Haya tumeshamaliza ya 'Ajali ya Ndege' na 'Kumshadadia Muokoaji' Majaliwa, sasa turudini huku kwenye 'Umuhimu' zaidi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ajali imeshatokea tayari na wengine wameshatuaga mazima duniani huku wengine wakiwa wamejeruhiwa na tunaendelea kuwa nao Hai hapa duniani.

Hongereni pia Watanzania kwa Kumsifia zaidi Muokoaji Majaliwa na Kumpa Zawadi nyingi huku Ushujaa wake ukitulazimisha tumjadili zaidi Yeye Mitandaoni kote, katika Vyombo vya Habari na Mitaani ( hasa Vilingeni ) ambako wengine ndiyo sehemu zetu za Kujidai huku tukicheza Karata, Bao na Draft.

Hivyo basi naomba kuanzia Leo Watanzania wote, Waandishi wa Habari, Vyombo vyao, Bloggers na Wamiliki wa Wovuti Agenda yetu Kuu iwe ni Suala la Mabadiliko ya Hali ya Hewa ( Climate Change ), Njaa Kubwa iliyoko sasa katika sehemu mbalimbali za nchi yetu, Uchumi mbaya na hali mbaya ya Maisha ( Ugumu wa Maisha ) ulioko sasa nchini Tanzania na kwa Watanzania.

Naomba nguvu hii hii tuliyoitumia Kushadadia Ajali ya Ndege huko kwa Watani zangu Wahaya Kagera ( Bukoba ) na hasa hasa Kumshadadia Muokoaji Majaliwa basi tuitumie pia katika Kuzungumzia Janga Kubwa lililoko la Njaa, Ukame, Umasikini na Uchumi mbaya kuliko wengi wenu mnavyojua au mnavyodhani.

Naomba kila mwana JamiiForums kuanzia sasa apaze Sauti juu ya Climate Change na popote alipo ahimize Utunzaji wa Mazingira ili Ukame upungue, mvua zianze Kunyesha ili hali isiendelee kuwa mbaya na wapaze Sauti zao popote walipo kwa Watanzania kutokuuza Vyakula vyao Nje ya Nchi kwani wenye Maono tumeshaona kuwa kunaenda kuwa na Janga Kubwa la Njaa, Magonjwa na Watanzania ( wana JamiiForums wengi ) Kufariki kwani Njaa huwa haiangalii Wewe ni Great Thinker au Komando.

Kwa mtakaonielewa mbarikiwe mno.
 
Yah suala la climate change ni suala la kuongelewa ila unajua kwanini kuna baadhi ya case pale U.S.A zinatatiliwa mpaka leo hii na zilitokea miaka 50 au 30 iliyopita huko nyuma
 
Hali ya ukame ni mbaya na inatisha, wakulima kwa wafugaji kote wanalalamika hali mbaya.

Ila sisi watanzania kama hujatujua tunapenda vitu vinavyotrend, sasa climate change haitrend hivyo huwezi ona tunatumia nguvu kubwa kujadili.
 
Kwahiyo nikisema tuna Jamii ya Kipumbavu ( Hovyo Hovyo ) nchini nitakuwa nakosea Mkuu?
 
Mkuu Genta kwa watanzania tulionao sasahivi hawana habarfi na kuhangaika na masuala ya maana kama hayo uliogusia Climate change, economy , etc etc akili zilizoko sasahivi ni uchawa tu unlimited watu wameenda likizo ya kufikiri, hakuna tena wanaowaza critically tumekuwa watu wa matukio tuuuu ndio maana hata issues za analysis na reasoning hazipati mashiko katika mijadala mbalimbali, kuna tatizo mahala.

Mungu atusaidie tu kwasababu kama zama za kina nyerere vijana ndio waliokua wana determine future ya kila jambo angalia vijana wa sasa hivi hawa wavaa hereni ni watoga pua , unadhani kuna future ya maana hapa Genta? wamejengwa kuwa wa kupokea na sio kutoa, you can not give what you dont have.
 
Hujakosea kabisa, angalia vitu vinavyotrend mitandaoni ndio utajua tuko na jamii ya aina gani.
Ndiyo maana kutokana na Upumbavu huo kuna muda huwa naona hata Aibu Kujinasibu ( Kujitaja ) kuwa Mimi ni Mtanzania kwani najiona kabisa kuwa sina IQ ya Kitanzania bali nina IQ ya Kiyahudi na Kitutsi tupu ambazo kwa 100% ni za Watu very Intelligent duniani.
 
