Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
Tanzania ni Nchi yetu sote hivyo ni wajibu wa kujivunia vivutio vilivyomo.
Mlima Hanang uliopo Katesh manyara ni mlima wa Saba Kwa urefu hapa Tanzania
Nikiwa viunga vya huko niliona Nami nisiishie tu kuuona bila kupanda. Nikiwa na rafiki yangu mmsai tuliazimia kupanda kihuni (Bila kibali) Kwan mwenzangu alikuwa anajua njia za Chocho za kuupanda.
Safari ilikamilika tukiwa tumebeba vitu mhimu Kwa ajiri ya kupanda kwa mara ya kwanza tulipanda kiangazi kwenye mwezi wa8 Hivi na Kwa mara ya pili tulipanda mwezi wa kumi.
VIVUTIO NA MAAJABU YA MLIMA HANANG
Ukiwa mlima Hanang mwanzoni tu Kuna pori la miti asili mbalimbali mizuri sambamba na mirungi.
Japo hairusiwi kukata mti au Jani ama kitu chochote mle hifadhini lakini manyokaa sisi tulichuma mirungi ya kututosha na kuanza kutafuna.
Kuna matunda fln Hivi yanafanana Kwa mbali na dragon fruit pia utayaona msimu wake.
Hali ya hewa ni rafiki sana ukiwa mwanzoni mwa mlima lkn kadiri unavyozidi kupanda juu hubadirika kuwa na unarudi kiasi na miti hupungua kabisa.
Mlima Hanang sio mlima mmoja Kwa jinsi nilivyoona Mimi. Pindi unapopanda unakuwa unaona kileleni ni pale lakini ukifika pale juu unaona mlima mwingine Kwa mbele mrefu kuliko hapo ulipo.
Utaendelea kuona hivyo hivyo zaidi ya milima 9 ama 12 ndo unafika kileleni.
Kuna sehemu unapita Kwa umakini mkubwa sana kwani ikitokea ume umeteleza na kuporomoka sidhani kama utaweza kupona ama kuokolewa.
Ukikaribia kileleni Kuna mapango 3 tofaut na umbali yapo tofauti Yale mapango unaweza kaa ukalala kabisa au hata mvua ikiwakuta kule mnaweza kujihifadhi pasipo shida yoyote Ile.
Mawingu ya mvua daima yatakuwa yanawafunika na hii huambatana na ukungu na vimanyunyu Hivi.
Wingu la mvua ni sawa na ukungu mzito sana mwenzio akiwa mita5 Toka ulipo wewe huwezi muona au utamuona Kwa shida sana. (Picha zote zenye weusi ni Wakati tukiwa ndani ya ukungu mzito wa wingu la mvua)
Miti Ina harufu nzuri sana kule mlimani ya kijani kibichi muda wote vile vile Kuna miti kama Ile Xmass namna unavyouna mti wa Xmass na kule mlimani ni hivyohivyo sema wenyewe hauna Maputo na yule father Xmass 😆
Kule juu Kuna miti fln ukiangalia kana kwamba imekauka lakini ukivunja katawi kadogo unagundua ule mti ni mbichi kabisa Cha ajabu hauna majani yoyote.
Pia utaona mimea fln imekaa kama dodoki la kuogea inatililisha maji ya ubaridi meupe mazuri.
Ukichukua huo mmea na ukakamua nakunywa maji yake yenye ladha nzuri na ya kuvutia mnoo (SIKUJUA kama ni salama ama la japo mwenyeji wangu alinambia hayana shida)
Maji kutoka katika kati ya miamba. Hii pia utaona hasa ukifika sehemu yalipo pango no2-3 utaona maji yakitoka kwenye mwamba.
Kuna nyasi amazing sana huko juu yaani hata ukitaka kulala Haina haja ya kutandika nguo unajilaza vyema kabisaaa kwanza haziwashi yaani full amazing!! 🤩 🤩
Basi ukifika kileleni Sasa hata Katesh huioni Tena utakuwa unaona vijiji vya mbali sana Kwa ukaribu sana Nangwa utaiona nayo Kwa machale sana.
Ukiwa kileleni utaona ziwa la magadi sijui kama lipo karibu na mlima lkn ukiwa juu unaona kana kwamba ukiruka unatua kwenye Ziwa Hilo la magadi (chumvi)
Huu ubao upo Barbara kuu ya Arusha to siginda.
Miti yenye harufu nzuri ya kuvutia Sana. Msukuma Mimi ilibidi niifikishe kwenye nguo zangu walau harufu yake ibakie😹😹
Moja ya mapango yaliyomo mlimani huko juu ukifika hapa matumaini ya kutoboa ni makubwa sana.
Moja ya sehemu mbaya sana hapa ukiteleza kwisha habar yako.
Hapa ndani ya wingu ama ukunguku mzito sana.
Kama unavyoona Kwa mbali ndo Ziwa la magadi wengine huita Ziwa la chumvi.
Maelezo ya ziada.
Mlima huu unapo upanda daima utafuata mwinuko maana hivyo Huwa ni ngumu sana kutoboa ni mlima mkali wenye mteremko mkali kiasi kwamba iwapo jiwe litaporomoka lazima lilete madhara Kuna sehemu unapopanda unapanda kama mbwa yaani unatumia miguu na mikono Yako wiwili😂😂
Japo sio lazima ufanye Hivi lakini wengi hufanya hivyo kuragisiha upandaji.
Ukiwa pale mwanzoni Kuna vitu nilijiuliza sana. Unakuta mtu wa kienyeji kabisa lakini ule mti una jina la kizungu Hadi mirungi nayo Ina majina ya kizungu karibia Kila mti umeitwa majina majina ya watu wakuja ama ya mataifa ya kizungu huko!!
Nilijiuliza hii imekuwaje Hadi na migadogado Ina majina ya kizungu Ili Hali wenyeji wa eneo like wanaijua Kwa majina yake?
Nikakumbuka hata Ziwa Victoria lilinguduliwa na mzungu pia.
Karibuni.