Haya ndo Makosa huyafanywa wakati wa kutengeneza "Password"

Haya ndo Makosa huyafanywa wakati wa kutengeneza "Password"

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Makosa Unayofanya Unapotengeneza Neno la siri:
  • Kutumia Jina lako au Tarehe yako ya kuzaliwa
  • Kutumia Neno la Siri moja kwa akaunti zako zote
  • Kutumia herufi peke yake
KUMBUKA
Unapounda neno la siri, hakikisha unatumia herufi kubwa na ndogo, namba, na alama za uandishi kwa usalama zaidi.

Epuka kutumia taarifa kama jina lako au tarehe ya kuzaliwa kwani ni rahisi mtu kutambua. Pia, tumia neno la siri tofauti kwa kila akaunti yako ili kuongeza usalama katika kifaa chako.

Kumbuka kutumia programu za kuhifadhi neno la siri zilizopo kwenye vifaa vyako kwani zitakusaidia kukumbuka nenosiri zako pale unapozisahau.
 
Labda niwe naziandika hzo password then n secreen shot nikiwa naziitaji kutumia niangalie Kwa gallary ,kusema Kila password uweke kichwan na vichwa vyenyewe hv tutapotezana mkuu
 
Kuna Mtandao niliweka namba za siri za Mwaka wa kuzaliwa..... Nikatumiwa meseji mfano wa uzi wako NDUGU MTEJA USITUMIE MWAKA WA KUZALIWA KAMA NAMBA ZA SIRI.......
 
Hivi hakuna app ya kutunzia password tofauti maana mimi na kubadili passwords ili niweze ku_log in ni mapacha
 
LinkedIn,GSMArena,Gmail,Yandex,Protonmail,EasyFirmware,JF,PhoneArena,Western Union,S-Manuals,Udemy........hapo sijamaliza list
 
Makosa Unayofanya Unapotengeneza Neno la siri:
  • Kutumia Jina lako au Tarehe yako ya kuzaliwa
  • Kutumia Neno la Siri moja kwa akaunti zako zote
  • Kutumia herufi peke yake
KUMBUKA
Unapounda neno la siri, hakikisha unatumia herufi kubwa na ndogo, namba, na alama za uandishi kwa usalama zaidi.

Epuka kutumia taarifa kama jina lako au tarehe ya kuzaliwa kwani ni rahisi mtu kutambua. Pia, tumia neno la siri tofauti kwa kila akaunti yako ili kuongeza usalama katika kifaa chako.

Kumbuka kutumia programu za kuhifadhi neno la siri zilizopo kwenye vifaa vyako kwani zitakusaidia kukumbuka nenosiri zako pale unapozisahau.
Elimu nzuri sana hii
 
Kichwa changu kina passwords kama Ishirini hivi plus na mambo ya dunia aisee ubongo una GB zisizohesabika...sishauri uwe na passwords nyingi nyingi tofauti kabisa utadata.
 
Tumia google ku save passwords Mkuu, japo mtu akishika hicho kifaa anaweza fanya maajabu kiurahisi sana
Tatizo mkuu maana kuweka auto save ni hatari sana kama mtu akipata access ya kifaa chako, ndio maana nilitaka app ambayo security yake ipo fresh kiasi unaweza weka passwords zako zote. Halafu ukakariri password ya hiyo app tu
 
Back
Top Bottom