Haya sasa Wacha niwafundishe chap jinsi ya kuimarisha na kupandisha " Nyota" za watoto WENU kuanzia wakiwa wadogo

Haya sasa Wacha niwafundishe chap jinsi ya kuimarisha na kupandisha " Nyota" za watoto WENU kuanzia wakiwa wadogo

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Ukienda kwenye vilinge vya waganga wa kienyeji, vibaraza vya maostaz, na makanisa ya mitume na manabii utakutana na idadi kubwa sana ya watanzania wanaenda kusafisha, kupandisha, kufufua, kufungua nyota zao etc, whichever come first .

Ukichunguza vizuri nini kimewafanya waone kwamba " nyota" zao zimeharibika, jibu utakalo pewa ni " kukosa vipato vya uhakika, biashara kufa, kufukuzwa kazi, kukimbiwa na mke etc"

( Haya yote yanahusiana na kutokuwa na hela)

Kumbe basi watu Hawa wangekuwa na hela au na akili ya kutengeneza constant money wasingeweza kuwaza kuhusu nyota zao kuharibiwa..

Sasa Wacha nikufundishe jinsi ya kuimarisha,kupandisha na kulinda nyota za watoto wako.

NYOTA NI NINI?

Kwa definition yangu, nyota ni akili inayo fanya kazi sawa sawa

Kama akili yako inafanya kazi sawa sawa basi hata " nyota " yako itakuwa sawa kwa sababu mambo yako yote muhimu yatakuendea vizuri kwa vile utakuwa unatumia akili yako vizuri..

Kama utatumia akili yako vizuri, basi hakuna uganga wala uchawi utakuwa juu yako.

Unatakiwa kujua kwamba, akili ya mwanadamu ina nguvu kushinda uchawi wa aina yoyote ile unao ujua na usio ujua.

Hata Yesu alipo waambia wanafunzi wake, " Kama mtakuwa na Imani walau punje ya haradali basi mtaweza kuhamisha milima" alimaanisha matumizi sahihi ya akili, kwamba endapo mwanadamu atatumia walau robo ya akili yake vizuri basi hakuna tatizo litamshinda juu ya uso wa dunia.

Hata wanasayansi wanasema haya maendeleo ya teknolojia ambayo mwanadamu ame weza kuya achieve juu ya uso wa dunia ni matokea ya matumizi ya chini ya asilimia 5 ya uwezo wa akili ya mwanadamu.

Narudia tena kwa mara nyingine, akili yako wewe mwanadamu ina nguvu kushinda uchawi wa aina yoyote ile.

Kama kuna majambazi wawili wanaishi let's say wilaya ya Temeke halafu wewe na mwenzako mkapewa task ya kuwaua, kwa ahadi ya malipo ya dola milioni moja Kila mmoja plus scholarship kusoma Ulaya miaka mitatu, wewe ukaenda kwa mganga ( kwa wachawi) halafu mwenzako akatumia akili yake basi mwenzako atapata matokeo ya haraka na uhakika zaidi kushinda wewe.

Kwa sababu wakati wewe una hangaika kwenye vilinge vya wachawi mwenzako ataenda kumpiga jambazi wake mkwassa and he will die. Atarejea baada ya miaka minne na kukukuta bado unazunguka kwenye vilinge vya waganga.

Yeye ametumia akili yenye nguvu wewe umetumia uchawi. Yeye kampiga mkwassa huyo jambazi, wewe upo chumbani kwako unachoma dawa ukitaja jina la jambazi kwa kumwambia " Kufa! Kufa ! Kufa!


JINSI YA KUPANDISHA NYOTA ZA WATOTO WENU...

1. Hakikisha mtoto wako anakula vyakula vinavyo imarisha utendaji kazi wa ubongo. Viwe vyakula vyake vikuu.

2. Hakikisha unamwambia mtoto wako kuanzia akiwa mdogo kwamba hakuna uganga wala uchawi wenye nguvu kushinda akili ya mwanadamu.

Wazo hili liki stick in his subconscious hatogusa kilinge cha mganga wala mchawi maisha yake yote.

3. Invest kwenye vitabu vinavyo toa maarifa ya jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kutumia akili yake mwenyewe.


4. Mfundishe mtoto wako kuiamini na kuitegemea akili yake. Mtengeneze aiamini na kuitegemea nguvu ya akili yake kwa kiwango kile kile ambacho una muamini Mungu.

Wakataze watoto wako kusema " kwa akili zetu pekee hatutoweza".

Na badala yake waseme " kwa akili alizo tupa Mungu tutaweza".
 
Mkuu shule bila ada haingii kichwani na cha bure hakina thamani.. Obviously umetoa shule kubwa sana kiwango cha shahada kwa lugha ya chekechea.. Ungetoza ada kidogo..
 
Mkuu shule bila ada haingii kichwani na cha bure hakina thamani.. Obviously umetoa shule kubwa sana kiwango cha shahada kwa lugha ya chekechea.. Ungetoza ada kidogo..
🙏🙏🙏🙏
 
Mkuu shule bila ada haingii kichwani na cha bure hakina thamani.. Obviously umetoa shule kubwa sana kiwango cha shahada kwa lugha ya chekechea.. Ungetoza ada kidogo..
All the best thing in this world are free. Hata kwenye ni bible imeandikwa " Bwana ametoa uzima tele Kila atakae atapata bure"
 
Back
Top Bottom