Haya tena makubwa Msaada!

Haya tena makubwa Msaada!

Shut up and live with it . ila dogo akijifungua usiache kwenda kumpa kampani shemeji.
 
Naomba ushauri wenu
Maswali yote yatajibiwa..?
Miaka 10 iliyopita niliwahi kuwa katika mahusiano ya mapenzi na kaka X nikiwa school
Baada ya shule tukapoteana yeye alienda nje na sisi kama family tukahama mkoa na kwenda sehemu nyingine na mawasiliano yakakatika..
Nina wadogo zangu pia wa kike shuleni mie pekee nilitumia jina la Babu yaani Condoreza ..M
Wadogo zangu wote wakatumia jina la baba yana N..E Na sasa nimeolewa na nina familia yangu naishi kwa Amani na upendo
Mdogo wangu kapata mpenzi kama kawaida mapenzi ya kileo nahisi anaka ujauzito…
Sasa wamefikia hatua ya kutaka kuoana mdogo wangu na mchumba wamefunga safari kumleta mchumba
kwanza kututambulisha sisi masisters na baadhi ya ndugu ili hatua zingine ziendelee
Na mahusiano yao sio ya muda mrefu sana..
Jumamos naitwa kutambulishwa Shemeji nakuta ni X wangu ..roho imekaribia kupasuka kwa mshituko
Moyo umekufa ganzi naona na yeye kabakia na mshangao..
Tufanyeje juu ya hili?
Sijasema lolote mpaka sasa..
:A S cry:
Bado hujasema kitu? Na wakati umeshasema mpaka umeandika....! Lakini kabla mie sijatoa nasaha zangu, ni vema nikakuhoji wewe kwanza....!
  1. Je, mahusiano yako na X yalipata kujulikana ndani ya jamii?
  2. Je, wewe binafsi unajisikia kumrudia Ex- wako? Au huko ulipo umekwisha fika?
  3. Unaonaje feelings zake juu yako, bado anakuhitaji?
 
Kama imeshafikia hatua kuwa ana ujauzito hauwezi ukareverse hiyo kitu. Pata muda wa kuongea na huyo X wako na kujua mawazo yake baada ya kushauriana inabidi mumface mdogo wako na kumueleza ukweli. Ukweli utawaweka huru though its awkward lakini mtazoea
Hapana ushauri wako ni mbaya cha kufanya wabaki kimya kimya tu, na kila mtu aendelee na maisha yake, lakini wasije wakarudia kamchezo kale walicho kacheza siku za nyuma.
 
Huyo alikuwa X wako na siyo mumeo, na bahati mbaya zaidi mdogo wako sasa ni mjamzito, huna ujanja acha ndoa ifungwe. Hiyo siri itabaki kuwa yenu wawili.

Angalizo: Msije kukumbushie enzi, mkikamatwa taleta tafrani ya aina yake na kuvunja ndoa zenu!
 
Bado hujasema kitu? Na wakati umeshasema mpaka umeandika....! Lakini kabla mie sijatoa nasaha zangu, ni vema nikakuhoji wewe kwanza....!
  1. Je, mahusiano yako na X yalipata kujulikana ndani ya jamii?
  2. Je, wewe binafsi unajisikia kumrudia Ex- wako? Au huko ulipo umekwisha fika?
  3. Unaonaje feelings zake juu yako, bado anakuhitaji?

1. Kwa sababu ilikuwa shuleni baadhi ya marafiki wachache walikuwa wanajua ingawa kwa sasa sijui wako wapi hao watu kila mtu ana maisha yake .
2.Kwa sababu nina mme na ninampenda na huyo X tangu tumeachana hakuwahi kuingia akilini mwangu mpaka nilipomuona juzi na mdogo wangu nikabaki nashangaa tu.
3.Siwezi jua feelings zake kwangu kwani sijakaa nae nikiwa mimi kama mimi na hiyo siku tulikaa wengi tunaongea mambo mbali mbali ya maisha na mengineyo
So siwezi jua ila mie sina feeling zozote kumbuka ni miaka kumi iliyopita.
 
