Haya ndio Mapinduzi ya Zanzibar, yamerikodiwa live na waitaliano 1964

RED Xs

Kwa hisani yako fungu akitabu kiitwacho ZANZIBAR TRADITION AND REVOLUTION kilondikwa na ESMOND GRADLEY MARTIN, published by HAMISH HAMILTON (LONDON) ISBN 0-241-89937-0 MWAKA 1978

soma p25

ripoti ya Marco Polo kuhusu zanzibar ilisema hivi.....zanizbar wakaazi wake ni weusi awana nywele za singa...

sasa pingana na hao wazungu

walipofanya mkutano wa ujerumani wa kuigawa afrika, wakazichukuwa sehemu zote za zanzibar isipokuwa wakaawachia visiwa vya unguja na pemba, mombasa na mafya na fukwe yote ya east afrika kama inavoonekana katika ramani hii ya 1886

View attachment 100137

kama unaweza kupingana na wazungu sawa

ukitaka kujuwa zaidi uliza tu
..ama labda sijaelewa..kwambamarco polo anasema "zanzibar wakaazi wake ni ni " weusi 'awana'(?) nywele za singa.." kama ni kweli hiyo inajitosheleza na ukweli wa uafrika wa zanzibar...lkn kuna jambo lingine moja..! muarabu, anakuwa muarabu kwanza.. sababu ya lugha..! ndo maana msiria au mlebanon, au au mjordan, au mpalestina mwenye haiba (hata wakati mwingine na macho ya buluu) ni mwarabu, na muirani ni muajemi..! naweza kukuuliza lugha ya wenyeji wa asili wa zanzibar ilikuwa ni kiarabu? kwa nini kiarabu si lugha kuu ya watu wa zanzibar kama ilivyo sudan, oman na nchi zingine ambazo kwa asili ni za kiarabu? kwa nini kiswahili zanzibar kama ilivyo (kwa kiasi kikubwa)karibu pwani yote ya afrika magharibi?..nashukuru kunitambulisha kitabu hicho, insha allah nitakitafuta nikisome kisha nilinganishe na vitabu vingine vya historia nilivyosoma...!
 
.....ashakhum.....wangazija pori maanaake nini kakaangu? mbona unakuwa na kauli kama za watu wa tabia ya "kijinsia ya elton john"...? ulianzia mwanzo wakati nilipozungumzia ubaya wa matumizi ya silaha bila kujali nani anaitumia? bila kujali kama ni jambazi, polisi, wapigania uhuru, wa polisario, ANC,SWAPO, FRELIMO, UMMA PARTY (YA ZANZIBAR0) PLO?...wenye kuelewa tunalaani matumizi ya aina yoyote ya silaha sbb ya matokeo yake..!matumizi ya silaha hayana heri popote yalipotokea, iwe unguja, iwe rwanda, iwe palestina, iwe kosovo, iwe libya..!wanawake , watoto na vikongwe ndio muhanga wakuu wa matumizi ya silaha..! kilichotokea zanzibar kimetokea kila sehemu duniani ambapo watu waliamua kushika na kutumia silaha..! hatufurahii, lkn hatukubali kuwa chini ya ukoloni..! kama una uelewo wa qur'an tukufu soma ktk 8:25 ya qur'an, tafuta na tafsir ya ayah hiyo kisha tafakari kilichotokea unguja mwaka huo wa 1964...kisha tafakari..! mungu awarehemu wale wote waliodhulumiwa nafsi zao kila mahali hapa duniani, hususan ktk afrika na palestina..

Mi nadhani at this point we can zoom down;

1. Bin Faza; Okello hayupo na harudi, Karume hayupo na harudi pia Nyerere. Tulishaulizana sana maswali kama haya katika mnakasha fulani. Hapa tutenge wahanga na kisa hiki na sababu za kisa.

YAANI; uhalali au uharamu wa WW2 sio idadi ya marehemu, bali ni sababu za kumpiga Hitler, wewe Bin Faza, kama utawala wa awali wa kisultani unaukumbuka unadhani mchango wake katika yaliyotokea januari 12, 1964 ni yepi?

