mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Ni mawazo yangu tu kuhusu mpango wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda. Tangu mpango huo uanze kumekuwa na hisia na uelewa tofauti katika jamii yetu, kiasi kwamba kuna mikakati tofauti ya utekelezaji na kebehi nyingi tu, hasa kutoka upinzani, hadi humu wanajamvi wanaita 'viwonder'.
Tukio kubwa zaidi ni la hivi karibuni ambapo Rais JMT alizuia mpango wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) wa ujenzi wa hoteli ya kifahari ndani ya Uwanja wa Kimataifa ya Biashara, maarufu kwa jina la Sabasaba. Rais akizuia ujenzi huo alisema, nanukuu:
Kwa nini mnataka kujiingiza katika biashara ya hoteli na bia? Ili watu walewe na kupigana humu? Haiingii akilini. Wao ndiyo wabatusisitizia biashara na viwanda na dhumuni la mwaka huu ni kukuza biashara kwa maendeleo ya viwanda'. Sasa wao badala ya kuzungumzia viwanda wanataka kujenga hoteli na majengo mapya hapa?. Ni kauli ya Rais ambayo siyo tu inatoa ufafanuzi sahihi wa uchumi wa viwanda, kwa mifano, pia isisitiza kubadilika kifikra kwetu sisi wote.
Najiuliza, kama viongozi wa TanTrade bado wana fikra za kutangaza biashara na siyo uzalishaji, je, hawa wazalishaji wa hizo bidhaa watawaza nini?
Hata vile mwelekeo wa uchumi wa viwanda unashika kasi inayoridhisha. Kwa wale waliokwisha kufika kwenye viwanja vya Sabasaba, au kuangalia kwenye luninga, hakika maonyesho ya mwaka huu yana bidhaa nyingi za viwanda vidogo vya wajasiriamali wa Kitanzania. Aidha kuna biadhaa nyingi tu za mazao ya shambani zilizoongezewa thamani km vyakula vilivyosindikwa.
Ikumbukwe kwamba wakati wa maonesho ya miaka ya nyuma sehemu kubwa ya bidhaa zilikuwa zikitoka nje. Waliokwenda kwenye maonesho nia hasa ilikuwa ni kununua hizo bidhaa, na kuna wakati watu walipanga foleni kuvinunua. Na ni bidhaa hizo hizo zilizozalisha Machinga.
Rais akizuia mpango huo wa ujenzi wa hoteli, aliushauri uongozi wa TanTrade kama wana fedha hizo, basi wazitumie kuwekeza kwenye viwanda.
Pamoja na ushauri wa Rais jwa viongozi wa TanTrade kujenga 'kiwanda cha mfano', fedha hizo zinaweza pia kutumika kuimarisha viwanda vidogo vya wajasirimali, ambao kwa kiwango kikubwa wametoa mchango unaoonekana kwenye maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu. Hii inaweza kufanyika kila mwaka, katika maonyesho hayo, kwa njia ya mashindano, sambamba na mashindano ya mabanda bora. Zawadi isiwe tu vikombe ila mitambo ya kuzalishia, au fedha ambayo washindi wataitumia kuongeza mitaji.
Hivyo basi, hoja yangu hiyo kwa viongozi wa TanTrade inagusa pia Makampuni yanayochezesha bahati nasibu, hasa hayo ya simu, yabadilike kwa kufikiria kuchezesha bahati nasibu ya wajasiriamali, waliowekeza kwenye viwanda, ili zawadi watakazotoa kwa washindi wazitumie kuboresha, kuimarisha na kukuza viwanda vyao.
KUPANGA NI KUCHAGUA