Haya ni matumizi mabaya ya ndumba

Haya ni matumizi mabaya ya ndumba

Kendrick Rama

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2019
Posts
409
Reaction score
456
Habari zenu wakuu,

Leo nimepatwa na kali ya kufungia mwaka. Ilikuwa majira ya saa 8 hivi mchana baada ya vimvua vya hapa na pale huku nikiwa kwenye kaduka kangu cha vifaa vya umeme maeneo ya Tabata Dar es salaam ghafla alitokea bwana mmoja akiwa na boda boda aina ya Boxer akidai yeye ni mteja na anahitaji main switch ya njia sita.

Kwa bahati mbaya ziliniishia ikabaki moja ya njia nne akasema hiyo hiyo anachukua na ndipo alinipa karatasi yake iliyojaa vifaa vingine kama earth rod, bomba, switch nk.

Nikawa namuangalizia hivyo vifaa na kusoma kwa umakini ile karatasi yake, sasa wakati naanza kumpigia hesabu akasema anaenda Tigo Pesa kutoa huo mkwanja kama laki tatu hivi na ushee.

Baada ya hapo sikumuona tena na nilimsubiri kwa muda hakutokea na ndipo niliachana naye na kuendelea na mishe nyingine.

Mshangao! baada ya masaa kama matatu hivi ndipo alikuja rafiki yangu naye pia ana hisa zake kwenye hii biashara na kugundua kwamba kuna bunda mbili za waya hazipo (2.5mm twin na 1.5mm single) zenye thamani ya laki mbili na arobaini.

Baada ya uchunguzi ndipo niligundua nimeibiwa lakini nahisi sio njia ya kawaida kwani kwa haraka mtu kubeba nyaya mbili za aina moja na roller nzima si rahisi kwani zilikuwa ndani na huwa naingia mwenyewe tu.

Pia kwa uzoefu wangu wa kazi hii huwa tunaibiwaga taa tu lakini leo ndumba limehusika wazi na yule mwizi.

Sasa hivi na mwanangu tumenuniana hapa 😅 lawama zote kwangu.
 
Pole mkuuu, Naona tayari Xmas imeanza kuchacha kwa upande wako. Kwa ufupi kadri tunavyokaribia msimu wa Sikukuu za Mwisho wa mwaka na Maandalizi ya Ada za Januari tuongeze Umakini sana lkn pia tujipange kuuumizwa sio kwa Wizi, Polisi wa Usalama barabarani kwa sasa ni kama Simba Porini, Utapeli uko full gear, Simu za ndugu kupiga Virungu usipime yaaani ni Vurugu mtindo mmoja.
 
shukrani ndugu ila nikikuta mwizi sehemu yoyote kichwa chake halali yangu
 
Haha wala ndumba haijahusika hapo mkuu. You just concentrated on gathering his needs, there the chance he got.
So next time kuwa makini tu
 
Haha wala ndumba haijahusika hapo mkuu. You just concentrated on gathering his needs, there the chance he got.
So next time kuwa makini tu
cha ajabu wakati anaondoka namuona hajabeba chochote... hapo ndipo nilipochoka kabisa kwani ilichukua kama nusu saa kuamini kama kweli nimeibiwa
 
Mkuu hapo sio ndumba hapo hapo alicheza na timing tu.
 
Pole, hapo dukani alikuja pekeyake Ila alikuwa na wenzake pembeni ambao walinyata kuja dukani kubeba hizo waya wakati wewe unahangaika nae kumuuzia bidhaa anazotaka.

Kama kuna watu nje ya duka watakuwa waliona.
 
alikuja peke yake na usafiri wake ambao ni pikipiki aina ya boxer
 
alikuja peke yake na usafiri wake ambao ni pikipiki aina ya boxer

No kuwa hao wenzako hukuwaona maana hawaji dukani hadi unapokuwa busy nae umeinama kitendo na hatua nyavu hakuna.

Hakuna ndumba hapo umeibiwa mchana kweupeee.
 
No kuwa hao wenzako hukuwaona maana hawaji dukani hadi unapokuwa busy nae umeinama kitendo na hatua nyavu hakuna.

Hakuna ndumba hapo umeibiwa mchana kweupeee.
hizi flem zetu zipo pembezoni mwa barabara mtu unaanza kumuona tangu anapotoka na kwa nje kuna jirani zangu wanachomea. ila kama ajatumia ndumba basi atakuwa ni professional wa wizi
 
Back
Top Bottom