2. Robo tatu ya wazenj wa sasa hawakuwapo wakati wa tukio lile, RED Xs, ni kweli kusema Wazenj wanataka warudishwe kwenye utawala wa familia ya Kisultani? Is this real? kwa kigezo kipi?

3. Katika hali ya kutoaminiana kama ilivyo sasa, kuna dhamana gani kuwa kundi moja halitajiona linadhulumiwa na kurudia tena ya 1964?

Bin Faza, RED Xs
 
hizo ni fikra za mitaani tu, ukweli huwa vyengine

and opposite is always true

wewe kaka ukija znz tutakupokea kwa mikono miwili
nimeshakuja znz kwa kweli watu wa kule ni wakarimu wanaoleta fujo ni wanasiasa wachache ambao wanatumiwa na mataifa ya nje na muungano utakapovunjika watakaoathirika ni wananchi wa kawaida
 
Wazee wa bibi wa bibi yangu ni wazigua na wagunya,hawa ndio waliomwita mwarabu kuja kuwasaida kuwaondoa wareno zanzibar,wewe Je,twambie wewe unatoka wapi? 🙂

Nashukuru kwa maelekezo yako ndugu yangu. Nafikiri inatosha kukwambia nami pia asili yangu ni kama vile melting pot....ina mikanganyiko na tafran nyingi mno...lakini siku zote najinasibisha yakuwa kabila yangu ni Mswahili.

Nafikiri inatosha tukiachilia kwa hapa. Tuko pamoja Insha Allah.

Ahsanta.
 
Bin Faza,

Kama nakuona mitaa ya forodhani jioni utapata ngisi wako na tasi, teh teh teh.

Nakusoma na miwani ya 3D.

Shariff Ritz,

Bin Faza, mbona tayari alishatufahamisha yakuwa hiyo Forodhani siku hizi hapana hata pa kutia mguu...ati imejaa Wamasai kuliko hata hiyo Serengeti!?

Dah!...lazim nikubali yakuwa Bin Faza ana vipande murua kila nimsomapo!ahaha!!

Ahsanta.

Cc;Boko Haram
 
rodrick alexander

nimeshakuja znz kwa kweli watu wa kule ni wakarimu wanaoleta fujo ni wanasiasa wachache ambao wanatumiwa na mataifa ya nje na muungano utakapovunjika watakaoathirika ni wananchi wa kawaida

Nimefurahi angalau wewe umefika zanzibar kwahivo unazungumzia zanzibar inayoijuwa kidogo, sio kama wengine humu wanapiga makelele matupu kumbe hata znz ilivokaa hawajui

sasa kuhusu wazo lako kwamba kuna wanasiasa wachache ambao wanatumiliwa na mataifa ya nje.........hili sikubaliani nalo na nahisi ni kama political statement tu

ukweli ni huu

1. wanasiasa wengi sasa huku znz hata walioko ccm wamechokeshwa na mtirirko wa mambo baina ya znz na tanganyika

2. hakuna taifa la nje linalowashawishi wanasiasa bali ni wasomi wetu sasa wamekuwa wakitathmini masuala ya muungano kuanzia 1964. na matukeo yaliojiri baada ya uchaguzi wa 1995, 2000, 2005, 2010

3. tathmini nyengine iliyofanywa ni ya matamshi yanayofanywa na viongozi wa tanganyika kupitia muungano,

tathmini mbili hizi zimeonesha wzi kwamba tanganyika haina nia njema na zanzibar, na hili hatuwezi kulistahamilia tena.

mfano mdogo katika uchaguzi wa 20000 majeshi ya msumbiji yalipelekwe pemba, tunaushaihdi kamili na hili, sasa kwanini wapelekwe majeshi ya msumbiji lakii kwanini wapeleke majeshi from the first place?

katika uchaguzi wa 2010, Dr sheni alikuwa tayari amekubali matekeo ya kushindwa, lakini mkapa na mzee mwinyi wakaja znz haraka wakalazimisha ccm ishinde, why? hili lilitokea pale pale hoteli ya bwawani, kwanini lazima iwe ni ccm tu, lazima kuna ajenda za siri dhidi ya znz

sasahivi hakuna kijana yoyote anayetamani kulisikia neno muungano hapa znz, isipokuwa tangayika bado inalazimisha, lazima kaka kutakuwa kuna ajenda za siri, au wewe unasemaje????
 
