Haya ndiyo mambo ya ajabu niliyowahi kuona na kushuhudia kwa macho yangu, sitoyasahau katika maisha yangu

Ha ha [emoji23] [emoji1787]
 
Hizo ni hisia zako mzee siwajui wagang na wala Sina mahusiano na waganga kabisa Kama ndyo mchezo wako basi usifikiri kila mtu anamchezo Kama huo

Wewe umeona nimetaja waganga hapo??

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Mim wiki imepita usiku nimelala chali nikaota mtu kashuka toka juu ya dali kashuka kwa kasi akanikali halaf akainua mkono anataka kunipiga kibao ,kilikuwa kibao cha nguvuu sana ,sasa nikawa nataka kuudaka ule mkono kilikuwa kitendo cha haraka ile ananyanyua mkono kutaka kunipiga nikashtuka na kukaa [emoji2301][emoji2301][emoji2301] nikasali nikalala ubavu [emoji23][emoji23][emoji23] sasa sijui ndoto tu
 
Mi sijawah shuhudia ila ni kwa ndoto kuna nyumba niliwah kuish aisee ikifika usiku napata mawazo
Kuna mtu aliwah kunizawadia perfume basi ile usiku nimelala nikaota mtu ananiambia kasogea masikion usitumie hiyo perfume tupa,kisha humo chumbani nikawa nasikia mtu pembeni yangu anasoma Quran alisoma muda mrefu sana ila sauti ni ya kiume na hapo sas nataman kuamka ila siwez nakuja amka jasho linanitoka kweli
Ile nyumba nilikuwa nabebwa kabisa najisikia hivi ikifika tu saa saba usiku unashangaa unaishua nguvu nasikia nimekamatwa miguu na wengine mabega wananinyanyua naona wanawake kwa wanaume wamevaa nguo nyeusi ila uson siwaon sura nilikuwa nabebwa ile nyumba ukikosea ukasinzia tu kosa na nilikuwa najijua nabebwa ila nakiwa sijiwezi naanza kusali kimoyo moyo wananichia wakiniachia tu naamka hapo hapo nakaa
Nilihama hiyo mitaa siku hiz walaaa sijui ilikuwaje
 
Manyumba mengine Yana Mambo ya ajabu sana

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Usilale chalii 😂 hayo mambo yapo sana
 
Duh
 
kuna visa viwili vinamuhusu mtu mmoja ambaye alikua mchungaji kanisa moja la TAG lipo jirani na nyumbani kwetu.

kisa cha kwanza nimesimuliwa na Mama yangu. akasema kipindi me nikiwa mtoto mdogo bado nanyonya nikiwa nimelala kitandani mida ya jioni. anaingia chumba akakuta kuna nyoka mkuubwa kitandani upande wa miguuni. alichofanya hakuniacha akanikwapua then akatoka mbio. baba hakuwepo bahati kulikuwa na mgeni mzee mmoja pale home amelala. yule mgeni akamuua yule nyoka, then akatenganisha kichwa na kiwili wili. akachimba mashimo mawili shambani kwenye mahindi then kichwa shimo lake na kiwili wili shimo lake. kesho asubuh na mapema yule mchungaji wa kanisa akaja, akawa anauliza vipi kuna nyoka mmemuona? mama akahisi labda na yule mchungaji alikuwa amemuona nyoka, akamfukuza nyoka akakimbia akaja upande wa home. mama akasema ndio jana tulimuua nyoka.

Pastor. mlivomuua ikawaje?
mama. tulifukia.
pastor. wapi?
mama. shambani
pastor. twende ukanioneshe.

mama akashangaa ila akaamua ngoja aende. akampeleka shamban akamuonesha. pastor akaomba jembe then akafukua. akatoa kichwa kwenye shimo lake, then akaja akafukia kwenye shimo la kiwili wili. ikaisha hiyO na maswali mengi kwa mama.


kisa cha pili nilipokua shule ya msingi kuna ndege mmoja alikuja kwenye lile kanisa la pastor. yule ndege alikua anakaa mule kanisani 24/7. hatoki nje. sisi daily tulikua tunacheza ktk uwanja wa kanisa na kanisa lilikua lina madirisha yana flem za nondo hakukuwa na vioo. so sisi tukawa tunampiga mawe kupitia dirishan lkn hatoki. alikuwa anahama kenchi moja kwenda jingine lkn hatoki. alikaa mle karibu wiki 2 ndo hatukumuona tena. na aina ile ya ndege me sijawahi kuiona mpaka leo. kwetu ni kijijini na tulikua tunawinda, so nmeona ndege wengi lkn aina ile sijawah ona.

Fast foward miaka Mingi baadae yule pastor alikuja kufariki kifo cha ghafla tuu kilichoacha maswali mengi.
 
Yaani Kuna watu huwa wanaunganisha uhai wao na wanyama au ndege aise.
 
[emoji16] ungeacha akupige
 
Nimeshuhudia jamaa alikuwa analima shambani kwetu kwa ng'ombe
katika kulima nikamuona nyoka nilivyomuita huyu mlimaji akatafuta kijiti akamgusa nyoka, alivyomgusa nyoka akakauka
Du Kuna mijitu Ina uwezo[emoji91]
 
Niwashauri tu kwa wale wanao penda kulala chari, aisee hilo ni kosa kubwa
Kulala chari Mara nyingi Huku kwetu Kanda ya Ziwa huwa tunasema mtu anaye lala chari maana ake lazma aote Ndoto mbaaya kama kukimbizwa au kuota watu walokufa , so ukitaka kulala lala chari tu ujiengeshe ila usingizi usikupitie
 
Duh
Ajabu kweli
 
Darasa la 6 nilitoka kukesha msibani asubuhi sana,wakati narudi asubuhi sana pembeni ya kaburi la yule marehemu nilimuona baba mrefu sana ana kanzu nyeupe sana na kofia ndefu kama kindoo ya barakashia.Nilipiga jicho Mara moja nikakimbia nyumbani na kugonga mlango.Hayo madude yapo wadau
 
Bora ulivyothibitisha mkuu Kuna watu wanadhani ni stori zakutunga
 
Uchawi hauendi kwa muhuni leo nimeamin
Et mtu anakuta hela njiapanda anaogopa kupita nayo
Mimi nilishapita nazo sana hizo mpaka nikatengeneza kautaratibu nadamka asubuhi sana natembelea njia panda zote napita nazo na sikudhurika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…