NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,587
- 13,425
- Thread starter
- #221
(9) NILIWAHI KUWA KWENYE MAHUSIANO NA BINTI MMOJA NILIYEMUOTA KWENYE NDOTO KABLA YAKUKUTANA NAE.
hii dunia Ina maajabu na kila mwanaadamu ana maajabu yake au uwezo aliopewa na mungu, hizi stori ninazo Shea hapa jukwaani ni Mambo yaliyonitokea na yanayoendelea kunitokea katika maisha maana bado naishi.
Ipo hivi, miaka minne iliyopita nilikua napiga mishe za kufundisha ujasiriamali sehemu mbalimbali.
Siku moja nililala nikaota njozi moja nipo maeneo ya relini sehemu ambayo sijafika kabla nikiwa pale relini nimekaa Mara alitokea binti mmoja alikua amesuka nywele msuko wa twende kilioni, mfupi wastani na ni maji ya kunde, ndoto ilinionesha Yule binti alitabasamu na Mimi nilivutiwa naye ndipo nilipoamua kumuita akanisogelea nikaanza kuzungumza nae nilimuambia maneno mawili tu nakupenda nahitaji uwe mpenzi wangu
Yule binti alicheka sana nilimsogelea nikamshika mkono alinyamaza kucheka akaanza kuona aibu na ndipo nilishituka katika hiyo ndoto.
UHALISIA KATIKA MAISHA YAKAWAIDA.
baada ya Kama wiki kupita nilisafiri kwenda Kijiji kimoja kinachoitwa idodi, nilifikia gest moja pale center kutokana na uchovu siku hiyo sikutoka kwenda sehemu yoyote.
Kesho yake nilitoka kwenda kutembea nakuangalia mazingira lakini katika pitapita nilijikuta nimetokea maeneo ya relini nilisogea mpaka kwenye reli lakini nilipokua nimesimama Mara gafla nilimuona binti wa dizaini ile ile niliyemuona kwenye ndoto takiribani wiki moja iliyopita.
Akili yangu ilikumbuka mpaka maneno niliyozungumza nilistaajabika sana nikajisemea kimoyomoyo hebu ngoja nijaribu kuzungumza Kama nilivyozungumza kwenye ndoto.
Nilimuita Yule binti akaja mpaka maeneo niliyokuwa nimesimama pale relini baada ya salamu sikutaka kuzungumza mengi nilimwambia Mimi nakupenda nahitaji uwe mpenzi wangu.
Alicheka sana Kisha nilimsogelea Kama nilivyofanya kwenye ndoto, aliponiona nipo karibu alinyamaza nakuanza kuona aibu, kumbuka ndoto iliishia hapo
Pale pale nilimwambia nipe namba yako ya simu alininipa na Kisha tukawa tuna wasiliana mwisho wa siku akawa mpenzi wangu kabisa.
Kwa upande wangu nilikua najiuliza sana juu ya huyo binti, maana mazingira tuliyokutana ni mazingira Yale yale, na usukaji wake ni ule ule tofauti ni mavazi tu maana wa kwenye ndoto alijifunga lubega lakini wa kiuhalisia alivaa mavazi ya kawaida tu.
Mwanzo nilikua namuhofia hata kulala nae nilihisi anaweza akawa ni jini lakini nilipomzoea niliona kawaida tu, nilitembea nae sana na hakuna baya lililonitokea.