Haya Ndiyo Makobazi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HAYA NDIYO MAKOBAZI

Makobazi ni viatu vinavyovyaliwa kwa wingi na watu wa Pwani ya Afrika ya Mashariki.

Hivi ni viatu wanavyovaa wanaume.

Juu ataweka kofia pengine ya ya mkono.

Itafata kanzu pengine ya Dariz.

Juu ya kanzu linaweza kuja koti.

Chini ya kanzu utakuja msuli au saluni kwa jina lingine na chini atahitimisha kwa makobazi.

Kwa hakika hili ni vazi maarufu la Waislam lau mtu yeyote anaweza kuvaa akipenda.

Haikatazwi.

Bahati mbaya sana nimesoma mara kadhaa hapa JF viatu hivi kugeuzwa kuwa ndiyo alama ya Waislam na kwa kejeli Waislam wakaitwa, "Wavaa Kobazi."

Kivazi hiki cha kupendeza kikageuzwa kuwa tusi.

Mimi hujiuliza.
Uadui huu na chuki hizi zimetokea wapi?

Uadui huu na chuki hizi nini chanzo chake?

Najiuliza haya kwa kuwa naijua historia ya Tanganyika ilipokuwa inapigania uhuru wake harakati hizi zikiongozwa na TANU chini ya Julius Kambarage Nyerere.

Nyerere hakuwa Muislam lakini waliomtanguliza mbele wengi wao walikuwa Waislam na kivazi chao ni hayo makobazi kanzu na kofia.

Mwalimu kuna wakati akipenda sana kuvaa kofia ya mkono.

Uhuru ukapatikana mwaka wa 1961.

Tanganyika ikawa taifa huru lenye umoja na heshima yake ulimwenguni.

Hii chuki ya kuchukia Uislam na Waislam kiasi Muislam akapewa lakabu ya kiatu chake avaacho imetokea wapi?


Baraza la Wazee wa TANU 1957
 

Attachments

  • 1676728430545.png
    200.7 KB · Views: 28
Kama Kobazi kama ulivyoliweka hapo ambalo inaonekana zuri tu.

Sasa kwanini watu wa imani flani wakiambiwa wavaa kobazi wanakasirika na kuona kama wanakejeriwa ?

Kwani kobazi lina ubaya gani?

Au wange waita wavaa kofia?

Kobazi ni Vazi zuri ilitakiwa kama mnaambiwa wavaa Kibazi ilibidi muone kawaida kwani ni kweli mnayavaa.

Sasa ubaya uko wapi hapo ?
 
Che...
Ninayo majibu lakini staha inanikataza kukujibu hivyo kwani nami nitakuwa natukana.

Ukitumia akili yako kidogo tu utafahamu.
 
sema wazee wakiislamu wanna nuru mnooo.waupande mwingine sasa umkute amechomekea🤭🤭🤭🤭🤭🤭maamae utacheka
 
Mzee MS
Utaonekana unachochea kejeli kama hizi ikiwa utaona kwa upande mmoja. Siku hizi Vijana waliokosa adabu wapo katika kila jamii. Hujawahi kusoma Watu wa imani flani wakiitwa Wagalatia?
 
Tuna vaa kobaz kama alivyo vaa Yesu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Km hiz
 
Alafu sehemu nyingine kobazi ni aina fulani ya kitafunwa, unakula kupotezea muda.

All ni all issue ya mavazi, hayo makanzu sijui koti nk siyo mavazi yetu ni baada ya arab kuja wakaanza kuwavesha wazee wetu hizo nguo ka lazima ili kujisitiri.

Ukiangalia askali wa muingereza alikuwa akivaa kaputura na shati na raia anapiga suruali ma shati, nao wakatuachia hayo mavazi.

Hakuna kujisifia kwa lolote na kwa yeyote kuhusu mavazi.
 
Tuna vaa kobaz kama alivyo vaa Yesu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Sawa kobazi ni kiatu kuzuri tu. Sisi kule vijijini tulikuwa tunavaa kobazi za Matairi ya Gari na maisha alienda vizuri tu.
Nyi wenzetu mnavaa kobazi za Vervet toka China na Arabuni ambazo ni nzuri zaidi.

Sasa kwanini muone kuitwa wavaa kobazi ni kejeri ?
Ikiwa hata Yesu alivaa pia.
 
Hitimisho tunavaa kobaz kama alivyo vaa Yesu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ni identity tuu mzee wangu. Kwa tanganyika kobazi ni ustaarabu wa pwani ambao umesadifishwa na uislam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…