"Ni Matunda ya filamu ya royal tour ndani ya Miezi miwili pekee tu! Watalii wafurika Tanzania".
Ikiwa ni baada ya Miezi miwili tu tangu filamu maalumu ya royal tour iliyomuhusisha rais was jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kutambulishwa rasimi nchini marekani na baadae Tanzania matalii waanza kumiminika kuja Tanzania.
Filamu hiyo iliyolenga kuendeleza na kustawisha sekta ya utalii Tanzania kwa kuonesha vivutio mbalimbali vya utalii Tanzanian bara na visiwani imeonesha kuzaa matunda mara tu baada ya miezi miwili kutoka ambapo watalii wengi wameweza kuja na kuongezeka mara dufu kutokana na filamu hiyo.
Kutokana na filamu hiyo wadau mbalimbali katika sekta ya utalii nchini wameoneshwa kufurahishwa na kuguswa na filamu hiyo kwa ongezeko la watalii nchini.
Ndani ya miezi hii miwili Tanzania Kupitia Royal Tour, tumeshuhudia ndege kubwa ya #eurowings ikileta watalii zaidi ya 300 na kuongeza safari zake kuwa itafanya huvyo mara mbili kwa wiki pale kiwanja cha ndege cha kimataifa cha KIA. .
Vile vile tumeshuhudia wachezaji maarufu wa timu kubwa duniani wakidhuru Tanzania. Ambao ni
1. Ander Herrera - PSG (France)
2. Jesus Vallejo - R. Madrid (Spain)
3. Mauro Icard - PSG (France)
Hakika mama hapo aliupiga mwingi
#MamaYukoKazini #MamaYukoKazini