Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kukufanya ukapokea mapigo kutoka kwa maadui zako wa kiroho

Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kukufanya ukapokea mapigo kutoka kwa maadui zako wa kiroho

third eye chakra

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2023
Posts
713
Reaction score
1,745
Mambo au Tabia Zinazofanya Kufifisha au Kudhoofisha Malango Yako/Nishati ya Ndani

1. 😞😞 Uzinzi au Ngono Hulela

Ni vyema kuwa na mke/mume au mtu mmoja kwa nia ya mahusiano na sio kutangatanga. Mara leo uko huku, kesho kule, hapo utavaa karma nyingi ambazo hazikuhusu. Sio kila umuonae anakufaa au ni binadamu; wengine ni majini yamevaa miili ya watu.

2. 🤔 Ulaji wa Nyama Kupita Kiasi

Kwa mtafutaji wa nuru ya kweli, ni vyema kupendelea kula vitu vyepesi kama mboga mboga.

3. 😎 Matumizi ya Vilevi Vikali

Matumizi ya pombe kupita kiasi, sigara, na vilevi vingine vikali vinaweza kudhoofisha nishati yako.

4. 😞😞 Kutamka Maneno Hasi kwa Watu, Kuwa na Mawazo Hasi

Unapowaza au kusema jambo hasi, ulimwengu nao huwa unakuletea hayo unayowaza au kutamka. Ukiwaza kuloga, utalogwa kweli; ukisengenya, nawe utafanyiwa hivyo.

5. 👉 Matumizi ya Bidhaa za Viwandani

Bidhaa za viwandani nazo hufunga malango kwa wepesi.

6. 👉👉 Maagano ya Ukoo, Mizimu nk.

Kutokana na karma ya vizazi ndani ya ukoo, matamko ndani ya vizazi hivyo yanaweza kukufunga usipige hatua yoyote. Hii inamaanisha unapaswa kuabudu mizimu na kuifanyia inavyotaka ili usiendelee kufungwa.
FB_IMG_17028427190130106.jpg
 
Uzinzi unazima Sana mambo ya kiroho , kuna wakati hukitaka kuisafirisha akili inagoma ujue uzinzi umekukwamisha.

Pia hata chakra -kupitia via vya uzazi inajifunga.

Japo himaniishi ukiwa mzinzi utaishi kwa mateso hamna unaweza kuishi tu na ukapata vya kusaza.

Ila kwa watu wenye nia ya kuishi katika Nuru uzinzi haufai .

Kuhusu maneno hasa negative statement it is true , hakuna uchawi mbaya Kama kujinenea maneno negative au kuwanenea watu negative statement ujue it will turn back and ruin ur life

Kuhusu nyama - hii spiritually hasa katika kufungua third eyes sio nzuri Sana .

NB :ulimwengu wa roho hauna mipaka hivyo kila MTU huongea kile ambacho kinafanya kazi kwake

Ila ukiweza kuwa positive kwa mambo yote utaona nguvu kubwa inaanza kukaa upande wako
 
Hiyo ya ngono nakubaliana nayo kabisa, hiyo ya kujinenea mema mhhh.... kuna watu wamejiita boss, tajiri, manoti, bahati, akili kubwa, muwekezaji, pisi kali, bosslady na hawana maajabu yoyote japo wanajinenea positive, na kuna watu wanasemaga hawana hela ila wana maendeleo balaa, which is which?
 
Back
Top Bottom