pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Matatizo ya msingi yanatatuliwa kupitia sheria ambazo zinatekelezwa chini ya katiba ambayo inaheshimika na wote. Acha nikupe mifano kadhaa ya hayo unayoyaita matatizo ya msingi ambayo yametatuliwa chini ya katiba mpya ya Kenya. Ubaguzi dhidi ya wanawake likija kwenye suala la kumiliki mali. Haki za wananchi likija kwenye suala la huduma bora bila ubabaishaji wala ubaguzi kwenye taasisi za umma. Kujumuishwa kwa mwananchi wa kawaida kwenye maamuzi yanayomhusu kupitia bunge za mashinani na pia kwenye kura za maamuzi. Wananchi mashinani kuwezeshwa kujiamulia wenyewe maendeleo wanayoyataka kwenye county zao kupitia 'public participation', hili limewekwa wazi kwenye sheria. Mhimili wa mahakama kuwa na nguvu za kubatilisha maamuzi hata yawe ya nani. N.K.Nchi za kijinga kijinga ndizo zinazokurupuka na kutuhumu katiba. Watu wanaojielewa wanashugulikia matatizo ya msingi ya nchi yao. Katiba will never solve the problems kama hakuna utashi wa kweli kwa viongozi.