Gombesugu; I dare say huyu REDx kajiandaa sana na hoja za kimantiki in a very EDUCATED approach manner. wewe ni scholar please mjibu kama alivyojieleza, that will be fair. Is it true Sultan wa Oman kwenye Berlin Conference alikuwapo? na because of that akapewa hilo pande la ardhi toka Mogadishu hadi Beira? Bin Faza, hebu hata wewe toa Msaada, ni kweli?

We know for sure MKWAWA, SINA, KIMWERI hawakuwapo, there should be a reason?

Gombesugu achana na Ungazija wake huyu bwana. Ukipoteza muda kwenye ungazija wake hutakumbuka point za kumjibu

cc RED Xs, Bin Faza,

Wickama,

Nafikiri kuna wakti mwingine nakushauri gumzo/hoja nyingine uziache tu zipite,au uliza suali kiustaarabu na nina hakika wapo wanajamvi wastaarabu wengi tu watakujuza kwa utuvu na kitaaluma.

Wewe local politics,History,dasturi na tamaduni za kiZanzibary au Ki-Unguja nina hakika huzijui asilan,na pia si wewe peke yako!?

Ndo maana mimi siku zoote husema yakuwa; masuala ya Zanzibar na WaZanzibary,nyinyi WaTanganyika daima yatakupeni taabu ziso mipaka!

Huyo jamaa unayehitaji nimjibu khadith/hoja zake...nafikri umefuatilia kisa cha mimi kuanza kumuuliza lile suali moja tu...specific/legitimate question na pia kumnasihi!?...matokeo yake nimepata triangular explanations/excuses!?

Ni pale tu alipoyataja yale maafa ya Zanzibar 1964,na kuyaita ati ni "mapinduzi matukufu".

Hakuishia pale,pia kutilia nguvu hoja yake ikamlazim kutaja nasaba yake ati yakuwa yeye ni "Mngazija" na pia ni "Muislamu",tena na huku akinukuu vipande kadhaa vya Qur'aan na kutoa mifano ya Maswahaba!?ahahaa!

Yaani kwa kifupi,katumia tricks/methods kama zile ulizokua ukitumia wewe kwenye ule mnakasha ulokwisha!

Kipata fursa,nakusihi pitia post/s yangu niloanzia kuzungumza nae plse!?

Ndipo mimi ikanilazim kiduchu kumnyooshea maneno na kumuuliza,je yeye ni kati ya wale Wangazija pori!?

Nakufahamisha yakuwa;hakuna Mngazija au kizazi cha Mngazija yeyote duniani kitakachokaa leo hii ati kufurahia yale maafa ya 1964 au kuyaita "matukufu"...asilan,abadan!

Mpaka kesho Wazee wetu,wakitukhadith yalotokea hiyo 1964 mioyo huwenda mbio na miili kuwatetema! Wengi wao baada ya yale maafa ya 1964 walikimbilia na kuzagaa Tanganyika,Kenya,Uganda na takriban kila kona ya dunia,huku wakiacha mali zao,ndugu na jamaa zao wa karibu mno mpaka kesho...kwani unafikri ni kwa kupenda!?

Khalaf,atokee kiwavi fulani ati adai yakuwa yeye ni Mngazija; tusonge mbele,hayo ni ya zamani,ebosi!?...mbele ipi hiyo twendayo na kwa haraka ipi tulonayo!? Tena huku tukikataa kujifunza yalotukuta nyuma,na kujua makosa yepi yalotendeka na walofanza ni wepi,na tumejifunza lipi katika kujirekebisha huko twendako!?

Kwetu sisi wengine History ni kitu muhimu kuliko vile nyinyi mnavyokhis!

Wenyewe tunajuana na tunajua yalotukukuta na dhuluma,mauaji tulofanziwa...na ubakaji walofanziwa Aunts zetu na ndugu zetu wengi mno tu wa kike hiyo 1964...na mpaka leo tuna ushahidi mwingi tu tena wa kina!

Imenilazim nikujibu kiduchu,nilipoona umejaribu kutoa hizo "nasaha" zako.

Ahsanta sana.

