hata mimi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 1,356
- 1,442
Kuna maneno mawili ambayo ukiyachukulia kikawaida unaweza kuyadharau sana lakini ni maneno ya muhimu sana kuyatumia kwenye maisha yetu ya kila siku
1.SAMAHANI
Vyovyote utakavyoiweka iwe kumradhi, nisamehe, niwie radhi, tafadhali nk; ilimradi tu uoneshe kukiri/kujutia kosa ulilofanya, kumtaka/kumwomba uliyemkosea asikuchukulie kwa namna ulivyokosea na kunuia kutolifanya tena kosa hilo. Hali hiyo inajenga sana jamii na inaunga palipo katika
2.ASANTE
Iwe nashukuru, ubarikiwe, shukrani, MwenyeziMungu akuzidishie, nk... ilimradi tu kuonesha umethamini huduma au msaada uliopatiwa basi jambo hilo litakuunganisha sana na ulimwengu hadi utashangaa
Mbali na hayo kuna mengine madogo madogo pia ambayo yana positive impact kubwa sana kwenye jamii.
Salamu
Salamu ipo ya namna nyingi kutegemea na muda na watu. Iwe shikamoo, habari, salam alaykum, Vipi, za saizi, mambo nk; ilimradi tu usinyamazie watu. Wajulie watu hali zao kwa kutoa salamu kila panapobidi. Jitahidi sana kusalimia (kuamkia) watu
Naomba
Neno hili nadhani sote tumepitia kuitwa watoto na tumekumbana nalo sana kwa miktadha tofauti
Hodi
Tumia neno au maneno yoyote ilimradi tu uoneshe kuomba ridhaa ya kuruhusiwa kuwa miongoni mwa waliopo kwa muda huo
Kuaga
Kwaheri, baibai, nakwenda, naondoka, nilikwepo, tutaonana nk ni vijineno vyenye maana sana maishani. Kuaga ni kutoa taarifa ya kujitoa katika waliopo kwa muda huo
Karibu
Neno karibu (tena) ni neno la kiungwana sana
Unapokuwa bado hujafa jitahidi kuyatumia mara kwa mara maneno hayo ila... zingatia tu kuwa si kila sehemu (muktadha) utalazimika kuyatumia!