nyerere. Poleni sana maana WAJINGA NDIO WALIWAO....... NA Mmeshaliwa haswa huko nyuma
 
Kwa nini iwe Tanganyika tu!? Je Kuhusu wanaoiomba Z'bar yenye mamlaka kamili hakutoa tamko?

tena sijui hapo wana siri gani, zanzibar ni nchi iliyokamilika ina katiba, bendera, vitambulisho vyao vya uraia nk.. lakin bado ccm inaendelea kuing'ang'ania znz, jaman nini hiki? are we out of our mind to see what is going on! dah! inauma sana hasa pale unapoenda znz na kufanywa kama mgeni huwezi hata kumiliki ardhi. jaman tuachane nayo tujenge tanganyika yetu, hao wakinanyerere na karume walifanya maamuzi kama vile nchi ni ya kwao kisa walikuwa wamesoma peke yao, wametupeleka pabaya sana. mndriiiiiii hiiiiiii nhiiiii(crying)
 
Kitu ambacho mwalimu hakujua ni kuwa kutakuwa na watu wataulinda muungano kutokana na uroho wa madaraka. Unfortunately he is not here to see it, anakumbuka zaidi ulevi wa urais wa Salmon Amour, uroho wa urais wa Seif, na uchu wa madaraka wa baadhi ya viongi wa bara.
 
Tunapenda kumwinua Nyerere katika masuala tunayoshindwa kuyatetea wenyewe.Tuutete muungano kwa hoja za wakati wetu si kumnukuu Nyerere tunaposhindwa hoja.Tumevunja azimo la Arusha ambalo Nyerere ndio muasisi wake mbona mnashindwa kuenzi Nyerere kwa kulirejesha azimio la Arusha ?.
 
Nahitaji kujifunza Kiswahili vizuri hapa; Maneno haya yalitamkwa na mwalimu kama sio mwaka 1994 basi ilikua February 1995 Kilimanjaro hotel, Nyerere kafariki October 1999; with that interval tunaweza kusema eti hayo ni maneno ya mwisho mwisho ya mwalimu!!!!!?
 
Back
Top Bottom