Haya ndio matokeo ya mwanangu darasa la saba nimefarijika sana

Vile vilitujenga sana mkuu.

Ndio tupo hivyo tulivyo.
Vimetudumaza sana mkuu angalia watu walivyo mafisadi yaani watu wanaiba vifaa vya hospital ya kwao kabisa ukiangalia ziara za viongozi ni kuongelea watu wasimamie miradi bila kuiba kila kukicha...
 
Utakuwa muhaya ama mtu wa kanda ya ziwa yani matokeo ya mwanao umeyafungulia uzi tena wa darasa la saba,, aisee
😂😂😂 nimeshangaa halafu mtoto mwenyewe hana A flat
Kuna mtoto wa sister nakaa naye yeye aliniambia mapema, mamdogo huo mtihani naondoka na A zote. Na kweli matokeo nimefanya kupigiwa simu na headmaster ananipa taarifa namwambia mwenyewe wala hashtuki!!!
 
Wapo ukumbini na sherehe ni kubwa sana mwendo wa kukata keki dogo kafaulu darasa la 7 B, Sasa huko mbele kuna fuka Moshi huo Moto wa huko mbele sio wa kitoto
Kumbe mzazi wake mwenyewe fala basi kwa kuhitimisha hiyo ni graduu ya manyumbu
 
Sasa darasa la saba nayo ni matokeo ya kuturingishia kweli,, hata ingekuwa chuo, sie tunataka maokoto hayo mavyeti yenye A ya kazi gani kwetu
 
Hivi na yy kafanya multiple choice kwenye mathematics?
 
Hongera sana, mkumbushe pia kwamba wewe si Alfa na Omega uwepo wako Duniani, jionbee maisha marefu na uweke akiba there is a what if question?
 
Shulen kwao hawakupewa majibu?

Ila sishangai, siku hizi hata Kidato Cha Nne, mtu anapata Div One alafu ana F ya Hesabu.
Nimeshindwa kuacha kumshangaa huyu ndugu yangu. Yaani kabla ya hayo anayoita matokeo mazuri alikuwa hajamfanyia assessment mwanae ili kufahamu ikiwa ana uwezo ama lah mpaka kasubiria matokea ya hisabati ya multiple choice?

Ana uhakika gani kuwa dogo hakupata support ndani ya chumba chumba cha mtihani ili naye aitangaze shule?
 
Kweli Kabisa...ila sio kilaza,ni slow learner! Mimi wa kwangu namjuw vizuri ..uwezo wake .Nilikwambia jitahidi upate A ,huko mbele ni kugumu! Unaweza usipate A maisha Yako yote! Nashukuru alielewa akapambana amepata A 3!😁
 
Huyo wa English medium na kuna wako wa kayumba wamepata A zote 5 na wana Grade A. Kiukweli sio sababu ya kulipa Mamlion ya ada halafu mtoto aje alingane au azikiwe matokeo na asielipa hata sumni ya ada!
 
Ni kumuombea tu mtoto aendelee hivyo, hizo sifa zingine unakausha.
Kuna Mpwa wangu kasoma kayumba katwanga A zote. Nyumbani akiambiwa asome ni shida. Akipewa mtihani anaukung'uta balaa.
 
Anapataje uraia "B" ......shabbash tia bakora huyo......
 
Hapo umeharibu ada tu
Kuna senti kayumba zimetoa A flat.
Mimi nilipata B Moja tu na A zote shule ya kijijini, na sisi tulikuwa batch la pili tangu shule ianze.
Inakuwaje English medium mtoto anapata B mbili na mzazi unachekea?
 
Hapo umeharibu ada tu
Kuna senti kayumba zimetoa A flat.
Mimi nilipata B Moja tu na A zote shule ya kijijini, na sisi tulikuwa batch la pili tangu shule ianze.
Inakuwaje English medium mtoto anapata B mbili na mzazi unachekea?
Naona St kayumba mnataka kujifariji hivi unajua kuwa hizo Pepa za Maarifa na Uraia wanazifanya Kwa lugha ya kiingereza au unadhani wamezifanya Kwa kiswahili?

Ukiizingalia hizo Pepa hazina tofauti na Pepa za form two

Na hizo Pepa ukiimpa huyo St kayumba aliyepata A flat anaondoka na zero

Nimesoma kayumba kuanzia darasa la kwanza Hadi form six huna la kunidanganya

Na Sasa huwa naangalia notice za wanangu na Pepa zao hakuna tofauti na yale Mimi niliyokuwa nasoma nikiwa form two
 
Hapo umeharibu ada tu
Kuna senti kayumba zimetoa A flat.
Mimi nilipata B Moja tu na A zote shule ya kijijini, na sisi tulikuwa batch la pili tangu shule ianze.
Inakuwaje English medium mtoto anapata B mbili na mzazi unachekea?
Watu hawalingani...bado mtoto anayesoma English Medium ana ufahamu na exposure kubwa kulinganisha na za kawaida! Ikiwemo Msingi Imara wa lugha ya Kgeni ..English!
 
Wenzio wanaonesha kama hayo lakini ya kidato cha nne. Mwanao bado yuko mbali, si pa kumsifia hapo.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Sasa darasa la saba nayo ni matokeo ya kuturingishia kweli,, hata ingekuwa chuo, sie tunataka maokoto hayo mavyeti yenye A ya kazi gani kwetu
🤣🤣🤣🤣 Maokoto ndio mpango mzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…