Cc;Bin Faza,Ritz,Boko Haram
 
rodrick alexander

Nimefurahi angalau wewe umefika zanzibar kwahivo unazungumzia zanzibar inayoijuwa kidogo, sio kama wengine humu wanapiga makelele matupu kumbe hata znz ilivokaa hawajui

sasa kuhusu wazo lako kwamba kuna wanasiasa wachache ambao wanatumiliwa na mataifa ya nje.........hili sikubaliani nalo na nahisi ni kama political statement tu

ukweli ni huu

1. wanasiasa wengi sasa huku znz hata walioko ccm wamechokeshwa na mtirirko wa mambo baina ya znz na tanganyika

2. hakuna taifa la nje linalowashawishi wanasiasa bali ni wasomi wetu sasa wamekuwa wakitathmini masuala ya muungano kuanzia 1964. na matukeo yaliojiri baada ya uchaguzi wa 1995, 2000, 2005, 2010

3. tathmini nyengine iliyofanywa ni ya matamshi yanayofanywa na viongozi wa tanganyika kupitia muungano,

tathmini mbili hizi zimeonesha wzi kwamba tanganyika haina nia njema na zanzibar, na hili hatuwezi kulistahamilia tena.

mfano mdogo katika uchaguzi wa 20000 majeshi ya msumbiji yalipelekwe pemba, tunaushaihdi kamili na hili, sasa kwanini wapelekwe majeshi ya msumbiji lakii kwanini wapeleke majeshi from the first place?

katika uchaguzi wa 2010, Dr sheni alikuwa tayari amekubali matekeo ya kushindwa, lakini mkapa na mzee mwinyi wakaja znz haraka wakalazimisha ccm ishinde, why? hili lilitokea pale pale hoteli ya bwawani, kwanini lazima iwe ni ccm tu, lazima kuna ajenda za siri dhidi ya znz

sasahivi hakuna kijana yoyote anayetamani kulisikia neno muungano hapa znz, isipokuwa tangayika bado inalazimisha, lazima kaka kutakuwa kuna ajenda za siri, au wewe unasemaje????

Bin Faza,

Hivi ni kweli nasikia siku hiyo ati Maalim Seif,alikuwamo mle ndani Bwawani na hao CCM "wakijadili",khalaf ati aliwatokea jamaa pale nje tena kwa bakora akiwataka wanyamaze na kumwachia yeye shughuli yoote!?... ni hapo nilipo-BOLD kwenye maelekezo yako.

Kama ni kweli Wallahi,wanasiasa si watu wa kuwaamini asilan kama tuambiavyo siku zoote!

Ahsanta.
 
gombesugu

Mkapa na Miwnyi walifika bwawani na wakazungumza na maalim na Dr shein kwa pamoja. inavosemekana maalim aliambiwa akubali kushindwa au znz itavamiwa kijeshi na balaa litakuwa kubwa zaidi

maalim aliweka maisha ya wazanzibari mbele na usalama wao wa baadae

Kwa maoni yangu Maalim alifanya busara kubwa sana siku ile, watanganyika wangetuuwa kweli
 
Wickama,

Nafikiri kuna wakti mwingine nakushauri gumzo/hoja nyingine uziache tu zipite,au uliza suali kiustaarabu na nina hakika wapo wanajamvi wastaarabu wengi tu watakujuza kwa utuvu na kitaaluma.

Wewe local politics,History,dasturi na tamaduni za kiZanzibary au Ki-Unguja nina hakika huzijui asilan,na pia si wewe peke yako!?

Ndo maana mimi siku zoote husema yakuwa; masuala ya Zanzibar na WaZanzibary,nyinyi WaTanganyika daima yatakupeni taabu ziso mipaka!

Huyo jamaa unayehitaji nimjibu khadith/hoja zake...nafikri umefuatilia kisa cha mimi kuanza kumuuliza lile suali moja tu...specific/legitimate question na pia kumnasihi!?...matokeo yake nimepata triangular explanations/excuses!?

Ni pale tu alipoyataja yale maafa ya Zanzibar 1964,na kuyaita ati ni "mapinduzi matukufu".

Hakuishia pale,pia kutilia nguvu hoja yake ikamlazim kutaja nasaba yake ati yakuwa yeye ni "Mngazija" na pia ni "Muislamu",tena na huku akinukuu vipande kadhaa vya Qur'aan na kutoa mifano ya Maswahaba!?ahahaa!

