Prince Kunta
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 22,797
- 28,904
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo imekAa poa sana na inamaanisha kwamba mashabiki wa yanga wana akili na mashabiki wa simba ni mbimbumbu+Hajji kawaponda wachezaji wa Simba. Cha kushangaza, wanaopiga mayowe, ni mashabiki wa Yanga. Imekaaje hiyo?
Nilikaribia kumpa hongera kwa kudhani amejifunza jambo muhimu sana kwenye shindano lolote lile, nalo ni kwamba dhamira ni zaidi ya uwezo. Lakini ghafla anageuka kuwa hjajifunza kwa kudhani kwamba pesa ndiyo hununua dhamira. Pesa hununua kitanda, si usingizi, hununua chakula, hainunui uhondo wa chakula, hununua mchezaji bora lakini hainunui uchezaji bora, hununua vichocheo vya dhamira ya ushindi - hainunui ari ya ushindi. Kama si kwa kurubuniwa kusaliti, hakuna mshindani anayeingia ulingoni bila ya dhamira ya ushindi. Lakini mazingira ya kabla, baada na ndani ya mchezo ndiyo yanayoifanya timu moja iizidi nyenzake kwenye ari ya ushindi. Kwa mechi ya jana, washabiki, vyombo vya habari (baadhi), wachambuzi (baadhi) na hata viongozi wenyewe wa Simba (baadhi) - akiwemo Manara mwenyewe - vimewanyima Simba ari ya ushindi na kuipeleka kwa Yanga. Kwa nini? 1. Fikiria tajiri mmoja anapita kijijini na kukuta msichana mzuri ambaye ameshachumbiwa na mwanakijiji waliyeafikiana wenyewe. Tajiri anavutiwa na uzuri wa msichana huyo na hapohapo ‘anapindua meza’. Unadhani huko mjini aendako msichana huyo atakuwa na nguvu ya kupigania ndoa yake iwapo kutatokea hitilafu japo ndogo tu? Sehemu kubwa ya usajili wa Simba, hata kama ni kwa mapendekezo ya benchi la ufundI, ni kwa wachezaji waliokuwa wametakiwa na Yanga. Wengine walikwishafikia hatua nzuri ya maafikiano, lakini Simba ikawatangazia maslahi bora zaidi. Wachezaji wa aina hii hata kama kwa asili wana mapenzi na Simba, watajikuta wamekwenda kufuata fedha zaidi na si kwa kuipigania Simba kwa sababu tayari walikwishaanza kujenga imani na Yanga wakati wa maafikiano ya usajili. 2. Wachambuzi wengi washabiki wa Simba waliibeza sana Yanga na kuwafanya ama watishike au waongeze dhamira mchezoni ili kuwaumbua wachambuzi hao. Kule kitanguliwa kwa mabao mawili kukawatia hofu zaidi Yanga, na wakalazimika kujituma (pengine kupita uwezo wao wa kawaida) ili kuondokana na aibu zaidi. Tambo za kupitiliza za Manara na wafuasi wake, akiwamo shabiki aliyeahidi nyumba yake iuzwe iwapo wasingeshinda mechi ile na fedha hizo wapewe Yanga, nazo zimewajengea zaidi Yanga dhamira ya ushindani kuliko fedha walizoahidiwa Simba. Kuna nadharia ya ‘diminishing ultimate utility’ kwamba hamu ya jambo lililo tunu hupungua kadri tunu hiyo inavyozoeleka. Fedha za bonasi wanazoahidiwa Simba zinapungua ari ya uhamasishaji kadri wanavyoendelea kuzipata, wakati nguvu za kejeli pitilizi za Simba zinaongeza ari kwa wachezaji wa Yanga kadri zinavyozidi kuwafikia. 