- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimeona kuna hizi jumbe ikiambatana na picha ikionesha matukio yanayofuata baada ya kupatwa kwa mwezi lilitokea Septemba 6, 2025.
- Tunachokijua
- Septemba 7, 2025 maeneo mbalimbali ulimwenguni waliata nafasi ya kipikee ya kushuhudia kupatwa kwa mwezi (Lunar eclipse), miongoni mwa watu waliopata bahati hiyo ni watanzania ambapo tukio hilo lilitanganzwa na mamla ka ya hali ya hewa nchini (TMA)
Madai
Mara baada ya tukio la kupatwa kwa mwezi, imekuwepo taarifa inayosambaa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na Facebook ikiwa na grafiki inayoonesha matukio yatakayofuata mara baada ya lile la kupatwa kwa mwezi.
Miongoni mwa matukio yaliyoanishwa ni pamoja na kupatwa kwa jua Septemba 21 (Partial Solar Eclipse), Septemba 22, Usawa wa msimu wa vuli (Autumn Eiqunox), Mvua ya nyota mchana (Daytime meteor shower) Septemba 27 yote yakitarajiwa mwaka 2025.
Uhalisia wa Taarifa hiyo ni upi?
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa ni kweli kuwa matukio hayo yanatarajiwa yatatokea kwa nyakati tofauti kama taarifa zilivyoeleza.
Kuhusu kupatwa kwa jua, Tovuti ya mambo ya anga ya nchini Marekani (NASA) imechapisha taarifa inayodokeza kuwa watu wawe tayari kwa ajili ya kupatwa kwa jua, Septemba 21, 2025 ambayo haitakuwa kamili itakuwa ni kiasi tu. Maeneo itakapoonekana ni Australia, Antarctica, bahari ya Pasifiki, bahari ya Atlantic.
Kuhusu usawa wa msimu wa vuli, hili ni tukio ambalo kitaalam linajulikana kama Autumn equinox ikiwana maana kuwa usiku na mchana kuwa sawa, ikiashiria kubadilika kwa msimu kutoka kiangazi kwenda vuli (kwa kaskazini), na kutoka baridi kwenda masika (kwa kusini).
Kwa mujibu wa tovuti ya mambo ya anga ya nchini Marekani (NASA) inaeleza kuwa kwa mwaka tukio hili hutokea mara mbili yaani mwezi Machi na Mwezi Septemba na kwa mwaka 2025 ilitokea Machi 20 na inatarajiwa kutokea tena Septemba 22.