Haya ni mambo manne Yanayoweza kuchelewesha usajili wa Kampuni yako

Haya ni mambo manne Yanayoweza kuchelewesha usajili wa Kampuni yako

Luhamba II

Senior Member
Joined
Mar 22, 2025
Posts
137
Reaction score
219
Usajili wa Kampuni unaweza kufanyia ndani ya muda mfupi sana, lakini Kuna sababu kadhaa zinazoweza kupelekea usajili kuchelewa, kwenye article hii nimekuandikia baadhi ya mambo hayo.

1. Utoaji wa taarifa nusu nusu
Hii imenitokea mara kadhaa, mteja anakupa taarifa nusu, mfano ananipa taarifa za shareholder mmoja alafu anasema nisubiri taarifa za shareholder mwingine.

Hii inafanya kazi ya usajili wa Kampuni ichukue muda mrefu sana.

2. Brela ORS system failure
Hii ni changamoto ya kila siku, Kuna wiki unakuta system ya Brela inasumbua siku 4 mfululizo.

Mfano jana nimetumia masaa 6 nikijaribu ku download consolidated form bila mafanikio, hii inafanya usajili uchelewe.

3. Uandaaji wa documents
Uandaaji wa documents unaweza kua wa shida sana pale ambapo mteja hajui mgawanyo wa hisa au capital ya Kampuni husika.

4. Kuchelewa ku sign forms
Watanzania wengi hawatumii digital signatures, sasa unatumia mtu documents aweke sign anakaa nayo 3 days ndo anarudisha, hii inafanya kazi ya usajili iweze kuchukua muda mrefu.

Hizi ni Sababu nilizokutana nazo Mimi mwenyewe wakati wa kufanya kazi ya usajili wa Kampuni hivo zimetokana na experience binafsi.

Hello, naitwa Luhamba Mimi ni mwanasheria na agency freelancer nawasaidia wafanya biashara kama wewe kusajili biashara leseni na Kampuni,

Kama unahitaji consultation zaidi kuhusu usajili wa Kampuni biashara au leseni unaweza kunitafuta WhatsApp au simu kwa namba 0678131068

Your Favorite Lawyer.
 
Gharama za kusajili kampuni zipoje mkuu? Itapendeza ukiziainisha hapa
 
Mleta mada, Angeweka na vitu muhimu kwa ujumla vinavyohitajika kusajili kampuni
Huwezi kusajili kampuni kwa taarifa nusu nusu,labda kama unatumia mtu wa kati,maana mtu wa kati atakusubiri mpaka ulete taarifa zote ndiyo aanze taratibu za kwenda Brela, wakati unaleta hizo taarifa nusu nusu hawezi kukuambia kama hizo taarifa ni nusu kwa sababu ni biashara atakuhimiza kuleta nyaraka nyingine ili kukamilisha usajili,lakini mtu wa kati hawezi hata mara kukuambia taarifa zako ni nusu
 
Tunahitaji kujua, ili ufungue. kampuni, unatakiwa ufanye yafuatayo
1>..............
2..............
3............... na kuendelea
 
Ndugu mwanasheria naomba unipe maelezo yote muhimu ya vile naweza kusajili taasisi ya Elimu(shule) inayomilikiwa na taasisi ya kidini katika mifumo ya Brela.
 
Back
Top Bottom