Kama imeshafikia hatua kuwa ana ujauzito hauwezi ukareverse hiyo kitu. Pata muda wa kuongea na huyo X wako na kujua mawazo yake baada ya kushauriana inabidi mumface mdogo wako na kumueleza ukweli. Ukweli utawaweka huru though its awkward lakini mtazoea

Hapo ndipo unapowatafutia balaa..
Itakuwa dadamtu akimtembelea mdogo wake..mdogomtu roho pah!
They the two should settle the matter to rest..no third party!
 
hapo lazima mkumbushie enzi zenu. Wanaume hatuonjagi mara moja!
Yawezeka wewe huna feelings zozote, lkn yeye je naye hana?
 
Dah!Hv Zile Za Kwenye Muvi Kumbe Uhalisia Unakuwepo!?
Kwanza Pole Sana Dadangu Kwa Hayo Yalokusibu.
Katika Hulka Ya Binadamu Naamini Kwamba anapoguswa Na Jambo Fulani Basi Lazima Kujari Kumetangulia,
Hapa Namaanisha wewe Suala La Kuduu Miaka Miwili Iliyopita Linauzito Gani, Iliari Nawe Umeolewa?
Sababu Inavyoonesha Hapo Suala Linalokupa Kiwewe Ni Kuduu Nae.

Unanifanya Niwe Na Shaka Laiti Kama Huyo Angekuwa mdogo/ndugu Wa Mumeo Na Akakaribia Hapo Nyumbani Angalau Kwa Wiki,basi Uzalendo Ungekushinda Na Ungeihitaji Ari Ya Zamani Irudi Kati Yenu
Hebu Achana Na Mambo Ya Zamani Na Wala Husitake Kuitia Doa Ndoa Ya Mdogo Wako,We Kubali Kwamba Huyo Ni Mume Wa Mdogo Wako Na Wewe Ni Shemejie.
Yale Yote Yamepita Wala Hayawezi Kubadirisha Kilichopo Sasa!.
 
muache mdogo wako afunge ndoa na huyo x wako,na hiyo ibaki km siri yenu wewe na huyo x,sioni umuhimu wowote wa kuweka yaliyopita wazi.pili km unaipenda ndoa yako na mdogo usikubali kukutana na uyo x sehemu hatarishi.
 
Dah pole,bt sioni kama kuna k2 cha kumzuia huyo mdogo ako kuendelea na huyo jamaa,it is past with u!make t past in a really sense,
 
Da i can imagine the situation,mimi siku zote naamini kweli inamuweka mtu huru kama ingekuwa mimi wewe sincerely ningemuita mdogo nimueleze kwa upendo na ushawishi kwamba ilikuwa past, nimeona sfaff mwenzangu kamuoa mdogo wa X wake though to me nisingethubutu ningezaa mtoto niendelee na maisha kuliko kuishi na mume, x wa sister
 
Huyo X wako mlisha fanya naye sex ?

Kama hujafanya naye sex sidhani kama shida.

Ndo mana vitabu vya dini vilikataza kufanya sex kabla ya ndo, hayo ndoa madhara yake, pole sana.

Inaonekana X yuko faster,si umesikia mdogo mtu ana ujauzito tayari?
 
better ukae 2 kimya ma dia coz ukisema utaharibu kila kitu na dogo teyar ana ujauzito,,,,,,,uconyeshe signs zozote za kufahamiana na huyo x shemeji.
 
Hii Ngumu tukirudi kwenye imani ya kidini ukweli unakuweka free
Ni ngumu sana kukaa na siri kama hii moyoni...
 
Some secrets are better kept as secrets.
Kitu kama hii ilishatokea kwa kaka zangu wawili na wifi mmoja. Kwa vile harm imeshatokea pregnancy na uchumba; bora ukae na siri yako na bahati nzuri wewe ni mkubwa, kwa mila nyingi za kitanzania shemeji mkubwa (wa kike) ni kama mkwe so hakuna utani mwingi.
 
Back
Top Bottom