Haya ndio matokeo ya mwanangu darasa la saba nimefarijika sana

Hongera sn kwake,jitahidi kuzidisha dua maana dunia ya sasa hivi imejaa changamoto
 
Na asome hadi awe Profesa; katika jina la Yesu!
 
Wenzio wanaonesha kama hayo lakini ya kidato cha nne. Mwanao bado yuko mbali, si pa kumsifia hapo.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Mimi sijamsifia hata haya matokeo hajui kama Mimi nimeyaona maana sijamwambia chochote aliangalia akiwa na mama yake na mama yake ameniambia yeye mwenyewe alivyoyaona matokeo yake alifurahi sana

Ila pia Mimi kama Mimi nimefarijika na nilishamtafutia shule Moja ya Masister kabla hata matokea hayajatoka
 
Huyo ni kilaza pro max.
 
Hongera kwa jitihada...na kwa dogo pia. Lakini kubali tu mtoto amekuzidi akili na iwe fahari kwako sio wivu
 
Hongera zake naiona PCM na PCB imesimama hapo
 
Mama ana influence kubwa sana kwenye ubongo wa mtoto na intelligence yake na si baba , kwa kiswahili kisicho fasaha ni kwamba mtoto anarithi akili ya mama na si baba .
Mke wangu akili yake ni ya kuungaunga lakini nikicheki akili ya watoto wetu wako vizuri
 
Yangekua ya form four ningekusifu umepambana ila haya ya dalasa la saba ambayo hayana maana yyte
 
Hayo mabanda si kitu kama elimu haina global qualities na mbaya zaidi hayo mabanda yananunulika.tunachotakiwa kujivunia ni quality ya elimu na si quatinty. Kuna haja gani ya kupata la saba A, form four I. 7,form six I. 3 na university GPA ya 4.8 au 5 lakin baada ya yote hayo, mtu anakosa cha kufanya na kuishia kulalamika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…