Haya ni maradhi au ni nini?

Haya ni maradhi au ni nini?

Mashaxizo

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2013
Posts
6,707
Reaction score
3,346
Habari za hapa.

Ilianza taratibu tumbo kujaa upepo na kutokua na amani kiasi cha kukosa hamu ya kula. hali hiyo ilijitokeza kwa siku ambazo nimekula viazi vitamu (chai ya asubuhi) kwa kawaida nakunywa chai za kimjini mjini (mikate na chai ya rangi, siku zengine supu na siku chache maharage)

Siku zilisonga na niliacha kula viazi vitamu. but hali iyo iyo ilijitokeza tena pale nikipiga mihogo (ya kuchemsha asubuhi) Mmmh! tofauti ya ujaaji wa upepo ilikuepo kiasi kwamba katumbo hujaa upepo mwingi pindi nikila viazi vitamu.

kinachojitokeza kwa vyote ni ile hali ya kuhisi uchungu uchungu baada ya mda kwa siku ambayo nimekula either mihogo or viazi vitamu.

Hapo nilijua Mungu hapendi nile hivyo vyakula huku nikijisemea haya ni maradhi ya kitajiri! Nilijua nilitakiwa nipige tu maziwa na vinyama nyama huku nikijilia samaki.

KILICHONILETA HAPA LEO:

Ni kwamba hali ya kitumbo kujaa upepo imejitokeza leo kisa jana nilipiga kiepe yai, khaa! Si mpenda sana hiko kilaji ila at least kwa wiki najigongea mara moja.

Leo mzima sina raha! katumbo kamejaa upepo na nakumbuka kuna mda nilijamba chumbani. (hutakiwi kucheka hamna asie jamba) khaa mbona nilitoka bila kupenda.

Jee hayo ni maradhi?

Kwanini wengine huwa kawaida tu kama mimi ilivyokua mwanzo? nini kinafanya wengine iwe kawaida ila kwangu iwe tatizo?

Tiba yake ni nini?

Sipendi kujiekea miko wadau.

Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom