GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Ajali imeshatokea tayari na wengine wameshatuaga mazima duniani huku wengine wakiwa wamejeruhiwa na tunaendelea kuwa nao Hai hapa duniani.
Hongereni pia Watanzania kwa Kumsifia zaidi Muokoaji Majaliwa na Kumpa Zawadi nyingi huku Ushujaa wake ukitulazimisha tumjadili zaidi Yeye Mitandaoni kote, katika Vyombo vya Habari na Mitaani ( hasa Vilingeni ) ambako wengine ndiyo sehemu zetu za Kujidai huku tukicheza Karata, Bao na Draft.
Hivyo basi naomba kuanzia Leo Watanzania wote, Waandishi wa Habari, Vyombo vyao, Bloggers na Wamiliki wa Wovuti Agenda yetu Kuu iwe ni Suala la Mabadiliko ya Hali ya Hewa ( Climate Change ), Njaa Kubwa iliyoko sasa katika sehemu mbalimbali za nchi yetu, Uchumi mbaya na hali mbaya ya Maisha ( Ugumu wa Maisha ) ulioko sasa nchini Tanzania na kwa Watanzania.
Naomba nguvu hii hii tuliyoitumia Kushadadia Ajali ya Ndege huko kwa Watani zangu Wahaya Kagera ( Bukoba ) na hasa hasa Kumshadadia Muokoaji Majaliwa basi tuitumie pia katika Kuzungumzia Janga Kubwa lililoko la Njaa, Ukame, Umasikini na Uchumi mbaya kuliko wengi wenu mnavyojua au mnavyodhani.
Naomba kila mwana JamiiForums kuanzia sasa apaze Sauti juu ya Climate Change na popote alipo ahimize Utunzaji wa Mazingira ili Ukame upungue, mvua zianze Kunyesha ili hali isiendelee kuwa mbaya na wapaze Sauti zao popote walipo kwa Watanzania kutokuuza Vyakula vyao Nje ya Nchi kwani wenye Maono tumeshaona kuwa kunaenda kuwa na Janga Kubwa la Njaa, Magonjwa na Watanzania ( wana JamiiForums wengi ) Kufariki kwani Njaa huwa haiangalii Wewe ni Great Thinker au Komando.
Kwa mtakaonielewa mbarikiwe mno.