Kendrick Rama
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 409
- 456
Habari zenu wakuu,
Leo nimepatwa na kali ya kufungia mwaka. Ilikuwa majira ya saa 8 hivi mchana baada ya vimvua vya hapa na pale huku nikiwa kwenye kaduka kangu cha vifaa vya umeme maeneo ya Tabata Dar es salaam ghafla alitokea bwana mmoja akiwa na boda boda aina ya Boxer akidai yeye ni mteja na anahitaji main switch ya njia sita.
Kwa bahati mbaya ziliniishia ikabaki moja ya njia nne akasema hiyo hiyo anachukua na ndipo alinipa karatasi yake iliyojaa vifaa vingine kama earth rod, bomba, switch nk.
Nikawa namuangalizia hivyo vifaa na kusoma kwa umakini ile karatasi yake, sasa wakati naanza kumpigia hesabu akasema anaenda Tigo Pesa kutoa huo mkwanja kama laki tatu hivi na ushee.
Baada ya hapo sikumuona tena na nilimsubiri kwa muda hakutokea na ndipo niliachana naye na kuendelea na mishe nyingine.
Mshangao! baada ya masaa kama matatu hivi ndipo alikuja rafiki yangu naye pia ana hisa zake kwenye hii biashara na kugundua kwamba kuna bunda mbili za waya hazipo (2.5mm twin na 1.5mm single) zenye thamani ya laki mbili na arobaini.
Baada ya uchunguzi ndipo niligundua nimeibiwa lakini nahisi sio njia ya kawaida kwani kwa haraka mtu kubeba nyaya mbili za aina moja na roller nzima si rahisi kwani zilikuwa ndani na huwa naingia mwenyewe tu.
Pia kwa uzoefu wangu wa kazi hii huwa tunaibiwaga taa tu lakini leo ndumba limehusika wazi na yule mwizi.
Sasa hivi na mwanangu tumenuniana hapa 😅 lawama zote kwangu.