Mkuu Genta kwa watanzania tulionao sasahivi hawana habarfi na kuhangaika na masuala ya maana kama hayo uliogusia Climate change, economy , etc etc akili zilizoko sasahivi ni uchawa tu unlimited watu wameenda likizo ya kufikiri, hakuna tena wanaowaza critically tumekuwa watu wa matukio tuuuu ndio maana hata issues za analysis na reasoning hazipati mashiko katika mijadala mbalimbali, kuna tatizo mahala. Mungu atusaidie tu kwasababu kama zama za kina nyerere vijana ndio waliokua wana determine future ya kila jambo angalia vijana wa sasa hivi hawa wavaa hereni ni watoga pua , unadhani kuna future ya maana hapa Genta? wamejengwa kuwa wa kupokea na sio kutoa, you can not give what you dont have.
Post yako hii ni nzuri sana Mkuu na nakubaliana nayo kwa 100% na kwa ulivyoandika tu hivi sina shaka na IQ yako kuwa ni Kubwa na Nzuri mno kama ya Wayahudi na Watutsi. Heko...!!!!!!
 
Tutumie pia hili janga la ukame na utayari wa serkali kwa ajili ya kile kinakuja isiwe tu mambo yenye mihemko ambayo yanatumika kama Political platform.
Vyama vya siasa vijenge hoja juu ya njaa inayokuja kwa taifa tena iwe kwa HASHTAG nyingi
 
Ajali imeshatokea tayari na wengine wameshatuaga mazima duniani huku wengine wakiwa wamejeruhiwa na tunaendelea kuwa nao Hai hapa duniani.

Hongereni pia Watanzania kwa Kumsifia zaidi Muokoaji Majaliwa na Kumpa Zawadi nyingi huku Ushujaa wake ukitulazimisha tumjadili zaidi Yeye Mitandaoni kote, katika Vyombo vya Habari na Mitaani ( hasa Vilingeni ) ambako wengine ndiyo sehemu zetu za Kujidai huku tukicheza Karata, Bao na Draft.

Hivyo basi naomba kuanzia Leo Watanzania wote, Waandishi wa Habari, Vyombo vyao, Bloggers na Wamiliki wa Wovuti Agenda yetu Kuu iwe ni Suala la Mabadiliko ya Hali ya Hewa ( Climate Change ), Njaa Kubwa iliyoko sasa katika sehemu mbalimbali za nchi yetu, Uchumi mbaya na hali mbaya ya Maisha ( Ugumu wa Maisha ) ulioko sasa nchini Tanzania na kwa Watanzania.

Naomba nguvu hii hii tuliyoitumia Kushadadia Ajali ya Ndege huko kwa Watani zangu Wahaya Kagera ( Bukoba ) na hasa hasa Kumshadadia Muokoaji Majaliwa basi tuitumie pia katika Kuzungumzia Janga Kubwa lililoko la Njaa, Ukame, Umasikini na Uchumi mbaya kuliko wengi wenu mnavyojua au mnavyodhani.

Naomba kila mwana JamiiForums kuanzia sasa apaze Sauti juu ya Climate Change na popote alipo ahimize Utunzaji wa Mazingira ili Ukame upungue, mvua zianze Kunyesha ili hali isiendelee kuwa mbaya na wapaze Sauti zao popote walipo kwa Watanzania kutokuuza Vyakula vyao Nje ya Nchi kwani wenye Maono tumeshaona kuwa kunaenda kuwa na Janga Kubwa la Njaa, Magonjwa na Watanzania ( wana JamiiForums wengi ) Kufariki kwani Njaa huwa haiangalii Wewe ni Great Thinker au Komando.

Kwa mtakaonielewa mbarikiwe mno.
Umekosa maji ya kuoga asubui eee
 
Ndiyo maana kutokana na Upumbavu huo kuna muda huwa naona hata Aibu Kujinasibu ( Kujitaja ) kuwa Mimi ni Mtanzania kwani najiona kabisa kuwa sina IQ ya Kitanzania bali nina IQ ya Kiyahudi na Kitutsi tupu ambazo kwa 100% ni za Watu very Intelligent duniani.
Kwa hapo, nimepishana nawe, juu ya Ututsi au u jews. Watutsi wangekuwa na IQ wangevuta kurefusha atenna za kike? Wasingeingia kwenye mauaji ya kimbali kwa kuchonganishwa na white guys kupitia sauti za habari na udini.
 
Sahihi kabisa mkuu tuelekeze nguvu zetu kwenye vitu vya muhimu kwa sasa tuhimizane kutunza mazingira kwa kupanda mitii
Na mengine nayo yapewe nafasi kwa uzito wake
 
Back
Top Bottom