Haya TEC wameshakuja na Tamko leo Jema, je, na Sisi wana JamiiForums Tamko letu litatoka Saa ngapi?

Haya TEC wameshakuja na Tamko leo Jema, je, na Sisi wana JamiiForums Tamko letu litatoka Saa ngapi?

Humu JF kuna makundi matatu kuhusu mkataba wa DPW, na yapo kama ifuatavyo;

1. Wanaunga mkono mtaba wa DPW kama uliovyo sasa
2. Wanaopinga mkataba huo
3. Wapo wa I dont care

Sasa, ili kuweka mzani sawa, kila kundi litoe tamko lake, halafu makundi mengine yaweke hoja mezani kwanini wanapinga hoja za makundi mengine..!!

Hii itakuwa tofauti na ilivyo mtaani kwa sasa, wanaopinga wameweka hoja kwa vipengele vibaya vilivyopo kwenye mkataba, LAKINI WANAUONGA MKONO WAO HAWAJADILI VIPENGELE VYA MKATABA, ILA WANANGÁNGÁNA TU KUSEMA WANAOPINGA WANAFANYA HIVYO KWA SABABU RAIS NI MWANAMKE, KWA SABABU RAIS NI MZANZIBARI, KWA SABABU RAIS NI MUISLAMU. ETC.. Binafsi nawaona hawana hoja ila wanajaribu kupindisha mjadala, utoke kwenye kujadili vipengele vyake na uingie kwa kujadili dini za watu, watu hao wanatoka wapi kati ya bara na visiwani na watu hao wana jinsia gani.
Naunga mkono hoja
 
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, mimi ni mtoto wa Mungu naishi kwa kufuata sauti ya mungu. tamko lisiende mbali, Kibaraza cha urisi hakipangishwi nasisi tunashida ya kukitumia kujikwamua kiuchumi kwanza kipo barabarani lazima tukitumie kujiajiri sisi kabla ya wageni kujiajiri kupitia kibaraza chetu.
 
Tunataka dp world waje hii nchi sio ya wakatoliki,wakatoliki hawana uwezo wa kutuamulia watanzania milioni 60 hii nchi tupo mabudha na wasio na dini pia tunaitaka dp world na tunaimani na serikali yetu inayoongozwa na rais samia muislam,dr mpango mkatoliki,pm majaliwa muislam na tulia akson mkatoliki.
 
Iwekwe poll tupige kura

1. mkataba ufutiliwe mbali
2. Mkataba urekebishwe
3. Mkataba uachwe kama ulivyo
What a Golden advice. Naomba Uongozi wa JamiiForums utusaidie kwa hili hasa kwa kufuata haya Maelekezo yako ya Upigaji Kura Wetu kama JamiiForums Members.

Cc: JamiiForums Founder Maxence Melo
 
Ninaungana na TEC 100% kwa Tamko.

Sasa ole wenu Tamko lenu lije tofauti na nilivyoanza Mimi mtajua kwanini Wimbo wa Taifa huwa hauna Kolabo na Nyoka hana Ugoko ( I'm Kidding guys )

Tafadhali naomba Wachaguliwe Members kadhaa na kwa Niaba yetu waje na Tamko la Jumla la wana JamiiForums wote juu ya Sakata zima la Kukataa Ubinafsishwaji wa Bandari yetu kwa DP World.

Nikija ( Log In ) hapa baadae Saa 4 na Nusu Asubuhi naomba nilikute hilo Tamko letu sawa?
Tamko la JF members liko kwenye 'signature collection petition' fuatilia mpaka mchana huu wanaokubali mktaba ni asilimia 16% wakati wanaokataa mkataba ni asimilia 83% huku asilimia 1% hawaeleweki wako wapi!!!
 
Tafadhali naomba Wachaguliwe Members kadhaa na kwa Niaba yetu waje na Tamko la Jumla la wana JamiiForums wote juu ya Sakata zima la Kukataa Ubinafsishwaji wa Bandari yetu kwa DP World.

Nikija ( Log In ) hapa baadae Saa 4 na Nusu Asubuhi naomba nilikute hilo Tamko letu sawa?
katika hilo jopo Faizafox asikosekane.,
 
Back
Top Bottom