Haya ni manukato/perfume gani?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Habari wakuu

Siku chache zilizopita nilitembelewa na mgeni nyumbani. Alikuwa amejipulizia manukato/perfume ambayo harufu yake imebaki kwa wiki nzima sasa kwenye sofa aliyokuwa amekaa.

Kwa wajuzi wa manukato naomba kujua ni brand gani za perfume zinaweza kudumu muda mrefu kiasi hiki. Mimi ni mpenzi wa perfume lakini nyingi ninazotumia ikikaa sana kwenye nguo labda ni masaa 24.
 
Hizo huuzwa kuanzia laki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikuwa ni ugeni wa kikazi tu na mmojawapo ndiyo huyo na sina mawasiliano nae
Kuna perfume nyingi bro. Nashauri kama haujaingia kwenye upenzi wa. Perfume anza mdogo mdogo.

Anza na Body Spray za be ndogo, kisha upande taratibu.

Kuna Uzi wa perfume humu, jukwaa la Mabishoo na madada duu, kuna perfume bei ghali unapata kodi ya miezi 6 Gomz.

Nashauri anza slow.
 
Natumia perfumes tangu utoto wangu mkuu sijaanza jana. Thanks nitaangalia huo uzi ulioutaja.
 
Ila pia mkuu inaonekana hapo kwako sofa hazisafishwi mara kwa mara......?
Maana harufu kubaki wiki kwenye kitambaa cha sofa ni kuwa husafishi au uliipenda hio perfume harufu yake ndio maana unaiulizia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…