3. Kejeli na dharau za wadau wa Simba dhidi ya Yanga zililishwa hadi kwa wachezaji wao,(angalia Kagere alivyoshangilia goli la kwanza, na wote walivyoshangilia goli la pili) ambao waliamini walishamaliza kazi waliyotumwa. Kejeli za wadau wa Simba zikawafikia na kiwahamasisha wachezaji wa Yanga (angalia ambavyo Balama hakushangilia goli la kwanza) ambao baada ya kulifunga wakaharakisha kwenda kuanza mpira ili watafute la pil. Na walipolipata angalia walivyoshangilia kwa ‘kuwapatia viuno Wanasimba’ badala ya kuhamasisha furaha kwa mashabiki wao. 4. Tambo za Simba kuwa na pesa zinawapelekea Yanga kuamini kwamba pesa hizo zinatumika hata kwa njia zisizo adilifu, ikiwamo kuhonga waamuzi. Sisemi kuwa hili linafanyika, lakini timu inapojisifia mno kuwa ina pesa haiwezi kuepuka kudhaniwa hivyo. Kwa hivyo matukio ya uamuzi wa jana hata kama ni sahihi yaliwaaminisha wachezaji wa Yanga kwamba mwamuzi alikuwa upande wa Simba na kwa hivyo wakaingia ari ya kumwonesha kwamba hataweza kuwatoa mchezoni. Nadhani ndio maana hata timu tajiri kama Man U, Real Madrid, Barca, PSG n.k. hazisikiki zikijivunia utajiri wao bali ubora wa timu, uongozi na huduma zao kwa vigezo vya mafanikio, si matumizi. 5. Wadau wa soka wa Tanzania hudhani kwamba kikosi kipana ni kukusanya wachezaji wenye uwezo mkubwa ulio sawa kwa kila nafasi, eti kupeana changamoto! Ingekuwa hivyo, wakati kufanya hivyo ni ama kutokuwa na timu moja ya kwanza inayozidi kuzoweana au kuua uwezo wa wataokosa nafasi kwenye timu moja ya kudumu. Kwa hivyo, mathalan, kuwa na Tshabalala na Gadiel ndani ya timu ni kupunguza uwezo wa atayekosa nafasi nyingi za kuanza. Na siku atayoanza kucheza atakuwa ni kivuli tu cha yule aliyesajiliwa awali, si yuleyule tena. Wachezaji wa aina hii ni wengi zaidi Simba kwa sababu ya matumizi ya siyo busara ya nguvu ya fedha kuliko walioko Yanga kwa sababu tu hawana uwezo wa kufanya hivyo. Isitoshe, wachezaji wa aina hii wanapokosa fursa ya kucheza mara kwa mara huwa ni fursa si ya kuvunjika moyo tu, bali ya kuanzisha chuki, fitina, majungu na utovu wa nidhamu ndani ya timu.
Tujue kwamba hiyo dhamira anayoisema Manara ilipungua kwa wachezaji wake kujengwa kwake ni sehemu ya mafunzo ya mwalimu. Angalia Diego Simeon,e mathalan, alivyo mahiri kwenye hilo. Kwa kauli yake hiyo, Manara anakiri bila ya kujijua kwamba mwalimu wao ni dhaifu na huenda anazidiwa na Mkwasa, angalau kwenye kuhamasisha timu ifanye vizuri.
Shukran. Nitafanya hivyo Manara atapowatolea tena povu Simba watapofungwa na Yanga!Mkuu mwangalingimungu ahsante kwa uchambuzi wako ILA nashauri kama unaweza ugawe uchambuzi wako katika paragraph 3 au 4.
Ahsante
"A leader says WE, not you or I". Amefeli sana kwa kuwayooshea vidole wachezaji.Haji ni mpumbavu na hana akili. Hao wachezaji wa simba si anaonana nao almost kila siku. Kulikuwa na sababu ya kuandika ujumbe kwa wachezaji wa Simba na kuuandika kwenye social media ? Only in Tanzania.
kwani hapo kakosea wapi? tuoneshe kosa liko wapi mtalaam wa kiswahili
Na yule mvaa power bank.Baadhi ya wachezaji wa Simba TAKUKURU wawachunguze...
Mwanzo wa Beno kupata nafasi
Mwanzo wa Beno kupata nafasi
Mwanzo wa Beno kupata nafasi