Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HAYA NDIYO MAKOBAZI
Makobazi ni viatu vinavyovyaliwa kwa wingi na watu wa Pwani ya Afrika ya Mashariki.
Hivi ni viatu wanavyovaa wanaume.
Juu ataweka kofia pengine ya ya mkono.
Itafata kanzu pengine ya Dariz.
Juu ya kanzu linaweza kuja koti.
Chini ya kanzu utakuja msuli au saluni kwa jina lingine na chini atahitimisha kwa makobazi.
Kwa hakika hili ni vazi maarufu la Waislam lau mtu yeyote anaweza kuvaa akipenda.
Haikatazwi.
Bahati mbaya sana nimesoma mara kadhaa hapa JF viatu hivi kugeuzwa kuwa ndiyo alama ya Waislam na kwa kejeli Waislam wakaitwa, "Wavaa Kobazi."
Kivazi hiki cha kupendeza kikageuzwa kuwa tusi.
Mimi hujiuliza.
Uadui huu na chuki hizi zimetokea wapi?
Uadui huu na chuki hizi nini chanzo chake?
Najiuliza haya kwa kuwa naijua historia ya Tanganyika ilipokuwa inapigania uhuru wake harakati hizi zikiongozwa na TANU chini ya Julius Kambarage Nyerere.
Nyerere hakuwa Muislam lakini waliomtanguliza mbele wengi wao walikuwa Waislam na kivazi chao ni hayo makobazi kanzu na kofia.
Mwalimu kuna wakati akipenda sana kuvaa kofia ya mkono.
Uhuru ukapatikana mwaka wa 1961.
Tanganyika ikawa taifa huru lenye umoja na heshima yake ulimwenguni.
Hii chuki ya kuchukia Uislam na Waislam kiasi Muislam akapewa lakabu ya kiatu chake avaacho imetokea wapi?

Baraza la Wazee wa TANU 1957