Yaani kwa kifupi,katumia tricks/methods kama zile ulizokua ukitumia wewe kwenye ule mnakasha ulokwisha!

Kipata fursa,nakusihi pitia post/s yangu niloanzia kuzungumza nae plse!?

Ndipo mimi ikanilazim kiduchu kumnyooshea maneno na kumuuliza,je yeye ni kati ya wale Wangazija pori!?

Nakufahamisha yakuwa;hakuna Mngazija au kizazi cha Mngazija yeyote duniani kitakachokaa leo hii ati kufurahia yale maafa ya 1964 au kuyaita "matukufu"...asilan,abadan!

Mpaka kesho Wazee wetu,wakitukhadith yalotokea hiyo 1964 mioyo huwenda mbio na miili kuwatetema! Wengi wao baada ya yale maafa ya 1964 walikimbilia na kuzagaa Tanganyika,Kenya,Uganda na takriban kila kona ya dunia,huku wakiacha mali zao,ndugu na jamaa zao wa karibu mno mpaka kesho...kwani unafikri ni kwa kupenda!?

Khalaf,atokee kiwavi fulani ati adai yakuwa yeye ni Mngazija; tusonge mbele,hayo ni ya zamani,ebosi!?...mbele ipi hiyo twendayo na kwa haraka ipi tulonayo!? Tena huku tukikataa kujifunza yalotukuta nyuma,na kujua makosa yepi yalotendeka na walofanza ni wepi,na tumejifunza lipi katika kujirekebisha huko twendako!?

Kwetu sisi wengine History ni kitu muhimu kuliko vile nyinyi mnavyokhis!

Wenyewe tunajuana na tunajua yalotukukuta na dhuluma,mauaji tulofanziwa...na ubakaji walofanziwa Aunts zetu na ndugu zetu wengi mno tu wa kike hiyo 1964...na mpaka leo tuna ushahidi mwingi tu tena wa kina!

Imenilazim nikujibu kiduchu,nilipoona umejaribu kutoa hizo "nasaha" zako.

Ahsanta sana.

Cc;Bin Faza,Ritz,Boko Haram

Yameisha Gombesugu. Salama lakini?
 
gombesugu

Mkapa na Miwnyi walifika bwawani na wakazungumza na maalim na Dr shein kwa pamoja. inavosemekana maalim aliambiwa akubali kushindwa au znz itavamiwa kijeshi na balaa litakuwa kubwa zaidi

maalim aliweka maisha ya wazanzibari mbele na usalama wao wa baadae

Kwa maoni yangu Maalim alifanya busara kubwa sana siku ile, watanganyika wangetuuwa kweli

Bin Faza,

Shukran kwa maelekezo ndugu yangu.

Maana sisi wengine umbea na mambo mengi hutupita.

Mambo ya kidunia wakti mwingine huleta simanzi nyingi mno...yaani yeye Bwana Ali Mwinyi ndo wakukaa na kushadidia vitisho dhidi ya Zanzibar na haki za Wenzie!?

Nakhis tuyache maana hapa si pahala pake,lakini nae pia tuna khabar zake ndefu na tunayajua yake mengi mno.

Ahsanta.
 
Yameisha Gombesugu. Salama lakini?

Wickama,

Salaam ndugu yangu.

Haina neno,kama siku zoote nisemavyo yakuwa sisi soote ni wamoja.

Ndo maana pia ni uzuri kuambiana kweli pale inapojiri.

Vipi Mfalme Obama kishaingia hapo,je atafika Mtae!?ahahaa!

Siku njema.

Ahsanta.
 
Gombesugu

Bin Faza,

Shukran kwa maelekezo ndugu yangu.

Maana sisi wengine umbea na mambo mengi hutupita.

Mambo ya kidunia wakti mwingine huleta simanzi nyingi mno...yaani yeye Bwana Ali Mwinyi ndo wakukaa na kushadidia vitisho dhidi ya Zanzibar na haki za Wenzie!?

Nakhis tuyache maana hapa si pahala pake,lakini nae pia tuna khabar zake ndefu na tunayajua yake mengi mno.

