Haya ni mambo ya kuzingatia uwapo mtandaoni ili kulinda taarifa zako binafsi kutumiwa vibaya na watu wenye nia ovu

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
mambo_ya_kuzingatia_uwapo_mtandaoni_ili_kulinda_taarifa_zako_binafsi.jpg

Wapendwa wana JamiiForums,

Tunafurahia kuwa sehemu ya jamii yetu inayoheshimu faragha yenu kwa kuwaruhusu kutumia majina bandia ili kuwa huru kutoa maoni yenu na kushiriki mijadala kwa namna mbalimbali.

JF kama mitandao mingine ya kijamii inakutanisha watu wa aina mbalimbali, wenyewe nia tofauti tofauti, mbali na JF kuchukua tahadhari zote kulinda wanachama wetu, ninyi pia mnawajibika kwa upande wenu kuchukua hatua stahiki kuhakikisha upo salama wakati wote.

Unapojisajli kwenye mtandao wowote, huwa kunakuwa na sera ya faragha (privacy policy) pamoja na vigezo/masharti (terms & conditions) zinazoelezea taarifa zinazokusanywa kwenye program/mtandao huo na vigezo vyao na jinsi gani taarifa hizo zinatumika, ambapo kama hukubalini na vigezo hivyo upo huru kutojiunga nao. Ni muhimu kusoma vigezo hivyo ili ujue unatoa taarifa gani kwao na jinsi gani zinatumika ili kulinda taarifa zako zisije kutumiwa vibaya.

Kwa upande wa JF sera ya faragha na vigezo zimeeleza wazi taarifa tunachukua ambazo ni zile unazotumia kujisajili yaani jina lako/user name yako unatumia kujisajili, barua pepe (email address) unayotumia kujisajili ambayo pia inatumika kuwasiliana na wewe ili kuboresha huduma zetu, siku na tarehe, browser unayotumia pamoja na operating system zinazotusaidia kuboresha huduma kulingana na kifaa chako, na taarifa nyingine utakazoamua kutushirikisha ambazo utajaza kwenye profile yako.

Sera hii imekueleza vizuri jinsi taarifa hizi zinavyotumika kwa kurefu pamoja na haki zako juu ya taarifa hizi, na la muhimu una chaguo, ikiwa haukubalini na sera hii uko huru kutotumia JF.

Je, unatakiwa kuzingatia nini ili kuhakikisha wewe kwa nafasi yako pia unalinda taarifa zako binfasi?

Usiwe mwepesi kutoa taarifa zako binafsi kwenye mijadala au kwa njia ya kutumiana ujumbe (PM): Chukua tahadhari kabla ya kutoa taarifa kama majina, namba za simu, au anwani yako kwa mwanachama au wanachama wenzio, hata kama mnawasiliana kwa Private Messages (PM). Si kila atakayekufuata PM atakuwa na nia njema na wewe.

Chukua tahadhari watu unaoamua kujenga nao urafiki mpaka kufikia hatua ya kufahamiana na kutembeleana nje ya mtandao. Mtandaoni au nje ya mtandao taarifa zako na usalama wako ni jambo la muhimu.

Epuka kuweka taarifa zako binafsi kwenye maandiko yako: Baadhi ya watu kwa makusudi au kwa kujisahau huambatanisha namba zao za simu, majina halisi, au taarifa nyingine za binafsi kwenye maandiko yao. Jambo hili linaweza kufanya wenye nia mbaya kumfahamu na kuutambua utambulisho wako, labda kama wewe ni mfanyabiashara ambapo ili biashara hiyo iweze kufanyika lazima uwasiliane na wateja wako, japo pia ni vizuri kuwa makini.

MUHIMU:
Ingawa JamiiForums inaheshimu na kuahidi kulinda taarifa binafsi za wanachama wake kwa uwezo wake wote kwa kuzingatia Katiba ya nchi, ulinzi imara wa faragha zako unaanza na wewe mwenyewe. Kuwa makini na namna unavyoshiriki mijadala yako na taarifa unazozitoa jukwaani au kwenye mitandao mingine. Kumbuka faragha yako ni utu wako.

Kwa pamoja, tunaweza kuifanya JamiiForums izidi kuwa salama kwa kuchukua tahadhari zote za msingi.

PIA SOMA
- Unatumia njia gani kulinda data/taarifa zako binafsi kwenye simu yako?

- Ulinzi wa Faragha ya Taarifa Binafsi ni Haki ya Msingi ya Binadamu
 
Iko poa sana.
 
Wapendwa wana JamiiForums,

Tunafurahia kuwa sehemu ya jamii yetu inayoheshimu faragha yenu kwa kuwaruhusu kutumia majina bandia ili kuwa huru kutoa maoni yenu na kushiriki mijadala kwa namna mbalimbali...
Haya bana JF tumewaelewa
 
Wabaya wengi hutumia jukwaa la MMU kuwadaka watu. Mtu anajifanya bebe, unampa details zote mpaka mnakufana physically.

Ndiyo maana mimi nimefunga pm yangu, hakuna mbwa wala paka yoyote anayeniPM.
 
Usiwaweke waja wa M/Mungu katika kapu moja.
Kuna wabaya na wazuri, hivyo mchuje mtu kutokana na sifa yake.
 
Back
Top Bottom