Najiuliza:
1) Kwanini viongozi wetu walichagua kukaa kimya au kupuuza sauti za Watanzania pale Watanzania walipodai haki kwa amani?
2) Kwanini walichagua kuzungumza kwa vitisho na ukali kwa raia ambao walijaribu kupaza sauti kudai usalama wa maisha yao na mali zao?
3) Kwanini waliahidi kutusikiliza na kututumikia lakini walitugeuka na kuwa mabwana zetu wanaojali tu wanavyojisikia wao na si tunavyojisikia sisi tuliowachagua? Kuna kiongozi alifikia kuwambia watanzania eti wahamie Burundi!
4) Ilikuwaje wakajiaminisha kwamba Watanzania walio kimya (hasa wa vijijini ambao au hawasemi ama sauti zao hazisikiki ama hawajui kama wana cha kusema) wapo upande wao na wale wanaosema ni maadui zao?
5) Kwanini mpaka sasa wakati Watanzania kutoka katika mikoa mingi ya nchi wameamua kutumia njia nyingine kupaaza sauti zao, sauti za wenye mamlaka, kama zikitolewa, bado ni za kutishia na kukatisha tamaa?
6) Kwanini katika nchi hii, usiporidhika na unachotendewa na Serikali yako, ukaamua kusema kutoridhika kwako, unaitwa mhuni na unatishiwa kushughulikiwa?
Nani ametufikisha hapa kama Taifa?