Ahsanta.

Naam funika kombe................

lakini yeye ijapokuwa kazaliwa tanganyika lakini kalelewa znz, Mangapwani, kasomeshwa na hata kupewa kazi na kufika nafasi kubwa wizara ya elimu ya zanizbar kabla ya mapinduzi. Inashangaza na kusikitisha, lakini tuyawache hapa penye kuku wengi hapafai kumwagwa mtama
 
Wickama

Mi nadhani at this point we can zoom down;

1. Bin Faza; Okello hayupo na harudi, Karume hayupo na harudi pia Nyerere. Tulishaulizana sana maswali kama haya katika mnakasha fulani. Hapa tutenge wahanga na kisa hiki na sababu za kisa.

YAANI; uhalali au uharamu wa WW2 sio idadi ya marehemu, bali ni sababu za kumpiga Hitler, wewe Bin Faza, kama utawala wa awali wa kisultani unaukumbuka unadhani mchango wake katika yaliyotokea januari 12, 1964 ni yepi?

2. Robo tatu ya wazenj wa sasa hawakuwapo wakati wa tukio lile, RED Xs, ni kweli kusema Wazenj wanataka warudishwe kwenye utawala wa familia ya Kisultani? Is this real? kwa kigezo kipi?

3. Katika hali ya kutoaminiana kama ilivyo sasa, kuna dhamana gani kuwa kundi moja halitajiona linadhulumiwa na kurudia tena ya 1964?

Bin Faza, RED Xs

kwani mimi sikubaliani na hayo, mbona hayo ni mawazo ya busara tu

isipokuwa pia ninakubalina na mawazo kwamba ikiwa hujui utokako, inawezekana hujui ulipo na definitely hujui uendako

haya mambo ya znz yana sura tofauti na WW2....kule baada ya vita wakapeana mikono wakaanza kujenga nchi na bara lao.....kwetu baada ya mapinduzi tunaona vimapinduzi vidogo vidogo vinaendelea kila baada ya miaka mitano.........kwahivo hatuwezi kuyasahau mapinduzi kwasababu bado hayajaisha

ahsante
 
Gombesugu

Naam funika kombe................

lakini yeye ijapokuwa kazaliwa tanganyika lakini kalelewa znz, Mangapwani, kasomeshwa na hata kupewa kazi na kufika nafasi kubwa wizara ya elimu ya zanizbar kabla ya mapinduzi. Inashangaza na kusikitisha, lakini tuyawache hapa penye kuku wengi hapafai kumwagwa mtama

Bin Faza,

Nakufahamu kwa yoote,chambilecho cha Shariff Ritz "nakusoma" kwa miwani ya 3D.

Hawa watu wengi wao ni Wazee wetu,na kuna wakti yatulazim tuwastiri kiduchu japo nyoyo zetu zabubujikwa na machozi.

Kama ulivosema tufunike kombe....maana hapa si pahala pake asilan!
 
afromwene

Hayaja rekodiwa live ni documentary sahihisha usemi wako na nidocumentary iliyotengenezwa kujibu waingereza na serikali ya bara.Imetengenezwa na waarabu na wafaransa unategemea nini soma zaid uliza wazee watakusaidia please narudia si live fikiria hali ya kisiasa iliyokuwepo kati ya mfaransa,mwarabu na mwingereza juu ya umiliki wa makoloni. Ukiangalia ya waingereza nayo inaonyesha ubaya wa waarabu TUWEMAKINI TUTAPOTOSHA UMMA

Mbona unaniangusha mkuu, fikra kama hizo zilitakiwa zitoke kwa hawa walioishia darasa la 7, kamada wewe msoni ndio hujui kwamba documentary zinakuwa pia kutoka live programs.............mfano wa documentary ya world cup finals si wananukuu zile live matches..........

lakini hii ya case ya genocide ya znz 1964 wazungu na wataliana walirikodi live sio documentary kama tujuwavo sisi.

au unachukusudia kusema ni kwamba watu hawakuuliwa huko znz mwaka 1964?
 
RED Xs

..ama labda sijaelewa..kwambamarco polo anasema "zanzibar wakaazi wake ni ni " weusi 'awana'(?) nywele za singa.." kama ni kweli hiyo inajitosheleza na ukweli wa uafrika wa zanzibar...lkn kuna jambo lingine moja..! muarabu, anakuwa muarabu kwanza.. sababu ya lugha..! ndo maana msiria au mlebanon, au au mjordan, au mpalestina mwenye haiba (hata wakati mwingine na macho ya buluu) ni mwarabu, na muirani ni muajemi..! naweza kukuuliza lugha ya wenyeji wa asili wa zanzibar ilikuwa ni kiarabu? kwa nini kiarabu si lugha kuu ya watu wa zanzibar kama ilivyo sudan, oman na nchi zingine ambazo kwa asili ni za kiarabu? kwa nini kiswahili zanzibar kama ilivyo (kwa kiasi kikubwa)karibu pwani yote ya afrika magharibi?..nashukuru kunitambulisha kitabu hicho, insha allah nitakitafuta nikisome kisha nilinganishe na vitabu vingine vya historia nilivyosoma...!

Sikusema kwamba zanzibar ni sawa na uarabuni, ukiwa utarejea makala zangu utakuta ninsema znz ni sehemu ya watu mchanganyiko. na sisi shatujisikii katik auafrika kama munavojisikia nyinyi huko tanganyika.

Ikiwa Marco Polo kasema kweli basi hiyo ni kuonesha dhahiri kwamba zanzibar ilikuwa ni sehemu ya watu mnyanganyiko tangu siku hizo......sababu mtu mweusi + nywele za singa nadhani mtu huyu anaweza kuitwa chotara..........mix ...kwani mwafrika ana nywele kipilipili.

Kumumbuka tu kwamba marko Polo alikuwa zanizbar mnano mwaka 1295.

sijui point yako hasa hapa uliposema mwarabu anakuwa mwarabu tu kwanza sababu ya lugha...........lakini nitapenda nisikubaliane na wewe kwamba lugha ndio inayompa mtu kabila yake..... ninao marafiki kibao tu hapo dar wenye asili za kinyamwezi, kichaga na kabila nyenginezo za mikoani lakini hawazungumzi lugha zao za kikabila, pengine na wewe ni mmoja katika kundi hilo. lakini bado huniambie mimi ni mchaga au mnyamwezi au kabila ingine lakini nimezaliwa na kukuwa dar siongei kiluga. sasa jee na hao utawasema sio watu wa kabial hizo kwasababu hawaongeo lugha za kabila zao......????

Pia sipendi ufikiri kamba labda hao waafrika waliokuwepo zanzibar miaka hiyo walipofika wasafiri wa kiarabu kama vile Masuud mwaka 916 walikuwa watanganyika. No walikuwa ni wazanzibari, na watanganyika walikuwa watanganyika ijapokuwa nchi 2 hizi zilikuwa na maina tofauti siku hizo

Kiarabu hakifanywa lugha kuu ya kwa zenj empire nadhani walikuwa na sababu hizo hizo kama waliokuwanazo wazungu waliokwenda kule afrika kusini........huku kwetu wakafanya lugha ya kiswahili ...mix kibantu + kiarabu..........kule afrika kusini wakafanya lugha ya Afrikaans..........mix lugha za kizulu + kidachi

Kitabu kizuri sana hiki, utaona mambo mengi ambayo watu wanapenda kudanganyana kila siku juu yao
 
Wickama

kwani mimi sikubaliani na hayo, mbona hayo ni mawazo ya busara tu

isipokuwa pia ninakubalina na mawazo kwamba ikiwa hujui utokako, inawezekana hujui ulipo na definitely hujui uendako

haya mambo ya znz yana sura tofauti na WW2....kule baada ya vita wakapeana mikono wakaanza kujenga nchi na bara lao.....kwetu baada ya mapinduzi tunaona vimapinduzi vidogo vidogo vinaendelea kila baada ya miaka mitano.........kwahivo hatuwezi kuyasahau mapinduzi kwasababu bado hayajaisha

ahsante

Faza; Hapa kwa kweli mimi Napata Darsa ya kunisaidia kuwaelewa huko mliko kwa hiyo wajibu wangu mkubwa kwanza ni kusikiliza tuu.

shukran sana
 
Back
Top Bottom